Ushauri: Nataka nimtambulishe boss mpenzi wangu ili apunguze mazoea

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,557
45,827
Nilipata mpenzi huku mkaka moja mzuri tu mwana JF, anaonekana ni mtu mwema japo ana mambo yake flani ila nimempa tu muda hata mimi najijua nina madhaifu yangu. Nina boss wangu, yule mzee ananipenda sana kama binti yake anajua sina mwanaume yoyote ananichukulia kama binti mwenye heshima tu na maskini kwaiyo ananilipia kodi, pocket money za hapa na pale.Tena anataka nikakae kwake inshort napata full sponsorship hapa mjini.

Sasa natamani nimtambulishe huyu mpenzi wangu ili asiwe ananichukulia kirahisi kivile ila naona kama udhamini utakoma. Hajawahi kunitaka kimapenzi na najua anajiheshimu sana wala hatokaa anitake ila nataka kuwa huru na maisha yangu.

Kwa situation hii nifanyeje wadau?
 
Haha...wa jf now karoho kanadunda anaombea kura ziangukie kwake.
Mpe mwenzetu bhna....
 
1. Mpenzi wako umemfahamisha yote haya unayotueleza na yuko tayari kushirikiana majukumu kama donna funds zikistop?
2. Utaendelea kumtegemea mzee mpaka lini? Hatuombei lakini Mungu akimchukua una chako tena kwenye biashara zaidi ya mke na watoto?
3. Umeshawahi kuwaza kuwa na wewe unahitaji mume na watoto na mzee anaweza kukupatia vyote hivyo?
 
kuhusu namba moja sijui yeye mwenyewe kama ataweza ila nafanya kazi
namba 2 na tatu nawaza sana ndo maana naitaji ushauri
 
Hakuna anaekupa vya bure bila kutegemea kitu kutoka kwako hata akuchukulie vipi. Kama kweli mwema na hataki kitu kwako basi angelisaidia jamaa zake wote kwanza kabla ya kukupa wewe huo msaada. Eti halafu ukakae kwake mmhh really Ukimtambulisha huyo mpenzi wako utakosa vya bure na kazi itayeyuka pia.
 
kazi sitakosa ila madikodiko yatakuwepo kweli?
 
kuhusu namba moja sijui yeye mwenyewe kama ataweza ila nafanya kazi
namba 2 na tatu nawaza sana ndo maana naitaji ushauri
Hilo namba moja angalia jamaa ana mpango gani na wewe, si ajabu umeanza kujenga castle kichwani na ndani ina wafanya kazi, watoto na wewe ni mke na pete kidoleni kumbe mwenzako huko hajafika.
 
kwa fastafasta kitendo cha kusema *udhamini utakoma* inamaanisha kwamba ur bf hana uwezo wa kukudhamini, na kama anao basi unataka uwe unachota huku na huku. chunga tamaa mbaya.
 
Nilipata mpenzi huku mkaka moja mzuri tu mwana JF, anaonekana ni mtu mwema japo ana mambo yake flani ila nimempa tu muda hata mimi najijua nina madhaifu yangu. Nina boss wangu, yule mzee ananipenda sana kama binti yake anajua sina mwanaume yoyote ananichukulia kama binti mwenye heshima tu na maskini kwaiyo ananilipia kodi, pocket money za hapa na pale.Tena anataka nikakae kwake inshort napata full sponsorship hapa mjini.

Sasa natamani nimtambulishe huyu mpenzi wangu ili asiwe ananichukulia kirahisi kivile ila naona kama udhamini utakoma. Hajawahi kunitaka kimapenzi na najua anajiheshimu sana wala hatokaa anitake ila nataka kuwa huru na maisha yangu.

Kwa situation hii nifanyeje wadau?
Mwenyew unaonaje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom