Ushauri: Nataka nioe Binti wa Kishua

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Habari za siku ndugu wanafamilia wa JF!, Poleni na Majukumu Mazito ya kifamilia na ya kutafuta Mkate wa Kila siku hasa kwa awamu hii ngumu ya 5.

Naomba nianzie hapa..

Kwanza kabisa mimi ni kijana wa Miaka 28 mwenye elimu ya shahada moja, katika harakati za maisha nilifanikiwa kukutana na binti mmoja miaka takribani 6 iliyopita, Nilitokea kupendana naye sana.

Huyu binti ni mtoto wa kishua ukilinganisha na familia yetu.. mara nyingi amekuwa akinisumbua katika mahusiano yetu(Hakuwahi kuonesha kunicheat).. hasa kwa kutaka breakup za ghafla ambazo anadai mzee wake anamshinikiza aachane na mimi.. huwa natulia anajiachisha kisha anajirudisha (Mapenzi yake kwangu hayakupungua mpaka hivi sasa naandika uzi huu).

sasa kwa kipindi chote tumekuwa tukipanga kuoana.. ila ninachogundua ni kwamba binti yupo tayari kishingo upande.. yaani ananipenda ila akifikiria status ya familia yangu haifanani na ya kwao anarudisha moyo wake nyuma ghafla na hata kutaka kubreakup.. akijisahau hurudisha mapenzi na ananipenda kama kawaida.

Kwa sasa imefika wakati ambao hata mimi nimeanza kuchoka na mwanamke ambaye hatabiriki..leo hivi kesho vile.. nataka nioe, Japo favorite option ni yeye.. Nampenda huyu mwanamke.. ila kigezo cha yeye kuwa kishua na kuonekana kutoridhika na hali ya kwetu kinanipa wasiwasi endapo kama huyu binti ataweza kunivumilia au la..(i'm sure of being financialy free)

Kuna wakati akipitiwa hujisahu na kuropoka kabisa kuwa baba yake hapendi aolewe na mimi na mara kadhaa amemsihi asiwe hata na mahusiano na mimi.. nikiwa naye haya maneno najifanya kuchukulia kirahisi but kiukweli ni maneno mazito.

Ndugu zangu.. mimi kama mtu mzima sasa.. nina uwezo wa kufanya mbinu zozote(Hata kwa Figisu) za kumuoa tu awe mke wangu.. ila je madhara ya kuwa na mke wa aina hii itakuwaje? ..kwa maana sitaki familia isiyo na Amani ...mtu ambaye mzazi wake hataki awe nami.. na kwa kiasi kikubwa hata kama ananipenda ameonesha kumsapoti mzee wake.

Ndugu zangu wanafamilia wa JF tumetofatiana uzoefu achilia mbali kuzidiana mitazamo.. ni matumaini yangu kuna watu wenye uzoefu na matukio ya aina hii.. naombeni mnipe ushauri kwa nyinyi wenye uzoefu..je kuna madhara gani kumuoa mwanamke mwenye situation kama hiyo?.. Je unashauri nimuoe au Niache?.. Je una maoni gani ya kudeal na situation ya aina hii?

Asanteni Sana

Khan
 
Achana nae hafai kuoa, tafuta mtu unayeendana naye status, na ivyo anavyolalamika eti Baba yake hapendi muoane, anyway dalili za mvua ni mawingu ,
 
Angekua na msimamo ningekushauri ushikamane nae ila kwa kua ni tofauti nashauri vice versa. Hakuna kitu kinabore kama kuwa na mpenzi asiye na msimamo. Akiambiwa na ndugu hivi anafata, akikutana na marafiki wanaotaka vile atafata mradi hajielewi nini anataka. But mwisho wa yote kupanga ni kuchagua na muamuzi wa mwisho ni wewe.
 
Achana nae hafai kuoa, tafuta mtu unayeendana naye status, na ivyo anavyolalamika eti Baba yake hapendi muoane, anyway dalili za mvua ni mawingu ,
Thanks.. nilipata haya mawazo..ila sikutaka niconfirm.. Asante kwa ushauri!
 
Angekua na msimamo ningekushauri ushikamane nae ila kwa kua ni tofauti nashauri vice versa. Hakuna kitu kinabore kama kuwa na mpenzi asiye na msimamo. Akiambiwa na ndugu hivi anafata, akikutana na marafiki wanaotaka vile atafata mradi hajielewi nini anataka. But mwisho wa yote kupanga ni kuchagua na muamuzi wa mwisho ni wewe.
Asante Ndugu.. ushauri murua Kabisa..
 
Tafuta level yako mkuu, huyo dem hajakupenda. Mwanamke akikupenda asee atafanya kila kitu awe na ww, sisi tunao experience haya mambo tunajuaa.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Habari za siku ndugu wanafamilia wa JF!, Poleni na Majukumu Mazito ya kifamilia na ya kutafuta Mkate wa Kila siku hasa kwa awamu hii ngumu ya 5.
Pole sana ndugu kwa mkasa huo, kama kuna safari ngumu isiyo na masahihisho ktk maisha ni safari ya ndoa unayotaka kuianza na mtu ambaye ana kigugumizi cha safari, yaani yeye yuko mguu nje mguu ndani ktk suala la ndoa, alafu kingine ktk maisha kila jambo lina uzito wake na kila mtu kwa mtu mwingine ana uzito wake, kwa tafsiri iliyo logically ni kuwa wewe huna nguvu kwake kama ilivyo kwa familia yake, inaonekana familia yake ina uzito mkubwa sana ktk akili yake kuliko malengo ya ndoa au uzito wa kutaka kuishi na wewe.

Wazazi wake hasa baba yake ana nafasi kubwa sana katika maamuzi yake kuliko malengo yako, nyakati zingine toa nafasi ili ujue mwelekeo wa malengo yenu yanaelekea wapi, kuanza kuchoka kwa tabia zake ni ishara ya kuanza kuelewa kuwa nafasi yako ktk maisha yake ni ipi na kutambua kuwa kama utamuoa una kazi ya ziada ya kuondoa ujinga huo ulio kichwani mwake, nilishwahi kusema na narudia tena kusema, wazazi wengi wanahisi wanakuza watoto kumbe hawatambui kuwa wanakuza wazazi wa baadae.

Ikwa yeye anaona familia yake haipendezwi na yeye kutaka kuolewa na mtu mwenye hali ya kawaida (kwa sasa hivi) basi awe muwazi na msimamo wake kuwa yeye asimamie wapi kuliko kuwa leo nyeusi kesho nyeupe mara nyekundu mara rangi ya maziwa, apo utashindwa kujua ipi ni ipi, na kingine kuvumilia mtu mwenye misimamo miwili miwili nayo ni changamoto kama sio shida, kama anaamua moja na aamue kwa moyo mkunjufu, umri unakimbia na wewe wahitaji familia, kukaa na mtu asie eleweka nalo ni tatizo pia, kazi na maamuzi yako mikononi mwako, kuna formula moja vitani inasema hivi

"Ukiona askari mwenzio analega lega wakati mapigano yamekolea kiasi cha kuhatarisha uhai wako na uhai wa platoon kama sio section basi mpige risasi ya kichwa ili mpate kusonga mbele". Nadhani kazi iko kwako kuamua nyeusi iwe ipi ama nyupe iwe ipi.
 
Tafuta level yako mkuu, huyo dem hajakupenda. Mwanamke akikupenda asee atafanya kila kitu awe na ww, sisi tunao experience haya mambo tunajuaa.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Asante mkuu.. Japo ni ngumu ila inabidi..
 
POLE SANA NDUGU KWA MKASA HUO, KAMA KUNA SAFARI NGUMU ISIYO NA MASAHIHISHO KTK MAISHA NI SAFARI YA NDOA UNAYOTAKA KUIANZA NA MTU AMBAYE ANA KIGUGUMIZI CHA SAFARI, YAANI YEYE YUKO MGUU NJE MGUU NDANI KTK SUALA LA NDOA, ALAFU KINGINE KTK MAISHA KILA JAMBO LINA UZITO WAKE
Asante sana Ndugu yangu, ushauri murua sana huu..
 
Huyo demu ata ukioa kwa kufosi akili ishalala nyumban na maana Mzee wake ndo last decisions controller madhara ni mengi sana kuna kudhalilika kutengwa na mengineyo.
 
Huyo demu ata ukioa kwa kufosi akili ishalala nyumban na maana Mzee wake ndo last decisions controller madhara ni mengi sana kuna kudhalilika kutengwa na mengineyo.
Hili la kutengwa linaonekana lipo wazi..
 
Back
Top Bottom