Ushauri: Nakusudia kukishitaki Chuo kwa uonevu wa miaka 8

Salam wakuu,

Nimekua napambana na uonevu wa wazi, manyanyaso, na kucheleweshewa thesis kwa miaka 8. Nilijiunga na chuo (jina nahifadhi) tangu mwaka 2013 nikifanya masters na tangu hapo chuo kimenipotezea muda, fedha na usumbufu mwingi sana huku ukiritimba wa hali ya juu ukigubika kila mlango wa chuo ninaopeleka malalamiko yangu.

Mpaka naandika uzi huu bado sijahitimu licha ya kuweka jitihada kubwa katika masomo yangu. Mikasa ni mingi ila yote inamlenga supervisor wangu wa kike (nina supervisor wawili) ambae kwa mda mrefu amekua Akinikwamisha kwa makusudi kabisa licha ya kua muaminifu katika kutekeleza kila jukumu langu, mwanamama huyu mwenye elimu ya Phd (jina nalihifadhi) amekua akinipatia wakati mgumu huku mara kadhaa akinipa vitisho vikali. Nimekua nikisingiziwa mambo mengi na kila mlango naokwenda nakuta jina langu linatuhuma nyingi za uongo kwa mfano tuhuma ya kughushi sahihi yake na nilipotoa vielelezo na ushahidi wa kutohusika kughulishi nyaraka zile nikakalipiwa na kuambiwa ninyamaze na nisiseme popote kua nimesingiziwa ubaya huo.

Kila mamlala ya chuo nayoifikia ni kama mwanamama huyu amekwisha haribu kabisa jina langu. Supervisor wangu wa kiume ambae ni prof amekua anajua magumu nayopitia na amekua ananifariji sana kua nisikate tamaa na amekua ananiambia anafahamu jinsi navyokwamishwa (japo kuna mangi niliyopitia hayafahamu na sijawahi kumwambia) prof ni mtu muungwana sana na mkarimu kwa hulka yake.

Nimekua mtu wa huzuni kwa miaka mingi ila sasa nakurudia kwenda mahakamani nikaiambie mahaka na dunia yote niliyopitia na kuiomba mahakama nitendewe haki.

Shida yangu hapa ni kua sina fedha ya kuendesha kesi hii ikichangiwa na kutumia fedha nyingi kushughulikia maswala ya chuo safari za mara kwa mara kufuatilia (chuo kipo mkoa tofauti na nilipo) nimejikuta naingia kwenye madeni mengi hata kuadhiri ustawi wa familia yangu. Katika hali hii nauona ugumu nitakaoupata kuendesha kesi tena kesi dhidi ya chuo kikubwa kabisa hapa nchini.

Najua Jamii Forums kuna wajuzi wengi wa mambo mbalimbali ninaomba kupata ushauri wa jinsi gani nitafanikisha kusudio langu la kupeleka shauri langu mahakamani kutokana na uwezekano wa kupata msaada ofisi yoyote ya chuo kupotea huku manukato ya mwanamama huyu supervisor wangu yakinukia kila ofisi ya chuo. (Lugha ya picha).

Nashukuruni sana najua hapa nitapata mawazo mengi mazuri kwa maana Jamii Forum ni mahala pa watu makini. Asanteni.

(Mkasa huu nimeandika kwa ufupisho sana kama ukitaka ufafanuzi wa jambo niulize ili unipatie ushauri kama unavyokusudia).

Pole sana ndugu, hii ni changamoto kubwa kwako lakini ukipata msaada mzuri wa mawazo kwa watu sahihi utalimaliza hili jambo ndani ya muda mufupi sana hapo hapo chuoni kwako. Huna haja ya kuhama chuo. Tatizo kubwa lipo kwako mwenyewe, jaribu kufikiria kwa mtazamo huo na uchukue hatua. Jiulize tu mwenyewe, angekua ni mtu mwingine kwenye tatizo kama lako hilo ingemchukua pia miaka 8 kutafuta suluhu?

Soma namna ya kumfanya supervisor aendane na mipango yako. Soma article za PhD, ni sawa tu na kwa masters.
 
Madam mmoja aliniita ofisini eti ananiambia nijiudhuru kusoma chuo...aaaaaaaaaa madama.siku moja nikashika tako la madam mambo yakawa bulbul.
 
Pole sana ndugu mwenyezi Mungu akupe nguvu na kukuvusha kwenye kipindi hiki kigumu kwenye maisha yako kwani miaka 8 simchezo mtoto anazaliwa mpaka anafika darasa la tatu. Kweli kuna binadamu wenye roho ngumu sana yaani ni bora angekufelisha mapema ungejua moja ungekuwa sasa hivi umeshaanza chuo kingine na labda ungekuwa umeshahitimu kuliko huo upuuzi aliokufanyia. Roho imeniuma sana hasa ukifikiria pesa ilivyo ngumu kupatikana na ikipatikana mnagawana pasu kwa pasu na tozo. Na mbaya zaidi kuliko vyote ni muda aliokupotezea

Lakini ni vizuri tu ukataja jina la chuo ili sisi wengine tunaosomemsha watoto, ndugu na jamaa tusipeleke watoto wetu hapo. Utakuwa umetusaidia sana kwani siku hizi vyuo ni vingi na vinafundishi kozi nyingi zinazoendana. Ili tusije tukakomaa kupeleka watoto au ndug zetu hapo kwenye hicho chuo chenye mwalimu mpuuzi wakati tungeweza kuwapeleka kwenye vyuo vingine vyenye walimu wenye weledi na kazi zao. Ila hicho chuo nacho cha ajabu sana mpaka leo hii bado kina walimu wenye hulka za kizamani za kukamata wanafunzi kuwa sifa labda tu kama ni hulka ya huyo mwalimu mmoja
 
Ungetaja jina la chuo na college pamoja na program uliyosoma,utasaidia wengi,kuficha haisaaidii chochote Kwa hatua uliyofikia
 
Hiyo kozi ya masters ni miaka mingapi, na ilianza 2013 na kuisha lini, pia tueleze, umegomba nimi na huyo mwanamama?
 
Kwa Tanzania ya sasa kama una Masters inatosha kabisa Phd itakusaidia nini. Achana nayo.
 
Natamani nikushauri lakini naogopa usije kosa yote.Japo Kuna mtu lilimkuta Kama lako na ushauri niyompa ulisaidia akakwaa PhD yake bila utata
 
Kwa Tanzania ya sasa kama una Masters inatosha kabisa Phd itakusaidia nini. Achana nayo.
Mimi niliwahi kujiambia hivi,kama masters na phd za kitanzania ni yale ninayoshuhudia ndani ya taifa hili hasa enzi ya awamu 5,nilijiambia sitaihitaji hiyo masters au hiyo phd, japo kwa wakati huu nimerejea kuutafakari uamuzi wangu wa wakati huo.
 
Pole sana walimu chuoni huwa wanalindana sana, staki kukumbuka pain niliyopitia kwenye thesis yangu ilikuwa kipindi kigumu na stress na huzuni nashukuru Mungu nilimaliza. Walimu wa vyuoni Wana roho mbaya sana na wivu na hupenda kuona watu wakiteseka
 
Ni roho za kimasikini tu zinawasumbua.
 
Salam wakuu,

Nimekua napambana na uonevu wa wazi, manyanyaso, na kucheleweshewa thesis kwa miaka 8. Nilijiunga na chuo (jina nahifadhi) tangu mwaka 2013 nikifanya masters na tangu hapo chuo kimenipotezea muda, fedha na usumbufu mwingi sana huku ukiritimba wa hali ya juu ukigubika kila mlango wa chuo ninaopeleka malalamiko yangu.

Mpaka naandika uzi huu bado sijahitimu licha ya kuweka jitihada kubwa katika masomo yangu. Mikasa ni mingi ila yote inamlenga supervisor wangu wa kike (nina supervisor wawili) ambae kwa mda mrefu amekua Akinikwamisha kwa makusudi kabisa licha ya kua muaminifu katika kutekeleza kila jukumu langu, mwanamama huyu mwenye elimu ya Phd (jina nalihifadhi) amekua akinipatia wakati mgumu huku mara kadhaa akinipa vitisho vikali. Nimekua nikisingiziwa mambo mengi na kila mlango naokwenda nakuta jina langu linatuhuma nyingi za uongo kwa mfano tuhuma ya kughushi sahihi yake na nilipotoa vielelezo na ushahidi wa kutohusika kughulishi nyaraka zile nikakalipiwa na kuambiwa ninyamaze na nisiseme popote kua nimesingiziwa ubaya huo.

Kila mamlala ya chuo nayoifikia ni kama mwanamama huyu amekwisha haribu kabisa jina langu. Supervisor wangu wa kiume ambae ni prof amekua anajua magumu nayopitia na amekua ananifariji sana kua nisikate tamaa na amekua ananiambia anafahamu jinsi navyokwamishwa (japo kuna mangi niliyopitia hayafahamu na sijawahi kumwambia) prof ni mtu muungwana sana na mkarimu kwa hulka yake.

Nimekua mtu wa huzuni kwa miaka mingi ila sasa nakurudia kwenda mahakamani nikaiambie mahaka na dunia yote niliyopitia na kuiomba mahakama nitendewe haki.

Shida yangu hapa ni kua sina fedha ya kuendesha kesi hii ikichangiwa na kutumia fedha nyingi kushughulikia maswala ya chuo safari za mara kwa mara kufuatilia (chuo kipo mkoa tofauti na nilipo) nimejikuta naingia kwenye madeni mengi hata kuadhiri ustawi wa familia yangu. Katika hali hii nauona ugumu nitakaoupata kuendesha kesi tena kesi dhidi ya chuo kikubwa kabisa hapa nchini.

Najua Jamii Forums kuna wajuzi wengi wa mambo mbalimbali ninaomba kupata ushauri wa jinsi gani nitafanikisha kusudio langu la kupeleka shauri langu mahakamani kutokana na uwezekano wa kupata msaada ofisi yoyote ya chuo kupotea huku manukato ya mwanamama huyu supervisor wangu yakinukia kila ofisi ya chuo. (Lugha ya picha).

Nashukuruni sana najua hapa nitapata mawazo mengi mazuri kwa maana Jamii Forum ni mahala pa watu makini. Asanteni.

(Mkasa huu nimeandika kwa ufupisho sana kama ukitaka ufafanuzi wa jambo niulize ili unipatie ushauri kama unavyokusudia).
Mtongozee, yaani wewe mtongoze tu, mpaka aingie king. Show piga la kibabe mpaka aanzae kukuamkia tu. Hapo utafanikisha malengo yako ndani ya wiki moja tu.
 
Back
Top Bottom