USHAURI NASAHA: Maridhiano ya Kitaifa yanahitajika Tanzania

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,596
3,639
Chuki ya kisiasa kati ya wafuasi wa CCM na washirika wao vs wafuasi wa vyama vya upinzani inaongezeka siku hadi siku.
Ukipitia mitandao ya kijamii ( japo CCM wanaibeza) utaona maoni ya hasira na chuki anayojibiwa kiongozi wa CCM (mfano, Mwigulu, Kangi Lugola, DC Kigamboni, Possi, n.k n.k).

Upendo umetoweka Tanzania yetu hii.

Vijana wa CCM nao hawapo nyuma hapo katika wachangiaji 1000, utaona wanaounga mkono kauli za viongozi wa CCM wapo 20 ( 980 wote wanaponda kauli za viongozi wa CCM).

Mimi nimeona sasa yatosha; hii chuki usiachwe iendelee kutawanyika.

1. Viongozi wa serikali ya CCM waache kutoa matamko yanayoamsha hasira za watu ( waongee ukweli wasipotoshe)
2. Viongozi wa Vyama vya Upinzani nao wafanye hivyo hivyo kama wa CCM wasitoe kauli zinazoamsha hasira.
3. CCM itoe fair political playground kwa vyama vyote.
4. Viongozi wa dini wasiegemee upande wowote wa kisiasa.
5. Tutofautishe kati ya matusi na kukosolewa.
Asanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana pambana kutafuta pesa na mali, haya makelele ya wanasiasa, vibaraka na wanachama wao itakuwa ni sehemu ya comedy au burudani katika maisha yako.

Kwakifupi una stress za maisha na hapo ulipo haujatoka wala kufanikiwa kimaisha jambo ambalo linakunyima usingizi sana. Kufuatilia kwako hayo mambo ya kisiasa ni namna tu unatumia kutolea stress za maisha.

Tafuta mali na pesa. Utaona utamu wa maisha ya hii dunia.

Usipofuatilia siasa na kuwa serious nazo basi hao wanasiasa wana uwezo wa kukuteka na kukupukutisha vijisenti vyako!. Hapo ndipo utakapokumbuka kumbe ungekuwa active katika nchi kutaka siasa safi hatma hiyo isingekukuta!

Mo Dewji alishaachana na habari za siasa na kuamua kutafuta hela, lakini hela zake hazikumsaidia asitekwe na infact ndizo zilizosababishwa atekwe!

Leo hii, Mo ananyang'anywa mashamba yake, na alishaachana na mambo ya siasa!

Kwa hiyo mdogo wangu shiriki kikamilifu katika kila hatua za kuona nchi yako inaongozwa kwa haki, kuwepo na utawala bora na uongozi bora kwa hiyo siasa haikwepeki. Athari za utawala wa kidhalimu hazibagui, hata hao wenye hela wanaionja joto ya jiwe!
 
hakuna maridhiano.kati ya mashoga na watu safi.kati ya giza na nuru
Mbona DAB alipotangaza vita dhidi ya mashoga, waziri alikuja mbio mbio kusema kuwa huo si msimamo wa sirikali?! Hii maana yake msimamo wa sirikali ni kinyume cha kile DAB alikuwa anafanya. Kwahiyo kuna maridhiano.
 
Usipofuatilia siasa na kuwa serious nazo basi hao wanasiasa wana uwezo wa kukuteka na kukupukutisha vijisenti vyako!. Hapo ndipo utakapokumbuka kumbe ungekuwa active katika nchi kutaka siasa safi hatma hiyo isingekukuta!

Mo Dewji alishaachana na habari za siasa na kuamua kutafuta hela, lakini hela zake hazikumsaidia asitekwe na infact ndizo zilizosababishwa atekwe!

Leo hii, Mo ananyang'anywa mashamba yake, na alishaachana na mambo ya siasa!

Kwa hiyo mdogo wangu shiriki kikamilifu katika kila hatua za kuona nchi yako inaongozwa kwa haki, kuwepo na utawala bora na uongozi bora kwa hiyo siasa haikwepeki. Athari za utawala wa kidhalimu hazibagui, hata hao wenye hela wanaionja joto ya jiwe!
Jibu murua kabisa,siasa ni maisha

akikujibu niambie tuna vijana mizigo sijui wanawazaga nn
 
Chuki ya kisiasa kati ya wafuasi wa CCM na washirika wao vs wafuasi wa vyama vya upinzani inaongezeka siku hadi siku.
Ukipitia mitandao ya kijamii ( japo CCM wanaibeza) utaona maoni ya hasira na chuki anayojibiwa kiongozi wa CCM (mfano, Mwigulu, Kangi Lugola, DC Kigamboni, Possi, n.k n.k).
Upendo umetoweka Tanzania yetu hii.
Vijana wa CCM nao hawapo nyuma hapo katika wachangiaji 1000, utaona wanaounga mkono kauli za viongozi wa CCM wapo 20 ( 980 wote wanaponda kauli za viongozi wa CCM).
Mimi nimeona sasa yatosha; hii chuki usiachwe iendelee kutawanyika.
1. Viongozi wa serikali ya CCM waache kutoa matamko yanayoamsha hasira za watu ( waongee ukweli wasipotoshe)
2. Viongozi wa Vyama vya Upinzani nao wafanye hivyo hivyo kama wa CCM wasitoe kauli zinazoamsha hasira.
3. CCM itoe fair political playground kwa vyama vyote.
4. Viongozi wa dini wasiegemee upande wowote wa kisiasa.
5. Tutofautishe kati ya matusi na kukosolewa.
Asanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haijawahi na wala haitakuja kutokea kufanya maridhiano na Shetani
 
hakuna maridhiano.kati ya mashoga na watu safi.kati ya giza na nuru

Karibu utoe mchango kama mtu mzima, punguza hizo karaha hapa...

Ilindeni CCM, kwa michango ya hoja zilizo na mashiko.
Wazee wamestaafu na hekima zao, jaribuni kutafuta msaada toka kwa waastafu.
 
Kwa kusoma mitandao unaweza kweli kuogopa kwambà kuna chuki kubwa sana. Hii siyo kweli. Kote duniani kwenye nchi ambayo wananchi wake wako huru raia hukosoa serikali yao. Pale ukosoaji unapogusa mambo ya msingi kabisa serikali hutoka hadharani kutoa kauli rasmi. Hapa kwetu hali ni tofauti. Inaelekea kuna mpango rasmi au usiokuwa rasmi ambapo kuna raia wamepewa au wamejipa kazi ya kuwajibu wenzao wanaokosoa serikali yao! Hali hii ilianza awamu ya 4 na sasa imeshamiri kama siyo kurasmishwa.Na kwa sababu hawa ni raia tu na wanajitokeza kujibia serikali hata kwa mambo ambayo hayastahili mabishano kutokea. Mabishano hayo kati ya raia wanaokosoa serikali yao na wale ambao wamepewa au kujipa kazi ya kuijibia serikali ndiyo yanayojenga taswira ya uhasama. Lakini hawa ni watu wachache tu. Watanzania walio wengi wanajua hali ilivyo na hawana uhasama na kundi lolote la raia wenzao. Kuna watu kwenye mitandao waonyesha kutamani baadhi ya wanasiasa wetu wafe! Watu wa aina hiyo wanazo sababu zao binafsi na ungeweza kuwahesabu hawafiki elfu. Maridhiano ya kitaifa ni jambo jema lakini siyo kwa mtazamo huu. Kweli kuna wakati kama taifà itabidi kufanya tafakuri ya kina na kutengeneza pale palipoharibiwa kwa maslahi binafsi. Ethiopia wameanza kazi kama hiyo ikiwa ni pamoja na kulipa fidia raia walioumizwa isivyo halali.
 
Hivi unakumbuka tulipoingia mfumo wa vyama vingi ni asilimia ngapi ya watanzania walitaka vyama vingi, na unafahamu kwanini Nyerere alishauri tukubali mfumo wa vyama vingi na kupuuza asilimia 80 waliotaka chama kimoja. Ilikuwa ni kutokana na hoja walizokuwa nazo wale wenye asilimia 20. Ukiangalia sasa hivi utaona hao unaosema wengi kwenye mitandao lakini hawaonekani kwenye uhalisia mitaani na ukasubiri waonekana kwenye uhalisia mtaani ujuwe kuwa hapo hatua ya maridhiano itakuwa imeshachelewa. Hao walio wengi mitandaoni ukisikiliza hoja zao utaona wanaongea mambo ya msingi. Hivi huko mtaani wakigundua kuwa kuna mambo ya msingi ambayo yameachwa kwa makusudi kusimamiwa wataacha kuchukuwa hatua. Kama tukidhania wanaongea na kuikosoa serikali ni wachache Kwahiyo hoja zao zisichukuliwe hatua hadi watakapo kuwa wengi itakuwa vigumu sana kuwanyamazisha wasichukuwe sheria mkononi. Kuna hoja zinahitaji majibu ya Kina kama mauwaji ya Kibiti, kushambuliwa kwa Lisu, Demokrasia, Uhuru wa watu, Katiba mpya, Ubadhirifu pesa za umma, na mengine mengi.
 
kula ndimu
Yaani wewe ni njaa tu na kutaka uteuzi wa huruma au wa kupewa kama ni mbunge bac ulipita wakati watu bado hawajaelemika muulize ucd, msiba, lumtuzi kama wakigombea jimbo lolote halafu kuhesabu kura asimamie Mmarekani na askari watoke marekani hamtapata hata kura moja labda yko tu na kama unabishi 2020 tuombe iwe hivyo USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom