Naomba Ushauri: Napoteza pesa mno nahisi kuchezewa

Achana na kamari haijawahi kutoa matajiri ni bahati na nasibu, ndo maana mjini matajiri wote ni wafanya biashara zinazo onekana machoni kwa watu

IMG_0335.jpg

Unamjua huyu mwamba?
Kawa usd billionaire kwa kamali.
Soma kitabu chake cha The set up.
 
Pamoja mkuu
Ila.nimefurahi ulivyompambanaji! Ukiweza kuachana na ulozi hakika utatoboza! Unajua waganga wa kienyeji wakati mwingine huwa wanatumia bahati zetu kujiendeleza! Yaani wewe unakuwa unamfanyia kazi yeye! Kila unachopata kinapitiliza kwenda kwake!
 
View attachment 2063607
Unamjua huyu mwamba?
Kawa usd billionaire kwa kamali.
Soma kitabu chake cha The set up.
Achana na wazungu hata huyo hujui maisha yake umesoma ya kitabuni ambapo ni ya kuandikwa unajuaje kama ni kweli ?

Tuje uhalisia wa maisha ya kitanzania
Je unapo ishi umemuona nani katajirika kupitia kamali.
Kama hamna acha kuaminisha watu ujinga
 
Hata nikisema leta hiyo hela nikutunzie utaidai siku hiyo hiyo.

Usitangulize sana waganga mweke Mungu mbele
 
Achana na wazungu hata huyo hujui maisha yake umesoma ya kitabuni ambapo ni ya kuandikwa unajuaje kama ni kweli ?

Tuje uhalisia wa maisha ya kitanzania
Je unapo ishi umemuona nani katajirika kupitia kamali.
Kama hamna acha kuaminisha watu ujinga
Au kwenye yale mabanda ya meridian, galsport sijawahi ona mtu amepaki hata ka passo njee,.ukichungulia kwa mbali unaona watu waliolose hope ndio wamejazana
 
Ila.nimefurahi ulivyompambanaji! Ukiweza kuachana na ulozi hakika utatoboza! Unajua waganga wa kienyeji wakati mwingine huwa wanatumia bahati zetu kujiendeleza! Yaani wewe unakuwa unamfanyia kazi yeye! Kila unachopata kinapitiliza kwenda kwake!
Sure kaka
 
Au kwenye yale mabanda ya meridian, galsport sijawahi ona mtu amepaki hata ka passo njee,.ukichungulia kwa mbali unaona watu waliolose hope ndio wamejazana
Huwezi kuta GXR imepaki pale, utakutana wamejaa boda boda sie wa tz eleven.

Betting utapata ela ya kusogeza siku na kuliwa kwa sana, wanao nufaika ni wachache sana kwenye watu buku hata 2 tu
 
Guys siku mkijua hela ni makaratasi tu, kwenye kila noti yameandikwa maneno haya "Fedha halali kwa malipo ya huduma au bidhaa ya"... Vijana tuzalishe mali au kutoa huduma ndio tuzibadili kwa fedha... tusifanye upatu
 
Kwanza kabisa napenda kuweka waZi kuwa kila kitu katika huu Uzi ni ukweli mtupu na ndo Hali nayopitia katika maisha yangu

Pia Kuna Mambo utaona nilikuwa nafanya au naendelea kuyafanya kama mjinga lakini ndo najikuta nafanya hivyo so naomba mtu anayeweza kunishauri Basi azingatie yote haya
.
Back 2015:
Nilivotoka chuo tu nikarudi home nikakaa Kama wiki hivi ikabidi niondoke home kulingana na kuwa nimelelewa tu pale Ila sio wazazi wangu wa kunizaa ni walezi maana hakuna mzazi wangu hata mmoja ninayemfamu ,( Mungu awarehemu). Nilivotoka home nilienda kujitolea shule moja hivi kufundisha ambako nilipiga kazi almost miezi 6 hivi kwa makubaliano ya kulipwa 60k kwa mwezi lakini nililiowa mwezi mmoja tu mingine yote kwa lugha rahisi niite nilidhurumiwa,
.
2016 January nikatafuta kampuni moja Ivi ya kijasiriamali ya kuuza bidhaa kwenye mitaa na kwenye magari Kama umewahi waona jamaa wanaoongea Sana kwenye gari wakiwa wanauza bidhaa Basi ndo mfano wa hio kazi ambayo nimepiga kwa muda wa mieZi 6 kampuni ikafa. So Kuna vihera vichache ambavyo nilikuwa navitunza kama 150k Ivi ambayo kwangu ilikuwa kubwa kipindi hicho so nikapanga room 20k kwa miezi mitatu na iliyobaki nikanunua godoro malaika na shuka ,maana Kule kwenye kampuni tulikuwa tunahudumiwa kila kitu isipokuwa msosi , so nikaendeleza kazi yangu ya kuuza bidhaa kwa muda huu nikawa nanunua madukani na kwenda kuuza mtaani, nakumbuka nilianza na 16k Kama mtaji ambapo nilijumua sabuni za kuogea dazan mbili na mafuta ya kupakaa

Nilikimbiza miezi kadhaa mtaji ukakua kiasi chake ,ikabidi niachane na kuuza bidhaa nijiingize kwenye kufundisha masomo ya utengenezaji bidhaa kadhaa za ujasiriamali ambazo nilikulaga course ya wiki moja kipindi Niko chuo ,so nikawa naandaa semina for free lakini baada ya semina nauza vitabu ambapo ndo faida ikawa inapatikana hapo nilipiga kazi hio kwa miezi Kama mitatu hivi nikapata total kama milioni 8 hivi huku miezi imesogeasogea,katika pitapita zangu humu jf nikakutana na uzi wa jamaa anaitwa Ontario uloenda kwa heading ya biashara ambayo hakuna benki itataka uijue,baada ya kusoma ule Uzi nikavutiwa kwa kuwa fedha nilikuwa nayo Basi nikatenga milioni moja kwa ajiri ya nauli malazi na ada ya mafunzo kwa siku 5 za mafunzo pale jangid plaza

Nilifanikiwa kuhudhuria darasa siku Zote tano huku nikiwa nalala gesti maana ndo ilikuwa Mara yangu ya kwanza kuja dar.

Baada ya kumaliza mafunzo sikufanikiwa kufungua Acc yoyote ya kutrade sababu nilikuwa Sina I'd yoyote wakati huo ko nikaamua kupotezea ,nilivorudi mkoa ikabidi nifanye semina kadhaa ili nirudishe ile milioni niliyoitumia kwenye hio semina na nikafanikiwa kama nilivopnga na mahesabu yangu yakarudi Kama mwanzo ambapo nilikuwa na million 8+
Mwanzoni mwa 2018 nikatafuta mkoa utakaonifaa kwa biashara ya mtaji huo nikaona ni dar ambapo nilipanga kuanza na biashara ya miamala mpesa na tigopesa na huduma zingine ndogo ndogo baadae wakatangaza maombi ya kutuma ajira Mimi sikutuma coz nilikuwa tayari Nina plan ya kufungua biashara, kweli nikafanikiwa kusafiri mpaka dar na ilinichukua siku 4 kutafuta eneo laini za wakala na nyumba ya kuishi na kazi ikaanza

Nimeenda nayo ile kazi na kweli nilibarikiwa kazi ikawa inanilipa nikaongeza na huduma zingine za stationary na nikawa nazidiwa na wateja so nimeenda na hio kazi huku mtaji ukikua Hadi kufikia 12+milioni


Ilivoingia 2019 siku moja baba mwenye nyumba jioni kanitumia text kuwa nimuwekee 700k kwa namba yake jioni nikifika atanipatia so nikaona sio mbaya nikamtumia hio pesa aliyohitaji lakini ilivofika jioni kanambia hio hela alitegemea kuwa mtu angemletea lakini hakuleta so nimsubirie kidogo, kweli nikaona sio mbaya nikaendelea na mambo yangu lakini ile hela mpaka siku ya tatu jamaa bado hajanipa nikawa nafikiria namna ya kuirudisha ile pesa ili nisione pengo maana niliongeza huduma Za benk wakala pia

Njia rahisi nikaona kubeti licha ya kuwa sikuwahi kubeti hata siku moja huko nyuma

Nakumbuka siku hio asubuhi navojisajiri na app ya betting nikaona Kuna Liverpool na Barca wanacheza usiku so sikuchelewesha ikabidi ni deposit 500k kwenye ile acc ya betting na nikampa Liverpool kuwa ashinde

Lakini ilipofika huo usiku bahati haikuwa kwangu nikajikuta nimeloose yaani Liverpool kapigwa 3-0 nakumbuka ilikuwa mwezi wa tano 2019 ,hapo nikazidi kuchanganyikiwa na nikaanza kubeti ovyoovyo ili mradi pesa irudi na viwango nilivyokuwa naweka ni kuanzia 100000 Hadi 500000 na hakuna mechi nilizokuwa nawin baadae nilivoona mtaji imepungua nikapanga kuuza fremu na vifaa vyote vya kazi niingie mkoa nikatuli nianZe kufanya forex niliyojifunzaga kwa wasouth walioletwa na Ontario pale jangid plaza.

Nilikuwa kila nikijaribu kuuza haviuziki huku naendelea kubeti mpaka nikajikuta nimebaki na 2milion pekee ikabidi nistop kubet nihangaikie kuuza vitu vya ofisi na gethon

Nilipambana bila mafanikio wateja hawaonekani baadae nikahisi Nina mikosi nikaingia humu nikaseach mganga wa kienyeji ambaye angetoa mikosi nikaona Kuna mtu amewahi kucomment kwenye Uzi wa jamaa aliyekuwa anauliza naye mganga na alielekeza yupo huko bagamoyo ikabidi na Mimi nichukue ile adress nimfuate yule mganga nilifika usiku Kama wa saa nne hivi nikaenda kulala kwa jamaa aliyenipeleka na bodaboda ili asubuhi niamkie kilingeni


Asubuhi ilipofika nikaamkia pale nikawakuta wanamajengo Hadi ya kulaza wagonjwa nikawaona wale vijana na nikawaambia direct kuwa na nahisi mambo yangu hayako sawa naomba mnisaidie ili mambo yakae sawa wakanitajia vitu vinavyotakiwa pale kuwa ni kuku,Nazi na sanda nyeupe

Nikatoa ile hela ili vitu vikatafutwe Kama 45000 hivi Basi wakaanza kusoma vitabu vyao vya kiarabu huku waloniambia Mimi niwe nachoma udi na kusema shida zangu pamoja na kuziweka zile Nazi kwenye Moto Kama nazikausha fulani hivi

Shughuli ikaendelea baadae walivomaliza kusoma na mm kunuia ikabidi nikazipasue zile Nazi na nikavishwa ile sanda nyeupe nikaogeshwa na dawa Fulani hivi baada ya hapo wakasema tayar Mambo yako yatakuwa super wakanambia kuwa nirudi baada ya wiki mbili na wakagurantee kuwa hivo vitu ambavyo haviuziki Basi nitaenda kuuza


Nikachukua boda mpaka lami na hapo nikapanda Basi mpaka tegeta nikatafuta gari la kwenda gethon ,nilivofika nikaanza kupigiwa simu na watu wakiulizia vile vitu nilivyokuwa nimetangaza Sasa sikujua ni ile tiba au tu watu walipanga kunitafuta yaani kwamba hata nisingeenda labda wangenitafuta tu ilikuwa suala la muda so sikujua exactly hasa baada ya wiki nikawa nimefanikiwa kuuza kila kitu nikapata Kama 4 milion na ile milioni 2 iliyobaki nikawa kama na 6milion+

Nikarudi mkoa Nikatumia Kama 2.2milion kupanga na kununua vitu vyote vya msingi gethon tayari kwa kuanza forex


Wakati huo nikawa nimepata I'd so nikafungua acc kwa templer nadhani ambao ni trader wanamjua nikaanza kudeposit na kutrade na nilikuwa sijawahi kutrade hata demo nikaanza moja kwa moja real account huku nikawa nasambaza affiliate link za brokers tofauti tofauti so niliendelea na shughuli hizi mbili huku forex ikinibariki maana mwanzoni nilikuwa naprofit Sana na nikawa nawaza utajiri muda wote baada ya Kama wiki hivi nikaanza kuchoma acc kila nikideposit nachoma, nilichoma pesa zote nikabaki Sina kitu, baadae wakati napita YouTube nikaona habari moja ya kuwa Kuna mzee huko sumbawanga anatengeneza radi ambapo kwangu ikawa kigezo kuwa angeweza kunitoa mikosi na kung'arisha nyota yangu so nikachukua namba nikampigia akadai anaweza kunitatulia ile shida niandae 100k sikuchukua round nikaondoka asubuhi kupitia mbeya nikafika sumbawanga saa tatu usiku nikalala gest na asubuhi nikamtafuta yule doctor , akanipa tiba nikarudi lakini sikuona mabadiliko bado na Kuna dawa za kuoga alinipa kiukweli sikuona mabadiliko labda Kama yalitokea indirect


So nilivofika home ikabidi nianze kuuza kimojakimoja huku naweka forex nachoma baadae nikauza kila kitu nikadeposit na kuanza kutrade huku nalala gesti nawithdraw dola 20 nakula na kulipa gesti mtaji wote upo kwenye acc, nimeenda Kama wiki hivi hela ikaungua ikabidi nitoke gest niingie mtaani kutafuta vibarua yaani hapo hata Mia moja Sina na hakuna wa kumuazima hela katika kipindi niliona Cha mtemakuni Basi ni kuanzia October Hadi December 2019 ambapo nilikuwa nalala nje na kazi Sina mpka nikawa naomba watu njiani wanipe hata jero ya kula maana vibarua vikawa hamna kabisa Yani kila nikitafuta naambulia patupu, nikaja nikauza simu kwa hasara ilimradi nipate hela ya kujikimu , nikaanza kuingia migodini lakini ile kazi sikuiweza kwa maana hata abc zake nilikuwa sijui

Ikabidi niache nikakumbuka Kuna siku nilikuwa nasambaza affiliate link ikabidi nitoke huko migodini nije mjini kwenye internet cafe nicheki Kama kweli wanalipa, nikalog in broker wa kwanza ni zero ,wa pili naye ikawa zero huyu watatu ile nalog in tu nakutana na commission ya dola 240$ ambayo ni Kama 600k kasoro chap nikanunua simu na zilizobaki nikadeposit na kuanza kutrade ambayo nayo nikaichoma so mpaka leo hapa kati nimepitia mengi Ila huyu broker ananilipa commission nzuri ambayo kwa mwezi ni kati ya Dolla 200$ na 500$ na analipa kila siku lakini nachoshindwa kujizuia ni kuwa hii hela Nikilipwa naanza kuitrade na nachoma Hadi mwezi unaisha nakuwa Sina kitu yaani nimekuwa Kama addicted Fulani hivi maana naweza trade nikaprofit Hadi $1000 na muda mwingine naweza withdraw nikanunua vitu vya ndani lakini siku nikichoma najikuta nauza Tena vile vitu na kudeposit Tena ambapo naweza choma na kurudi sifuri Tena ko maisha yangu yanazunguka tu hapo hakuna Cha maana nafanya na hii Hali naichukia vibaya mno lakini kuacha siwezi kabisa ,


Mfano hapa nilikuwa naishi chumba Cha pango la 130000 na vitu vya ndani vya kupendeza baada ya Kodi kuisha nimeshindwa kulipa maana hela niliyoweka ya Kodi nimechoma so nilichofanya nikauza kila kitu nimaepanga room la 40000 na nimebaki na godoro tu na shuka na wakati getho lilikuwa full .


Yaani nashindwa kujua Nina shida gani nimeogea chumvi ya mawe wapi nimeenda kwa madoctor wa asili bado mambo magumu


Hatari niliyonayo saivi nikuwa Sina kazi nategemea commission wakinilipa ndo nakula na kutrade ambapo daily nachoma

Nifanye nini niweze kunyoosha mambo yangu jamani maana najikuta nazunguka palepale hakuna nachofanya


Mimi nahitaji niwe na mchongo mwingine nje na hii commission na nimekaa muda mrefu almost miaka miwili nazunguka palepale na hakuna Cha kufanya na vipi ukishakuwa addicted na jambo Fulani unaweza liacha kwa namna gani maana huwa nafutaga account lakini najikuta naZirudisha Tena

Sorry kwa Uzi mrefu




MFANO HII NI COMMISSION YA MWEZI WA 12 HUU YAANI TOKA TAREHE MOJA HADI LEOView attachment 2063570
View attachment 2063617View attachment 2063618
Lipia tangazo refu la forex
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom