Ushauri: Namna ya kusajili Private Company kwa TZ. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri: Namna ya kusajili Private Company kwa TZ.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Miradi, Aug 27, 2012.

 1. M

  Miradi Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau,
  nahitaji msaada wenu, mimi nahitaji kusajili kampuni ya ushauri wa kitaalamu (consultancy) ila iwe private company je:-

  1. Nahitaji mambo gani?
  2. Gharama yake kiasi gani?
  3. Nani anaweza kunisaidia zaidi?

  Asanteni.
   
 2. C

  Chinga boy JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nenda brela utapata maelekezo yote hapo
   
 3. M

  Miradi Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu brela haiko huku kijijini
   
 4. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Mods ipelekeni jukwaa husika hii. Business & Economic
   
 5. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,129
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  Kwani hapa uwezi kumsaidia?unampa hata hints hata akienda uko brela anajua anaenda kufanya nini,mambo mengne tuwe na busara jamani,sio mpka ujibu kila kinacho ulizwa hapa,kama haujui umia kwnye threads za saiz yako,nenda jocks uko utakoment vzuri tu,bt baadh ya mambo we need to be serious lets get down to bznes.
   
 6. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  unatakiwa kwanza kuchagua jina la kampuni yako ndugu, kisha unawaandikia brela barua ya kuomba watafute hilo jina kama lipo kwenye database yao. jina linaweza kukataliwa kama
  • linaharassment
  • linafanana na jina la taifa mfano tanzania co ltd
  • linashahabiana na jina lilopo mfano kuna simba cement halafu wewe ukataka uwe na lion sement au kuna quicks ltd nawe ukatak uwe na qwix ltd ni majina yanaomislead hayo
  jina likishathibitishwa na brela kuwa linafaa utatakiwa kuandaa memorandums & articles of association the utazifile kwa registra of co(BRELA) baada ya hapo registra atakupa certificate of registration, hiki cheti kitaonyesha kuwa tayari kampuni imesajiliwa(imekuwa legal entity) baada ya kukamilisha michakato mingine ambayo ni pamoja na tin utapewa kitu kinaitwa certificate of comencement of businees, hiki cheti kitakupa wewe mamlaka ya kuanza kufanya biashara.
  gharama za kusajili kampuni ni kama ifutatavyo
  1. registration fee (tsh 50,000-300,000) hii inategemeana na share capital kwa kampuni zenye share capital, anbayo share capital inaanzia 20,000 na kuendelea
  2. filing fee anbayo ni 45,000
  3. stamp duty ambayo ni 12,200
  hivyo basi mfano ukisajili kampuni ambayo ina share capital ya chini kabisa itakugharimu tsh 107,200 na yenye share capital ya juu kabisa ni 367,200
  kumbuka hizi ni gharama ambazo utatakiwa kulipa brela, hivyo hapo hakuna lega consultation fees ambayo haipo constant, inategemea na wakili utakayempata akakuandalia/ kukusainia hizo memorandums & article of associations, hivyo basi gharana za utaalamu na ushauri wa kisheria zinaweza kupelekea jumla kuu hadi ya tsh 500,000+ kutegemeana na wakili unayemtumia
  kwa uelewa wangu wa business law niliyofundishwa ni hayo tu najua, kama niepunguza au nimeongeza nipo tayari kurekebishwa kwa upendo na upole. kila la heri mkuu. inaweza kunipm kama ungehitaji ushauri zaidi.
   
 7. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Voice of widom
  Asante kwa ushauri mzuri wa kijamaa. Umetusaidia wote kwa kweli. Swali langu ni hili, nini faida ya kuandikisha kampuni na kufanya biashara bila kuandikisha kampuni kwa biashara zisizo za mikataba kama za ukandarasi kama maduka, hotel, uasfirishaji n.k?
   
 8. M

  Miradi Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana check PM
   
 9. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kuna faida nyingi ndugu ya kufanya biashara kama kampuni. Nizitaje chache
  kampuni ikishasajiliwa inakuwa ni sawa na mtu(inaweza kushtaki au kushtakiwa kwa jina lake) mfano voice of wisdom co ltd ni tofauti na voice of wisdom.
  Mara nyingi benki zinakopesha kampuni kirahisi kuliko mtu binafsi.
  Katika suala la ufilisi ukiwa na kampuni ukakopa ukashindwa kulipa wewe kama mmiliki(share holder) hutafilisiwa, kitakachofilisiwa ni kampuni na sio wamiliki.
  Kampuni huwa inalipa kodi baada ya kupata faida tofauti na biashara ambayo si kampuni unalipa kodi hata kama umepata hasara mfano xyz ltd inalipa kodi tu endapo makaguzi ataonyesha kwenye audit report kwamba xyz ltd amepata faida, hivyo basi kama umepata hasara hutalipa kodi na kodi uliyolipa by provision utai-"carryfoward mwaka wa biashara unafuata.
  Mwisho ni kwamba taasisi nyingi za serikali na mashirika binafsi yanapenda kufanya biashara na kampuni zaidi kuliko mtu binafsi.
  Kwa sasa somo liishie hapa, kama kuna maswali na marekebisho ruksa.
  By mshauri wa biashara yako.
   
 10. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  nimeiona na nimeijibu mkuu, mihangaiko ndo imenifanya nikachelewa kuijibu
   
 11. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inavoelekea ni msomi mahiri wa mambo haya.
  Je, nini gharama ambazo hazoepukiki kila mwaka ukiachilia mbali kupata faida au kukosa faida. Kuna mpiga mahesabu anayetambuliwa na serikali na mambo mengine kama yapo.
  Please mwalimu wetu mwema, usichoke kutufubdisha kwa njia hii.
   
 12. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  duh, mod alihamisha hii post nimeitafuta sana jukwaa iliyokuwepo hadi nikahisi imefutwa. Turudi kwenye swali la msingi, gharama(expenses) zinatofautiana kulingana na aina ya biashara,ila kuna zile common ktk biashara yeyote ile na kama nitakosea wahasibu na wakaguzi na maofisa kodi wenzangu mtanisaidia. Garama(expenses) ni kama ifuatavyo
  1. Rent(in case eneo ofisi umepanga).
  2. Electricity bill
  3. Phone & internet charge
  4. Salary & wages
  4. Fixed assets depreciations
  5. Bank charges
  6. Repair & maintanance
  7. Transport charge
  8. Consultation fees
  9. Rates
  10. Insurance
  NB: "hizi (expenses)garama sio mandate ziwepo, na hailazimishwi kuingia hizo garama(expenses). Ila kuna zile ambazo ni lazim ulipe brela maadam una kampuni ambazo ni pamoja na kufile annual return(tsh 15,000) kucertify doc sh2,000/page, kubadili jina kampuni 15,000, na kureserve jina la kampuni 50,000 n.k".
  List ya expenses ina vitu vingi sana ambavyo kwa lugha ya kiuhasibu tunaita (operating expenses) yaani gharama ulizoingia ili kupata mauzo/kuuza kitu fulani.
  Hizi expenses zinatofautiana kulingana na nature ya biashara na lazima zitolewe kwenye gross profit/loss ili upate net profit/loss ambayo ndo inachajiwa kodi kwa anayeoperate biashara inform of company(tofauti na ambaye hafanyi biashara kama kampuni kwani huchajiwa kutokana na mauzo bila kudeduct xpenses/ bila kujali umepata faida au hasara). Na kuna wakati tra wanaweza kukufanyia field audit watahtai kuona supporting doc za hzo expense kama risit, payroj salary, lease contract etc.
  Naamini nimejitahidi kwa kadiri ya uwezo kujibu swali lako, vinginevyo sijakuelewa. Pia unaweza kunipm kwa ushauri wa mambo yahusuyo biashara kodi kwa ujumla( am professional in the field).
  mpiga mahesabu anayetambulika ni mtu yeyote ambaye ana CPA(CERTIFIED PUBLIC ACCOUNTANT)
   
 13. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  mkuu Voice of Wisdom.
  Nimeku pm. sijui kama imekufikia.
   
 14. Penguin-1

  Penguin-1 JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naanza kupata picha sasa....
   
 15. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  imefika na nimekujibu ndugu
   
 16. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Pia unaweza kupata maelezo mengine kupitia BRELA
   
 17. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ujumbe umetulia
   
 18. cerengeti

  cerengeti JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,165
  Trophy Points: 280
  1. unatakiwa kwanza kuchagua jina la kampuni yako ndugu,
  jina likishathibitishwa na brela kuwa linafaa

  2.utatakiwa kuandaa memorandums & articles of association the utazifile kwa registra of co(BRELA) baada ya hapo registra atakupa certificate of registration, hiki cheti kitaonyesha kuwa tayari kampuni imesajiliwa(imekuwa legal entity) baada ya kukamilisha michakato mingine.

  3.gharama za kusajili kampuni ni kama ifutatavyoregistration fee (tsh 50,000-300,000) hii inategemeana na share capital kwa kampuni zenye share capital, anbayo share capital inaanzia 20,000 na kuendelea, filing fee anbayo ni 45,000, nastamp duty ambayo ni 12,200

  4. gharama lega consultation fees utakayempata akakuandalia/ kukusainia hizo memorandums & article of associations, zinaweza kupelekea jumla kuu hadi ya tsh 500,000+ kutegemeana na wakili unayemtumia.

  kwa ushauri zaidi nitafute 065 308308
   
Loading...