Ushauri: Nataka mtoto wa mdogo wangu nimsomeshe, shangazi yangu anakataa

Kama ako 18 tayari ni mtu mzima.. Mwambieni achague yeye anataka aishi na wewe au la...

Kaa nae ongea nae atakuelewa tuu kama ni mtoto anaejitambua, achague analoona lina faida kwenye maisha yake ya baadae
Yaan nlikua nataka niseme ivi
Ila umeniwahi tuu......
 
Eid Mubarak Waungwana...

Nnaa jambo linanitatiza kichwa na sijui hata niamue vipi,
Mtoto wa shangazi yangu amefariki amewacha watoto wa5,lakini kabla ya kufariki mtoto wa shangazi niliongea na Dad kua nimejisikia vibaya kuona hali nilomkuta sasa nikamwambia Dad wacha nimchukue huyu mtoto wa kike as niko na watoto wa kike nisingependa kumuona mtoto
yule anakulia kwenye mazingira ya ajabu, dad kasema sawa, siku ilofatia nika omba shangazi aje Dad na mtoto wa shangazi yangu mkubwa wa yule mgonjwa,nikamuomba mgonjwa kua anipe mtoto nimsaidie kulea na mimi ndio ntakua responsible kwa chochote cha yule mtoto sio yeye tena
kuanzia shule na maisha yake yote,masikini hakukataa baada ya 2days akafariki,mimi nikawa nimesha chukua jukumu.
Baada ya mazishi watu wakagawana watoto mimi nikasema huyu mmoja ananitosha,wakabakia wa4 dad akachukua2kids na 2 wakawa kwa bro, sasa jana huyu mtoto mkubwa wa shangazi amekuja anasema amekuja kumchukua huyu bint nnae kaa nae anataka kuishi nae na mtoto yuko shule na wenzie anasema atampeleka shule akajifunze Hotel managemnt she is only 18yrs na mtoto ana valishwa ma baibui ana banwa mtu na shape yake mimi namfunga funga,shangazi nimemwambia hasemi kitu Dad anasema mpe jamani huyu mtoto ataharibika as huyu mtoto wa shangazi watoto wake hakuna hata alomaliza hata la 7 iweje leo akamsomeshe mtoto wa mdogo wake,kwenye issue kama hii wapi niende as huyu Bint atapotea nahitaji msaada,sina shida ya wa toto nnao wangu 6 Alhamdulillah ila huyu anahitaji kusoma sio kwenda kumufanya akawa hana maisha najisikia vibaya sanaaaa... au niwache kama ilivyo? na jee huyu mtoto akisha haribika nani atakua responsible as she is only 18 nahitaji msaada wenu wa mawazo please..
Hapo nimekupeni kwa ufupi ili nisiwachoshe...
Kama marehemu alikuachia wewe
Basi wewe ndo uko responsible nae
Kabla hajafa alikuachia huyo wewe, kumbuka hilo
 
Sasa mbona teyari unafahamu nn kinachofata...we madam ulishachukua jukumu la kumsomesha vp sasa umpe mtu mwingine??halafu huyo ameshakuwa mtu mzima mwelimishe achague mwenyewe inawezekana we unataka asome kumbe mwenzio anawasiliana na huyo shangazi ako aje amchukue akaishi nae..ila na wewe kama miezi uliyekabidhiwa mtoto na marehemu una final say juu ya mtoto..
Mkuu mtoto wa 18yrs hata kama anawasiliana nae aje amchukue lakini huwezi kukubali anavyotaka mtoto sababu kwangu
rules za mtoto kutembea bila baibui hakuna lazima uvae baibui au hata tukiwa tumesafiri nje unaweza kuvaa nguo yako ya heshma na mtandio kichwa, sasa uenda anamjaza ujinga kua wale washamba njoo huku nikupe freedom,lakini sio kama anampenda yule mtoto,mtoto nimemuliza amenyamaza kimnya nimemwambia afikirie wala asiniogope ikisha Eid tutaongea..
 
Mrembo she is 18 lakini namchukua same as my Daughter siwezi kusema mtoto wangu she is 18 ndio amekua aamue anachotaka sio sawa yule mamake mkubwa ni muharibifu tuu,shule mbona hakupeleka wanawe? na wakati namchukua mbona hakusema ntamlea mimi? au wale wa4 why asichukue mmoja why huyu nnae lea mie? anajua she will have bright future as nxt year wanakwenda Toronto kusoma sasa hapendi maendeleo ya huyu mtoto thats what i can see,manake silioni..
Mmhh kama ndo ivyo komaa ubaki nae tuu utaonekana m'baya sasa ivi lakini baadae watakushukuru
 
Najitahidi,ila what i see hapa huyu mtoto nae anataka kwenda manake nimemuliza hakusema kitu amenyamaza..
Hata kama ana 18 years mwambie kabisa ushauri atakao uchukua sasa ivi kuna mawili aujutie maisha yake yote au aufurahie..... Mshauri tuu kama mtoto mwambie kwa heshima ya kumuenzi mama yake abaki tuuu
Miii binafsi nmeanza kuina Giza mbele yake kama ataondoka
 
Mkuu mtoto wa 18yrs hata kama anawasiliana nae aje amchukue lakini huwezi kukubali anavyotaka mtoto sababu kwangu
rules za mtoto kutembea bila baibui hakuna lazima uvae baibui au hata tukiwa tumesafiri nje unaweza kuvaa nguo yako ya heshma na mtandio kichwa, sasa uenda anamjaza ujinga kua wale washamba njoo huku nikupe freedom,lakini sio kama anampenda yule mtoto,mtoto nimemuliza amenyamaza kimnya nimemwambia afikirie wala asiniogope ikisha Eid tutaongea..
Sasa hapo unaeza pata picha ya haraka haraka ya huyo mtoto...kumuuliza na kukaa kimya kuna kitu hapo anamaanisha....je alipokuwa kwa mzazi wake alikuwa na malezi ya namna hyo unayo mpa wewe?mfano huo uvaaji wa kujistiri ambao nakuunga mkono kwa 100%...muelimisha kwa maswali rahisi tuu mfano huyo anayemtaka ampe uhuru watoto wake alio walea kwa uhuru wamefikia wapi??Sasa kama ana akili atachagua mwenyewe dhahabu ni ipi na makinikia ni ipi..ila kama ndo sikio la kufa.......
 
Mrembo she is 18 lakini namchukua same as my Daughter siwezi kusema mtoto wangu she is 18 ndio amekua aamue anachotaka sio sawa yule mamake mkubwa ni muharibifu tuu,shule mbona hakupeleka wanawe? na wakati namchukua mbona hakusema ntamlea mimi? au wale wa4 why asichukue mmoja why huyu nnae lea mie? anajua she will have bright future as nxt year wanakwenda Toronto kusoma sasa hapendi maendeleo ya huyu mtoto thats what i can see,manake silioni..
Mmmmh
 
Mkuu mtoto wa 18yrs hata kama anawasiliana nae aje amchukue lakini huwezi kukubali anavyotaka mtoto sababu kwangu
rules za mtoto kutembea bila baibui hakuna lazima uvae baibui au hata tukiwa tumesafiri nje unaweza kuvaa nguo yako ya heshma na mtandio kichwa, sasa uenda anamjaza ujinga kua wale washamba njoo huku nikupe freedom,lakini sio kama anampenda yule mtoto,mtoto nimemuliza amenyamaza kimnya nimemwambia afikirie wala asiniogope ikisha Eid tutaongea..

Naona dalili ya dogo mwenyewe kuamua kutemana na wewe.

Punguza ukoloni pia, being strict kwa hawa teenagers wa kizazi hiki siyo solution kabisa.
Lazima uende nao katika namna ya kisaikolojia na kiakili kuwateka katika malezi yao na siyo misheria sheria tu
 
Hayo mambo ni ya kifamilia zaidi nadhani hivyo mnaweza kulimaliza kifamilia, hebu wekeni kikao cha kifamilia mueleweshane vizuri then mfikie muafaka. Ila zingatieni wellbeing ya hao watoto maana nimeshuhudia ndugu wakigombania watoto wa ndugu yao anapofariki kumbe watu wanatafuta tu house help baasi walaa hawana habari na watoto, mwisho watoto wanateseka sana.
 
Mkuu mtoto wa 18yrs hata kama anawasiliana nae aje amchukue lakini huwezi kukubali anavyotaka mtoto sababu kwangu
rules za mtoto kutembea bila baibui hakuna lazima uvae baibui au hata tukiwa tumesafiri nje unaweza kuvaa nguo yako ya heshma na mtandio kichwa, sasa uenda anamjaza ujinga kua wale washamba njoo huku nikupe freedom,lakini sio kama anampenda yule mtoto,mtoto nimemuliza amenyamaza kimnya nimemwambia afikirie wala asiniogope ikisha Eid tutaongea..
Pamoja na yooote, sijui kumpa uhuru aamue sijui nini wewe ndo utakayemuokoa huyo binti. Kwa sababu inaonyesha huyo bwana anataka kumchukua harafu amfanyie mishe za kumpatia mwanaume apate pesa. This is true wala hamna kupindisha hapa.
 
Naona dalili ya dogo mwenyewe kuamua kutemana na wewe.

Punguza ukoloni pia, being strict kwa hawa teenagers wa kizazi hiki siyo solution kabisa.
Lazima uende nao katika namna ya kisaikolojia na kiakili kuwateka katika malezi yao na siyo misheria sheria tu
Neno zuri pia!!
 
Kuna vitu vingine hapa duniani unafanya tu haviitaji ushauri kbs as long as ur doin the ryt thng
 
Back
Top Bottom