Ushauri nataka kumiliki Nissan Dualis

stackoverflow

Member
Jul 10, 2019
20
15
Wakuu kwema. Baada ya kujichanga changa nimeamua sasa nitafute usafiri. Hii Nissan Dualis nimeielewa sana japo siijui kiundani sana kutokana sio nying mtaani. GARI INA CC 1990

NAOMBENI USHAURI JUU YA HII GARI KUANZIA MATATIZO YAKE NA ULAJI WA MAFUTA. Baadhi ya watu niliowauliza wameniambia hii GARI Haifai inakunywa sana Mafuta je Nisahihi?

Kuhusu Upatikanaji wa spare Ntapambana tuu

1150978
 
Imekaa kama Murano new model... Nissan model nyingi ziko vizuri sana ila zina anasa moja au mbili zinazowatesa wengi... Ulaji wa mafuta na spare kuwa juu.

Hivyo chukua lakini kuna hayo niliyotaja hapo yazingatie. Lakini kama ukizingatia kanuni zake utaishi nalo vizuri tu
 
Imekaa kama Murano new model... Nissan model nyingi ziko vizuri sana ila zina anasa moja au mbili zinazowatesa wengi... Ulaji wa mafuta na spare kuwa juu
Hivyo chukua lakini kuna hayo niliyotaja hapo yazingatie
Lakini kama ukizingatia kanuni zake utaishi nalo vizuri tu
ASANTE BOSS KWA USHAURI WAKO. Shukran sana
 
Kagari hua kana sura mbaya sana,sijui hata umekapendea nini.

Anyway kipendacho roho,all the best boss.
 
Kwa mujibu wa Jamaa mmoja mweny showroom ameniambia inafika mpaka 14Km/L Naomba usahihi wa hizi Taarifa kwa anayejua zaidi ... Hii ni kwa 2WD

NISSAN DUALIS

Grade20G

ModelKJ10

Registration2008/10

Body ColorBlack

Manufacture2008/09

TransmissionAutomatic

Mileage 43,585

Drive2wheel

Engine Size : 1990

Fuel :petrol

StatusIn-Stock

SteeringRight

Doors5

Seats5

Fuel Consumption14.2km/L

OptionsAC | PS | PW | AB×2 | ABS | AW | SR | AUDIO |
 
stackoverflow,

Cc 1990 kuleta consumption ya 14.2km/l ni impossible.

Cheki hata magari kama grande mark 2, cresta, verossa etc zenye cc 1990 utaona kwny review wanakwambia inaenda 100km/8litre ila aanza kuitumia sasa kwny mishe mishe za kila siku ndio utajua kwanini watu wanakimbilia IST.

Nb:Najua naongelea engines za co. 2 tofauti, toyota vs Nisssan lkn in general kwa cc hizo 14.2km/l ni impossible.
 
Kakudanganya...gari yangu ndogo ya cc 1500 ndiyo napata 14/15 kwa lita moja nikiwa highway..

Hiyo itakuwa 12km kwa L ukiwa highway...
Mishe mishe za mjini itashuka mpaka 8..

Hiyo gari ulaji wake ni sawa na x trail. stackoverflow,
 
Kakudanganya...gari yangu ndogo ya cc 1500 ndiyo napata 14/15 kwa lita moja nikiwa highway..

Hiyo itakuwa 12km kwa L ukiwa highway...
Mishe mishe za mjini itashuka mpaka 8..

Hiyo gari ulaji wake ni sawa na x trail. stackoverflow,
Uko sahihi kabisa. Ni sawa na Nissan x trail. Ukiwa long safari km 13.5 kwa lita moja ukiwa mjini ujue unatumia zaidi gia kubwa kwa hiyo akili kichwani.

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom