Brother Kaka.
Member
- May 11, 2015
- 66
- 32
Wakuu,
Mwaka jana nilianzisha kiofisi changu kidogo tu mtaani cha secretarial services (hasa kuprinti na kuscan kwani nilibaini kuwa nilipo ni njia kubwa ya wanachuo) baada ya kupata laptop refurbished, scanner na printer ndogo.
Kwa kuwa sipendi migogoro,
Nikaenda TRA nikakadiriwa kulipa 150,000/= kwa mwaka na nikajitahidi kulipia kwa awamu zote nne.
Ingawa muda mwingi biashara inayumba,
Najitahidi kuvumilia, kwani kinachoniokoa ni kwamba eneo nililopo ni la kilocal sana hivyo hata pango yake ni ndogo (nachangia Elfu 25 kwa mwezi)
na ofisini ninakaa mwenyewe,
Hivyo hata nikipata Elfu tano ya kula kwa siku- nashukuru kuwa mkono unaenda kinywani.
Changamoto imekuja baada ya kwenda TRA majuzi ili nifanye malipo kwa kuepuka usumbufu,
Naambiwa mwaka huu inabidi nilipe 318,000/=,
Nikajaribu kujitetea kuwa mauzo yangu ni finyu sana,
Hicho kiasi kinanibana kiuchumi-
Afisa wa TRA anang'ang'ania kuwa haiwezekani mwaka huu nilipe sawa na ile ya mwaka jana, ni lazima iongezeke mara mbili.
Kwa kifupi nalazimishwa kulipa kiwango cha juu cha kodi kuliko mauzo yangu ya mwaka (Turnover).
Kwa elimu yangu ndogo, ninavyotambua ni kwamba
- Kwa mauzo (turnover) ya kuanzia 4,000,000 TZS hadi 7,500,000 TZS kwa mwaka,
Kodi ni 150,000/=.
- Wakati kwa mauzo ya zaidi 7,500,000 hadi 11,000,000 TZS kwa mwaka,
Kodi ni 318,000/=
(Na zaidi kadri ya ukubwa wa mauzo).
Na mimi mauzo yangu hayafiki hata 5,000,000/= kwa mwaka.
Tumevutana kwa muda mrefu,
Hatimaye nimeondoka ofisini kwao bila kufikia muafaka.
Nishaurini wakuu,
Natakiwa nifanye nini ili wakubali niendelee kulipa kiasi kilekile cha awali?