Ushauri: Naona kama huu ni utumwa!

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,268
2,310
Asalamu wakuu!
Ni imani yangu mnaendelea na majukumu yenu ya kujitafutia chochote kitu maisha yasonge.

Back to topic!
Mimi ni kijana muajiliwa hapa mjini Dar kwa takribani miaka miwili sasa. mshahara wangu si haba mana take home ni kama Tshs. 980,000/= per month.

SHIDA YANGU! kwa takribani muda huu wote wa miaka miwili sijafanya lolote la maana zaidi ya kula, kunywa na kuvaa yaani kuna muda nafuria hata hela ya kula nakuwa sina.

Nikaamua nijaribu kufanya analysis ya expenditure zangu per month nione gap iko wapi! on average (3 month average) ikaonyesha matumizi yangu kwa mwezi ni kama ifuatavyo!

1. Kodi ya nyumba-200,000
2. Maji na umeme-40,000
3. Chakula (mwezi)-250,000
4. Hela ya emergency-100,000
5. Suport fund (ndg)-100,000
6. Vocha na nauli kazini-40,000
7. Ada ya dogo (Form 4)-100,00
8. Chakula kazini (Posta)-100,000
9. Mengineyo* -50,0000
*Nguo, viatu n.k
JUMLA ni Tshs. 980,000.

Yaani kwa mwendo huu nimefungwa kwenye hiyo circle (utumwa). Natamani hata lije dili la kontena lakini wapi. Kwangu mimi naona hii kazi ni utumwa na sitaweza kuendelea kwa kuendekeza huu upuuzi.

katika kuondokana na hili janga nimeonelea kuwa nirudi tu mkoani nikalime na nikajiajili kuliko kukaa hapa mjini bila ramani.

Naombeni wazoefu wanaolima mikoani na mnaoweza kumiliki hata ka vitz kwa hii mishahara tupeane mawazo maana mimi sometimes namchukia hadi wife kwani naona kama tuliwahi kuoana na ndio chanzo cha matatizo.

NB. Nimeoa, nina mtoto (3).
 
Mbona mshahara mkubwa sana huo ni hivyo hukujipanga tu broo kaa utulie jipange usinamnie kua huna deal lolote lile la kukuingizia shs mbili tatu katika week kwa mjini dar haliwezekani labda mazingira ulojiweka sio tu jichanganye na watu waswahili wanasema ishi na watu upate vitu
 
Huo mshahara mbona mkubwa sana? Kuna watu wanapata robo ya huo na maisha yanaenda. Ila muhimu ni kuwa na kitega uchumi kingine kinachokuingizia pesa.
 
Yaani umepanga Kwa laki 2 kwa Mwezi au?

Basi Umasikini Upo Akilini Mwako Tu.. Ili Uwe Tajiri Jaribu kuwa Mbahili Hata Mwaka Basi halafu Fanya Kitu Cha Maana

Maana Naona Kuna Chakula Kazini 100000 Na Chakula Tena 250000 Wakati Kwa Mtu wa Kawaida Tsh 150000 inatosha Kabisa Kwa Mwezi kama Upo Mwenyewe

jukwaa La Uchumi nq Biashara Lipo Humu mbona Pitia Thread Za Ujasiriamali La Sivyo utagonga 30 hujafanya La Maana
 
Daaaah,,,,,kalime tuu labda shida utazopata zitakufanya use an akili,,,Kwa mshahara huo MZee hupaswi kuwa the shida,,,acha maisja ya kushindana
 
Mbona mshahara mkubwa sana huo ni hivyo hukujipanga tu broo kaa utulie jipange usinamnie kua huna deal lolote lile la kukuingizia shs mbili tatu katika week kwa mjini dar haliwezekani labda mazingira ulojiweka sio tu jichanganye na watu waswahili wanasema ishi na watu upate vitu
asante mkuu nitalifanyia kazi, japo mimi ni changanyikeni sana, nadhani nahitaji kukaa karibu na wenye madili
 
1. Kodi ya nyumba-200,000
2. Maji na umeme-40,000
3. Chakula (mwezi)-250,000
4. Hela ya emergency-100,000
5. Suport fund (ndg)-100,000
6. Vocha na nauli kazini-40,000
7. Ada ya dogo (Form 4)-100,00
8. Chakula kazini (Posta)-100,000
9. Mengineyo* -50,0000
*Nguo, viatu n.k
JUMLA ni Tshs. 980,000.
mkuu mshahara wako mbona mkubwa sana kaa chini upunguze matumizi mfano namba 3 &8 vinausiana na chakula sijajuwa uko officen unakula Milo mingapi, moja unatosha tena mchana, halfu namba 4&9 hapo napo lazima ujiangalie utanunuaje nguo kila mwenzi na mtu unataka maendereo jifunze kukomaa. kingine Jitahid upate shamba maeneo ya Karibu na dar litakusaidia kununua chakula . ONGEZA NAMBA 10 UWE UNAWEKA SAVE YA PESA sidhani emergency money inaisha yote per month.
 
Yaani umepanga Kwa laki 2 kwa Mwezi au?

Basi Umasikini Upo Akilini Mwako Tu.. Ili Uwe Tajiri Jaribu kuwa Mbahili Hata Mwaka Basi halafu Fanya Kitu Cha Maana

Maana Naona Kuna Chakula Kazini 100000 Na Chakula Tena 250000 Wakati Kwa Mtu wa Kawaida Tsh 150000 inatosha Kabisa Kwa Mwezi kama Upo Mwenyewe

jukwaa La Uchumi nq Biashara Lipo Humu mbona Pitia Thread Za Ujasiriamali La Sivyo utagonga 30 hujafanya La Maana
Nimejitahidi sana kubana matumizi lakini wapi, sometimes inavuka hadi 300k mana hyo ni wastani.
 
1. Kodi ya nyumba-200,000
2. Maji na umeme-40,000
3. Chakula (mwezi)-250,000
4. Hela ya emergency-100,000
5. Suport fund (ndg)-100,000
6. Vocha na nauli kazini-40,000
7. Ada ya dogo (Form 4)-100,00
8. Chakula kazini (Posta)-100,000
9. Mengineyo* -50,0000
*Nguo, viatu n.k
JUMLA ni Tshs. 980,000.
mkuu mshahara wako mbona mkubwa sana kaa chini upunguze matumizi mfano namba 3 &8 vinausiana na chakula sijajuwa uko officen unakula Milo mingapi, moja unatosha tena mchana, halfu namba 4&9 hapo napo lazima ujiangalie utanunuaje nguo kila mwenzi na mtu unataka maendereo jifunze kukomaa. kingine Jitahid upate shamba maeneo ya Karibu na dar litakusaidia kununua chakula . ONGEZA NAMBA 10 UWE UNAWEKA SAVE YA PESA sidhani emergency money inaisha yote per month.
mkuu nitairejea hii actual expenditure plan, kazini ni mulo mmoja na maeneo nilipo ni kama Tshs. 5000/= normal
 
Back
Top Bottom