Ushauri: Nalazimishwa kulipa kodi kubwa kuliko mauzo yangu.

Brother Kaka.

Member
May 11, 2015
66
125
Wakuu,
Mwaka jana nilianzisha kiofisi changu kidogo tu mtaani cha secretarial services (hasa kuprinti na kuscan kwani nilibaini kuwa nilipo ni njia kubwa ya wanachuo) baada ya kupata laptop refurbished, scanner na printer ndogo.

Kwa kuwa sipendi migogoro,
Nikaenda TRA nikakadiriwa kulipa 150,000/= kwa mwaka na nikajitahidi kulipia kwa awamu zote nne.

Ingawa muda mwingi biashara inayumba,
Najitahidi kuvumilia, kwani kinachoniokoa ni kwamba eneo nililopo ni la kilocal sana hivyo hata pango yake ni ndogo (nachangia Elfu 25 kwa mwezi)
na ofisini ninakaa mwenyewe,
Hivyo hata nikipata Elfu tano ya kula kwa siku- nashukuru kuwa mkono unaenda kinywani.

Changamoto imekuja baada ya kwenda TRA majuzi ili nifanye malipo kwa kuepuka usumbufu,

Naambiwa mwaka huu inabidi nilipe 318,000/=,

Nikajaribu kujitetea kuwa mauzo yangu ni finyu sana,
Hicho kiasi kinanibana kiuchumi-
Afisa wa TRA anang'ang'ania kuwa haiwezekani mwaka huu nilipe sawa na ile ya mwaka jana, ni lazima iongezeke mara mbili.

Kwa kifupi nalazimishwa kulipa kiwango cha juu cha kodi kuliko mauzo yangu ya mwaka (Turnover).

Kwa elimu yangu ndogo, ninavyotambua ni kwamba
- Kwa mauzo (turnover) ya kuanzia 4,000,000 TZS hadi 7,500,000 TZS kwa mwaka,
Kodi ni 150,000/=.

- Wakati kwa mauzo ya zaidi 7,500,000 hadi 11,000,000 TZS kwa mwaka,
Kodi ni 318,000/=

(Na zaidi kadri ya ukubwa wa mauzo).

Na mimi mauzo yangu hayafiki hata 5,000,000/= kwa mwaka.

Tumevutana kwa muda mrefu,
Hatimaye nimeondoka ofisini kwao bila kufikia muafaka.

Nishaurini wakuu,
Natakiwa nifanye nini ili wakubali niendelee kulipa kiasi kilekile cha awali?
 
Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,133
2,000
Kwa kusema kweli watu binafsi kwenye kodi wanaumia sana kuliko hata kampuni. Kama ungekuwa na kampuni ungeweza kupeta tu hadi pale utakapoweza kutengeneza faida, ila kwa mtu binafsi ukikadiriwa ndo basi tena hakuna namna nyingine ni lazima ulipe. Mimi nakushauri mambo mawili:
1. Tsh 318,000/= kwa mwaka ni sawa na Tsh 26,500/= kwa mwezi = 79,500/= kwa kila quarter. Kama hutaki migogoro jikamue lipa.
2. Kama kweli mauzo ya biashara yako hayafiki Tsh 318,000/= kwa mwaka funga hiyo biashara (in fact hiyo sio biashara, itafutie jina jingine) na kisha angalia biashara nyingine au mambo mengine. TRA don't care much about performance kwa hizi biashara ndogondogo huko mitaani maana mara nyingi hawatembelei, kwa hiyo wao wanaangalia muongozo wao unasemaje tu. Kwa hiyo wakiona unaendelea na biashara na mwaka jana umelipa kodi vizuri basi wanakadiria kwamba mwaka huu biashara imekua kidogo na hata mauzo yameongezeka.

That is the way it is!
 
Kwa mantiki hiyo,

Kila mwaka kiasi cha kodi kitakuwa kinaongezeka ?
 
Prisoner of hope

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
2,438
2,000
Kwa kusema kweli watu binafsi kwenye kodi wanaumia sana kuliko hata kampuni. Kama ungekuwa na kampuni ungeweza kupeta tu hadi pale utakapoweza kutengeneza faida, ila kwa mtu binafsi ukikadiriwa ndo basi tena hakuna namna nyingine ni lazima ulipe. Mimi nakushauri mambo mawili:
1. Tsh 318,000/= kwa mwaka ni sawa na Tsh 26,500/= kwa mwezi = 79,500/= kwa kila quarter. Kama hutaki migogoro jikamue lipa.
2. Kama kweli mauzo ya biashara yako hayafiki Tsh 318,000/= kwa mwaka funga hiyo biashara (in fact hiyo sio biashara, itafutie jina jingine) na kisha angalia biashara nyingine au mambo mengine. TRA don't care much about performance kwa hizi biashara ndogondogo huko mitaani maana mara nyingi hawatembelei, kwa hiyo wao wanaangalia muongozo wao unasemaje tu. Kwa hiyo wakiona unaendelea na biashara na mwaka jana umelipa kodi vizuri basi wanakadiria kwamba mwaka huu biashara imekua kidogo na hata mauzo yameongezeka.

That is the way it is!
Umeongea vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,375

Kwa mantiki hii ina maana ni vyema kwa mfanya bishara mdogo mdogo kukwepa kwepa kulipa kodi au kuwasumbua kidogo TRA ili wajue kuwa biashara haiendi vizuri??

Kwamba kilichomponza jamaa hapo juu sio kukua au kutokukua kwa biashara yake, ila ni kihere here chake cha kulipa kodi kwa uaminifu bila usumbufu japo biashara ni ndogo??
 
busha

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,647
2,000
Minilipandishiwa makadirio kama ww...
,,nikafunga biashara then nikampeleka dogo akaingiza details zake tra,,akafungua biashara ilieile,,,

TRA inaumiza sana wajasiriamali wanao chipukia,, Hovyo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
C_O

Member
Jan 3, 2019
54
125
Nazani ni muim pia kuwa na utaratibu mzuri wa kurecord transactions zako na hapo itakupa urahisi wa kujua kwamba mwaka ujao utafanya mauzo kiasi gani kulingna na factor mbali mbali then hand them to tra kwa uwakika watakupangilia kodi ambayo haitakuumiza

Nt: jua kufungua/kuandaa income statement na balance sheet pia cash flow na financial books zngne za muimu kama huwezi tafuta muhasibu pro zen atakusadia pia na kukupa ushauri kwnye swala kama ilo

are just my thought
 
Englishlady

JF-Expert Member
Apr 11, 2013
2,031
2,000
Wakuu,
Mwaka jana nilianzisha kiofisi changu kidogo tu mtaani cha secretarial services (hasa kuprinti na kuscan kwani nilibaini kuwa nilipo ni njia kubwa ya wanachuo) baada ya kupata laptop refurbished, scanner na printer ndogo.

Kwa kuwa sipendi migogoro,
Nikaenda TRA nikakadiriwa kulipa 150,000/= kwa mwaka na nikajitahidi kulipia kwa awamu zote nne.

Ingawa muda mwingi biashara inayumba,
Najitahidi kuvumilia, kwani kinachoniokoa ni kwamba eneo nililopo ni la kilocal sana hivyo hata pango yake ni ndogo (nachangia Elfu 25 kwa mwezi)
na ofisini ninakaa mwenyewe,
Hivyo hata nikipata Elfu tano ya kula kwa siku- nashukuru kuwa mkono unaenda kinywani.

Changamoto imekuja baada ya kwenda TRA majuzi ili nifanye malipo kwa kuepuka usumbufu,

Naambiwa mwaka huu inabidi nilipe 318,000/=,

Nikajaribu kujitetea kuwa mauzo yangu ni finyu sana,
Hicho kiasi kinanibana kiuchumi-
Afisa wa TRA anang'ang'ania kuwa haiwezekani mwaka huu nilipe sawa na ile ya mwaka jana, ni lazima iongezeke mara mbili.

Kwa kifupi nalazimishwa kulipa kiwango cha juu cha kodi kuliko mauzo yangu ya mwaka (Turnover).

Kwa elimu yangu ndogo, ninavyotambua ni kwamba
- Kwa mauzo (turnover) ya kuanzia 4,000,000 TZS hadi 7,500,000 TZS kwa mwaka,
Kodi ni 150,000/=.

- Wakati kwa mauzo ya zaidi 7,500,000 hadi 11,000,000 TZS kwa mwaka,
Kodi ni 318,000/=

(Na zaidi kadri ya ukubwa wa mauzo).

Na mimi mauzo yangu hayafiki hata 5,000,000/= kwa mwaka.

Tumevutana kwa muda mrefu,
Hatimaye nimeondoka ofisini kwao bila kufikia muafaka.

Nishaurini wakuu,
Natakiwa nifanye nini ili wakubali niendelee kulipa kiasi kilekile cha awali?
Nenda ngazi ya juu mpaka kwa meneja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
683
1,000
aliyekwambia tra wanafatwa nani,ili ulipe kodi, nchi hii ishapigwa sana...so na wewe ukipata nafasi pigaa....tra hakuna tunzo ya mlipaji bora mwaka.
 
Freelancer

JF-Expert Member
Sep 22, 2008
2,856
2,000
Changamoto nayoiona ni wafanyabiashara wengi wadogo wadogo kutoweka kumbuku kumbu za mauzo na matumizi ya biashara zao. Hapo ofisa wa TRA hana taarifa yoyote ya kuitumia kupima kama biashara inakua au haikui. Mwisho wa siku anaweza kukukadiria zaidi au kidogo. Sijui hii changamoto itatatuliwa vipi?
 
Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,603
2,000
Nazani ni muim pia kuwa na utaratibu mzuri wa kurecord transactions zako na hapo itakupa urahisi wa kujua kwamba mwaka ujao utafanya mauzo kiasi gani kulingna na factor mbali mbali then hand them to tra kwa uwakika watakupangilia kodi ambayo haitakuumiza

Nt: jua kufungua/kuandaa income statement na balance sheet pia cash flow na financial books zngne za muimu kama huwezi tafuta muhasibu pro zen atakusadia pia na kukupa ushauri kwnye swala kama ilo

are just my thought
Atapata wapi mhasibu wa bure? Record keeping is not a free activity; benefit yake ita-justfy cost yake?
 
C_O

Member
Jan 3, 2019
54
125
Atapata wapi mhasibu wa bure? Record keeping is not a free activity; benefit yake ita-justfy cost yake?
Yap ndio unatakiwa kumlipa hawez akakufanyia bure nazani once ukiamua kuwa kwnye biashara ao ndo watu wa muim kuwa karbu nao itakup urahc, pia itakufngua kweny mambo meng ambayo huyajui

Infact nina bro ambae n kama rafk kwang na n mwanasheria niktaka msaad kwny certain staff ananfanyia kwa as little as 30k Tsh
 
C_O

Member
Jan 3, 2019
54
125
aliyekwambia tra wanafatwa nani,ili ulipe kodi, nchi hii ishapigwa sana...so na wewe ukipata nafasi pigaa....tra hakuna tunzo ya mlipaji bora mwaka.
As in business usipo kuwa unalipa kodi kwa wakat au hulipi kabisa nazani kuna price utalipa..

Sheria zipo wazi kabsa ambazo n rafk kwa mfanyabiashara pia na mamlka ni vitu vya muim kuvijua nazan kabla ata ujaanz biashara
 
Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
1,434
2,000
TRA ya Tanzania kazi yao kuuwa biashara za wananchi sio kukusanya kodi

Niliwahi kuwa na kabiashara Fulani maeneo ya Ilala wakaniambia kwa kuwa Tin yangu ni ya kampuni kodi ni 2m haishalishi msingi wangu shs ngapi au mauzo yangu kiasi gani na nikaambiwa ukirudi mwakani lazima itapanda nikaona isiwe shida nikaifunga biashara na Tin yao pia nikaifunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom