Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

Mkuu angalia maelezo yake ni kama anatumia Mshahara kukopa kama ndivyo achukuapo hela mwezi huo huo wanaanza kukata pia kumbuka amesema ndio anaenda kuanza biashara so ktk hicho kipindi utaulipa vipi huo mkopo?
Atalipa na biashara yake. Ujue si kweli kwamba huwezi kopa kuanzisha biashara.

Kikubwa ni kuwa na Plan nzuri watu wanakopa wanaanza biashara freshi kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasumbiwa na uoga na kuona kuajiriwa ndo Dili sana. Wewe huna kazi na muda wako? maana ya kuajiriwa ni kwamba wewe Muda ulio pewa na Mungu huna kazi nao bali inabidi uwapatie vichwa ambao ni risk taker wafanyaie kazi.

Endelea kubinasifisha muda wako kama Madini.

Sent using Jamii Forums mobile app
ndio maana duniani kuna machaguo ni kama ilivyo producers na consumers ukisema wote muwe wazalishaji wananuaji watatoka wapi.ni lazima wengine waajiri na wengine waajiriwe! kwa kubaliana na chaguo hilo lazima uchukue hatua ya ku forego baadhi ya vitu,hata wewe katika kujiajiri kwako kuna vitu ambaye aliyeajiriwa anavipata huku wewe huvipati
 
Pia lazima ujue hiyo pesa unayopata ni mkopo utakalipwa na kitu gani?, sio huo mshahara ndio utakalipa huo mkopo?.
Fanya biashara ukiwa kazini. Na katika hiyo pesa chukua silimia 25 ndio uwnze hiuo biashara kilichobakia kiwe kipo kuangalia uimara wa hiyo biashara, na utakuwa ukiongeza mtaji kadiri biashara inavyoimarika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hivi ndugu hakuna mtu aliyekuwa tajiri kupitia kuajiriwa,
Wazo lako la kujiajiri ni zuri ila jinsi unavyotaka kufanya jipange vizuri.
Mi mwenyewe nipo ngambo huku nasomeshwa na Serikali shule ikiisha sirudi tena job
 
Pia lazima ujue hiyo pesa unayopata ni mkopo utakalipwa na kitu gani?, sio huo mshahara ndio utakalipa huo mkopo?.
Fanya biashara ukiwa kazini. Na katika hiyo pesa chukua silimia 25 ndio uwnze hiuo biashara kilichobakia kiwe kipo kuangalia uimara wa hiyo biashara, na utakuwa ukiongeza mtaji kadiri biashara inavyoimarika.

Sent using Jamii Forums mobile app
mshika mbili moja humponyoka wahenga walisema huwezi kuwa wa moto na uvugu vugu-watu wengi wana fail maishani kutokana na kutaka kuwa kotekote fanya moja ukiweza ujue umeweza na uki fail ujue ume fail
 
usichukue hela ya mkopo ukaanzie biashara .. utapotea .. tafuta hela yako mwenywe isiyokua na riba wala ya kudaiwa .. biashara yeyote mwanzoni lazma iwe ngumu .. mbka uje kukomaa kibiashara unaweza ukawa ushadondoka mara nyingi kifedha .. nakushaur pia usiache kazi .. tafuta hela yakwako mwenywe na ufanyie kazi .. mweke mtu akusimamie mbka pale biashara itakapokomaa ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu mpendwa....mawazo kama hayo....unatakiwa uwe unayajadili mwenyewe na kuyafanyia maamuzi mwenyewe juu kwa juu.....huku ukijiweka tayari kukabiliana na changamoto za maamuzi yako.......

Maamuzi kama haya yanayohusisha mustakabali wa maisha yako Wewe ndio muamuzi sahihi kwa kadri unavyoona inafaa maana wewe ndio mhanga wa yale yanayoendelea maishani mwako...........

d94539673262020c82c1e76b2a04967e.jpg
471a44a095569c9e8337bbd5471d45bc.jpg
131c213a8987b8983300f88722ff4ded.jpg
 
Kujiajiri ni wazo zuri sana, siyo rahisi kufanikiwa maishani kwa kutegemea ajira.

Siwezi kusema idea yako kama ni nzuri au laa, watu huwa wana suggest kukopa kuendeleza biashara na siyo kuanzisha biashara.
Ila sometimes mtu huna option hiyo. Hatujui ni biashara gani unataka kuanzisha, au hata wewe una nidhamu kiasi gani kwenye hela, maisha na biashara, so kukwambia ufanye au usifanye ni kubahatisha.

Mimi niliacha kazi mwaka jana mwezi 7 na kuanzisha kampuni yangu. Mwanzo huwa ni mgumu, hasa kwa sababu ya expectations.
Ukiwa una plan biashara huwa tuna assume baada ya muda flani itaanza rudisha hela, mara nyingi haiwi hivyo.
So ushauri wangu, kuwa realistic kwenye expectations na pia like me nilinunua bodaboda kuingiza hela za kula nikiwa napambana na kampuni (ingawa bodaboda nayo inataka dereva mzuri, luck for me, wangu azingui)
All in all, panga, pangua, panga tena, kuwa na plan B na tafuta muda kwa namna yoyoye ile do research. Jifanye mwehu tu, zunguka uliza watu depending na biashara unayotaka kufungua.

Watu wengi wenyeelimu au waajiriwa tuna fail kuingia kwenye biashara kwa sababu tuna overthink. Tunawaza mno, tuna run scenerios nyingi, mara nyingi either zina tukatisha tamaa au tuna poteza interest, unakuja kushtuka darasa la 7 anakupita kimaendeleo.

All the best aisee. Biashara ndo mpango mzima. So far sijutii kuacha kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana mkuu kwa kutoa maelezo yenye maana yanayotokana na experience yako. Hii imenisaidia hata mm japo sio mwanzisha mada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja na Mimi nitoe mawazo katika ubongo wangu.

1.usiache Kazi.
Kazi inakuwa back up ya biashara yako,sababu biashara inatoa faida na unazitumia,but sometimes ina kuwa vice versa biashara itagota and itahitaji wewe uzame mfukoni utoe pesa yako kuikwamua biashara yako.
So don't dare dear brother kuacha Kazi yako.

2. Mkopo hatuanzishiagi biashara,Bali mkopo tunaendelezea biashara hayo ni mawazo ya kijasiliamali zaidi and since I'm let's share the bread. So,kama una mtaji wako we anza Naona tu brother,now days Hata kilimo sometimes kinazingua watu wanalima matikiti maji au vitunguu wamebaki navyo mashambani.
So,
i. Fanya tafiti ya biashara unayoitaka. Ili ujue una invest kiasi gani,then unaihudumia vipi mpaka ianze kutoa faida na zipi changamoto zake.
ii. Baada ya kufanya tafiti ya biashara then jitafakari wewe na ulicho nacho,wengine wanasema million 10 ni ndogo,brother hiyo ni ela Kubwa kwangu Mimi kama mjasiliamali hakuna ela ndogo. Inategemea na unchokifanya,malengo na utakachokifanyia.
iii. Ukishatafakari hayo then sasa chukua Hatua kama uingie mazima au unachange plans.
Usisahau kumuomba Mungu akusimamie katika mipango yako.

All in all don't quite the job bro. All the best. With it you can shine.
 
Kama risk ya biashara husika ni ndogo, kwa maana kuwa unaijua vzr, na labda una mentor, kopa, acha kazi anzisha.. Ila kama ni mambo ya kubahatisha, jipe muda, komaa na kibarua tu ujichange mwenyewe kwanza
 
Swali dogo tu kwako mtumishi kabla ujaacha kazi je ulishawahi kuchukua mkopo wowote ule angali ukiwa mtumishi? Je kama uliuchukua uliufanyia nini? Kama ukuchukua uliogopa nini?

Mtumishi amini hakuna kazi mbaya ni wewe tu mtazamo wako fikiria hiyo ajira yako inakupa uwezo wa kukopa milioni kumi huoni ajira yako ni zaidi ya biashara ukitulia vizuri, ulizia wafanya biashara ambao unataka ukaifanye hiyo biashara je biashara zao zinaweza kuwa dhamana benki wakapewa milioni kumi?

Kabla ujaacha kazi ulizia wafanyakazi wenzako ambao unamini pamoja na changamoto za kazi yenu ila wao wanafurahia maisha na wanasonga mbele kimaisha


Jambo jingine nyie watumishi mnafanyaga mipango yenu siri sana hampendi shirikisha watumishi wenzenu mnasahau wapo wenzenu umo makazini umri mdogo mnaona kama wajinga ila wana experience ya maisha na utafutaji zaidi yako
 
Tatizo wabongo sometimes tunaamini kufanya biashara ni mpk iwe mashamba,mara kilimo cha tikiti,mara kufuga Sungura/Kware au kumiliki duka.

Hivi kwani kwa kama mtu ni Mwanasheria kwanini asifungue firm yake,mhasibu na yeye hivyo hivyo na engineer awe na Co. Yake au huko siko kujiajiri?

Nb:inaweza isiwe applied kwa Mtoa mada.
 
Tibaijuka alipewa bilions za escrow ila bado anakomaa kuomba ajira ya ubunge

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu habari za majukumu.

Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.

Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.

Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.

Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.

Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.

Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.

Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.

Natanguliza shukrani.

BAKI KWENYE KIBARUA CHAKO MKUU

Niliwahi kuandika nyuzi apa yenye kichwa UZUSHI/UPOTOSHWAJI UNAOHUSISHWA NA UJASIRIAMALI, nilipata critics nyingi hasa kwa watu wasioelewa au pengine wamepotoshwa au hawajui na wala sio wajasiriamali.

Nimehusunisha uzi huo na hiki kinachokusibu ww, apa ushauri uliotolewa mwingi ni wa watu waliosikia au kusoma kuhusu ujasiriamali kutoka kwa watu wasio wajasiriamali au nao ni wajasiriamali tayari lakini hawajui dhana ya uhalisia wake ulivyo.

Mengi yamesemwa lakini kwa ushauri wng ni kuwa BAKI KWENYE KIBARUA CHAKO, infact kuwa mpole tu hata usidiriki kukopa na kufanya 'side husle/business' utalia charii.

Baki kwenye ajira yako maana unachokitafuta au kinachokusukuma kukimbilia ujasiriamali hutokipata na kwa ukweli ulivyo ni bora ubaki kibaruani. Nime highlight sabab zinazokufanya utake kuwa mjasiriamali na kwa hakika kama dhumuni lako ni kuchoka kupelekeshwa, kufanya kazi nyingi na kupata maslahi duni..huku chalii ni kwamba utafanya kazi kubwa tena kubwa na unaweza usipate malipo(faida) ata kwa mwaka mzima.

Unasema unataka uhuru, unafanya kazi masaa 11/12 jaribu kutizama mtu kama Elon musk au Marc Cuban hawa jamaa wanafanya kazi zaidi ya masaa 17-19 kwa siku, sasa ww 11 hrs zinakuchosha..fikiria mara mbili.

Anyway ya kuambiwa changanya na yako, ila kama sabab ni hizo zinakusukuma kutaka biashara/ujasiriamali nafikiri unahitaji kufikir zaid na kuwa na motive kubwa zaid ya hizo maana huku shuruba ni marambili zaid ya hizo kazini.

Kila la kher, kumbuka Men who do not have goals are doomed forever to work for these who do have goals.
 
Ndugu yangu mpendwa....mawazo kama hayo....unatakiwa uwe unayajadili mwenyewe na kuyafanyia maamuzi mwenyewe juu kwa juu.....huku ukijiweka tayari kukabiliana na changamoto za maamuzi yako.......

Maamuzi kama haya yanayohusisha mustakabali wa maisha yako Wewe ndio muamuzi sahihi kwa kadri unavyoona inafaa maana wewe ndio mhanga wa yale yanayoendelea maishani mwako...........

d94539673262020c82c1e76b2a04967e.jpg
471a44a095569c9e8337bbd5471d45bc.jpg
131c213a8987b8983300f88722ff4ded.jpg
Mkuu point sana.

Umeingea point. Humu atatiwa uoga wa kufa mtu.

Ukitaka usifanye jambo basi anza kutafuya washauri kamwe hutafanya na ndo kinacjo fuata kwa huyu jamaa.

Humu wengi ni waajiriwa how come mwajiriwa amshauri mtu aache kazi? Never hapen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom