Ushauri: Nashindwa kumuelewa mama yangu mzazi

okonkwo jr

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
2,419
1,737
Habari sana ndugu wa jf? Natumaini hamjambo ,naomba niende kwenye hoja.

Mimi ni mtoto wa nne kuzaliwa katika familia ya watoto saba,mama na baba walitengana zamani sana hivyo kupelekea sisi kukulia kwa babu.Kiufupi katika watoto hao saba mwenye unafuu wa maisha ni Mimi lakini hawa ndugu zangu sita maisha yao si kihivyo kwani nikipatacho huwa tunagawana wawapo na shida.

Kiufupi baada ya kuajiriwa serikalini mwaka 2013 nilifanya kazi kwa miaka miwili baadae nikaamua kumjengea mama yangu mzazi nyumba,kwani nilikuwa nimeweka nadhiri ya kujenga nyumba ya mama kabla sijaoa wala sijajenga nyumba yangu,nikiri kuwa huyu ni mama tu na wala siwezi sema amehangaika kunisomesha wala mini hapana,kwani hata nilipokuwa nasoma sekondari alikuwa akinitamkia maneno ya kunikatisha tamaa,Mara ooh soma tu lakini hautafanikiwa lakini pia katika ndugu zangu wa kiume hakuna hata mmoja anayeelewana na mama maana ni MTU wa maneno na mpenda kijionesha kwa watu ili khali maisha yake ni magumu sana.


Nilipoanza kumjengea nyumba kwa kumpatia ramani na namna vile nyumba ilipaswa kuwa alinielewa,maana nilimwambia nataka nyumba iwe ya nyumba viwili na sebure na bati zisizidi 40,ikumbukwe kuwa wakati natoa maelezo hayo Mimi nilikuwa mbali kikazi hivyo sikuwa na muda wa kuja kuona kinachofanyika kwa mama zaidi ya kutuma pesa,cha kushangaza mama hakuzingatia maelezo yangu katika ujenzi ,na alicho kifanya alijenga nyumba ya vyumba vinne na sebure kubwa tu,kwani tofari zingine hadi alikopa ili kujengea hilo jumba.nilipopata likizo niliamua kwenda kwa mama ili ninunue bati na vifaaa vingine nipaue nyumba ile ,nilicho kikuta sikuamini ,nilipomleta fundi atathimini gharama aliniambia bati 80 na mbao 2500 zilikuwa zikihitajika,walahi nilitamani kulia, nikiri kuwa mama alinikera sana hadi nikakosa uthamani wake kwangu kwani kwa gharama zile nilikuwa kubwa ikizingatiwa kipato changu ni kidogo sana maana haizidi laki NNE kwa mwezi,japo nashukuru mungu huwa naweza kikumudu vilivyo na ilikuwa ngumu kwangu kendeleza ujenzi ,Kiufupi mama aliniudhi na nilikata tamaa.japo na Mimi ni binadamu na yule ni mama mzazi huenda yapo niliyomkosea lakini daah, imezidi.


Mwaka huu nilipata taarifa kuwa nyumba anayoishi mama yako imechoka na itaanguka wakati wowote,hivyo niliamua kumpigia simu mama kumuliza na nikamwambia mama kwa kuwa nyumba mlojenga ni kubwa na kipato changu ni kidogo kwani mshahara wangu hauzidi laki 4 nikiwa na tegemezi zaidi ya 50 naomba hiyo nyumba niiezeke kwa mfumo wa sloap ili uhame kwenye hilo jumba bovu Ila nikipata pesa tutaezua na kujenga unavyotaka alikataa kabisa,lakini cha ajabu ukienda kwa watu unakuta maneno mengi eti Mimi nimelinga na kumsahau baada ya kufanikiwa kimaisha, lakini mama anasahau kuwa Mimi hapa nilipo baba mzazi ambaye yuko na zaidi ya miaka 70 ananitegemea Mimi hata familia ambako mzee wangu anaishi inanitegemea Mimi,jumlisha na familia yangu ongeza na mama yangu anayetaka vitu nisivyoviweza yaani ni baraa tupu kwakweli .wakati mwingine huwa nakata tamaa kabisa wakuu

Wakuu naomba ushauri wenu kwa huyu mzazi wangu je anania gani na Mimi ? nahisi kuzikosa baraka za mama na huenda nikalaaniwa na Mimi watoto wangu wakaja shindwa kuniheshimu,nifanye nini ili nikae meza moja na mama ,maana inaweza pita hata mwaka hata kusalimiana kwenye simu hakuna .lakini si Mimi tu hata kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ni hivyo hivyo.

Samahani kwa uandishi wa kuchosha wapendwa.
 
Usilalamike mama amekufanyianmangaoi toka tumboni hadi miaka 23 haaaa we unalalamika we Fanya nao ngeza juhudi
 
Usilalamike mama amekufanyianmangaoi toka tumboni hadi miaka 23 haaaa we unalalamika we Fanya nao ngeza juhudi
huo nao ni Ushauri
Mimi namshauri okonkwo jr aachane naye kabisa, hawa Wazazi kuna kipindi hawaelewi kuna na sisi tunaelekea hukohuko tutakuwa wazee km wao.
Mtembelee wakati wa Likizo na umuelezee kuwa na Nduguzo nao washiriki kummalizia hilo Jengo
Kuna siku utakuta keshamrithisha anayempenda kisa wewe tu hujampigia simu
Mama zetu wana yao anaweza mpenda mmoja na hasa wa mwisho aliye naye karibim pesa zote unazomtumia anampa, iwe chakula hata ardhi
na Hili utajajuta na kurudi hapa Jukwaani
toa kwa kadri ya uwezo wako
 
Wazazi wengi wa kike ndio tabia zao kabisa. Sio wewe tu unayekutana na hayo ni wengi sana.
Cha msingi fanya kitu kilichokuwa ndani ya uwezo wako. Mpaka hapo umejitoa vya kutosha na ukiangalia hakuna anayekusaidia kati ya hao ndugu zako.
Pigana na husichoke kumuweka mikononi mwa Yesu ambadilishe.
 
Back
Top Bottom