Ushauri: Nahitaji kununua gari ninunue lipi kati ya haya?

Aug 22, 2013
66
66
Ndugu zangu habari zenu,

Nimechoka kubanana kwenye daladala nataka japo na mimi ninunue kagari cha kunizunguusha mjini ila nipo njiapanda kati ya Honda fit,Toyot ist na Audi A4 ipi inaweza kunifaa hasa kwenye swala la upatikanaji wa spea matumizi ya mafuta na ubora kwa ujumla.
 
Ngoja wataalamu waje kukushauri, mi nitajisemea tu Toyota IST kwani naona Airtel wanazitoa
 
Toyota ndio magari yanayoongoza kwa speak kupatikana kirahisi, na hilo ndio muhimu. Jihadhari usije nunua gari ambao spea inabidi uziagize Nairobi.

Vv
 
ndo nini hiyo speak!!gari gani ambayo spea zinaagizwa Nairobi!
 
Kwa hizo gari ulizoweka hapo kwa kuwa ndo order of preference uliyonayo ningekushauri ununue IST. Sababu ushapewa na wadau hapo juu. Honda itakusumbua spares plus AUDI
 
Taarifa imefika unataka kununua gari.... Nakushauri pitia Garage mbili tatu watakuambia maana si ndio watengenezaji wa kila siku?????????? Huku utaambiwa ist zetu ni baby walker wakati hata baiskeli hatunazo.
 
Kama unahofia mafuta bora ununue pikipiki,1ltr unaenda hadi 25km,Mnunuaji wa gari aangalii ulaji wa mafuta,kama umeweza ku-make hadi kufikia uamuzi wa kununua gari ya thamni zaidi ya 10m utashindwaje mafuta?
 
Kwa Tanzania magari Aina ya Toyota ndiyo prefence, kwani spare zake ni nyingi kuliko gari aina yoyote zinazo onekana hapa.
 
Pia ndiyo magari yanayoongoza kuibiwa kirahisi, ama kuchomolewa vifaa vyake na baadaye vifaa hivyo kuvikuta madukani. Wezi hawaangaiki na wizi wa magari ambayo yatawapa shida kupata "Soko".
 
shida ya toyota spare zipo nyingi ila hazidumu, kila wakati unanunua spea. Hayo magari mengine spare zake ni mkataba wa kudumu
 
Kwanza jiulize unahela ya kununua gari?,bila shaka unayo ndo maana ukasema,pili jiulize unahela ya kulimudu gari kiuendeshaji?,isije fika mahala ukaanza hadi kutumia hela ya mambo muhimu ktk kufanya gari liwe barabarani,watoto wasije punguziwa matumizi ili tu gari liwe barabarani,naamini uko makini na halitatokea hili,t
Tatu,una hitaji gari kwa matumizi gani?,isijekuwa ni mkurupuo tu wa kutaka kuwa na gari,tambua kwanza matumizi unayotaka kufanya nanhilo gari ndoujiulize utanunua gai gani kulingana nanmatumizi,km ni la biashara tafuta gari linaloendana na aina ya biashara,
Haya ni baadhi tu ya mambo ya kukuongoza na kujiuliza kabla ya kununua gari,kitendo cha ww kuuliza tu humu ni ushahidi tosha kuwa ww ni mgeni na magari hvo nnaloshauri usikurupuke,haya magari yanamatatizo zaidi ya tunavoyaona watu wakimiliki,km si muda sahihi usinunue,na km ni muda sahihi tafuta gari sahihi kulingana na unachotaka kulifanyia,epuka magari ya mikononi na midomoni mwa watu
 
Kama unahofia mafuta bora ununue pikipiki,1ltr unaenda hadi 25km,Mnunuaji wa gari aangalii ulaji wa mafuta,kama umeweza ku-make hadi kufikia uamuzi wa kununua gari ya thamni zaidi ya 10m utashindwaje mafuta?

fuel economy ni muhimu kwa mtu wa kipato cha kawaida, usije jikuta gari inatafuna mafuta ya elfu50 kila siku wakati mshahara wako 1.5M kwa mwezi, utaanza kutembea kwa miguu kila ukikutana na jirani unaanza kujishauwa uko kwenye kampeni ya kupambana na kitambi wakati mtu mwenyewe uko safi hauna kitambi. Ukiona mtu anaingia petrol station na kujaza mafuta ya elfu6 ujue hiyo gari inambaka vibaya mno, akikuta watoto wa jirani wanasubiri daladala kwenda shuleni anawachunia wakati wanasoma shule moja na wake. Wengi hatujuwi kujipimia kulingana na uwezo, mtu anajikamua kununua Crown Majesta wakati safari yenyewe mara moja kwa mwaka, tena haendi zaidi ya morogoro, anataka kuwaonesha walimwengu tu kuwa ana gari "kali"..gari kali inakuwaga mtumba!? Kinachofuata hapo ndani ya nyumba anakuwa mkali tu, mama akisema anataka kwenda sokoni anazua visingizio, watoto kuwapeleka sehem anasema mko wengi pandeni daladala....anawaza mafuta tu!
 
Du kama ndio hivyo basi bora asinunue gari,ya nini ninunue gari ya cc 500 nikipitiwa na lori tu napepesuka kisa ni fuel economy? For me nah no go so........
 
lipitwe na roli ukienda wapi, jangwani kufundisha twisheni?...lol

Hata hapa Town,sometimes barabara inakuwa haina jam kwahiyo ukipishana na daladala lazima upepesuke kama haujapakiza mtu unaweza ukajikuta mataroni,Vigari hivi vya cc mbili au tatu kuitafuta morogoro ni mtihani.
 
Carina TI mpango mzima hautajuta

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwanza jiulize unahela ya kununua gari?,bila shaka unayo ndo maana ukasema,pili jiulize unahela ya kulimudu gari kiuendeshaji?,isije fika mahala ukaanza hadi kutumia hela ya mambo muhimu ktk kufanya gari liwe barabarani,watoto wasije punguziwa matumizi ili tu gari liwe barabarani,naamini uko makini na halitatokea hili,t
Tatu,una hitaji gari kwa matumizi gani?,isijekuwa ni mkurupuo tu wa kutaka kuwa na gari,tambua kwanza matumizi unayotaka kufanya nanhilo gari ndoujiulize utanunua gai gani kulingana nanmatumizi,km ni la biashara tafuta gari linaloendana na aina ya biashara,
Haya ni baadhi tu ya mambo ya kukuongoza na kujiuliza kabla ya kununua gari,kitendo cha ww kuuliza tu humu ni ushahidi tosha kuwa ww ni mgeni na magari hvo nnaloshauri usikurupuke,haya magari yanamatatizo zaidi ya tunavoyaona watu wakimiliki,km si muda sahihi usinunue,na km ni muda sahihi tafuta gari sahihi kulingana na unachotaka kulifanyia,epuka magari ya mikononi na midomoni mwa watu

zilipoingia simu maneno hayahaya, mara vocha, mara chaji, wakati vocha zilikuwa zinaitwa dollar 5, 10 etc, sasahv gari ni sehemu ya maisha ya yeyote anayeweza kumiliki, hakunahaja ya kumtisha mtu, ionekane kumiliki gari ni kuwa bilinea, pia ukiwa na usafiri wa maana utendajiwako unaboreka.
 
Back
Top Bottom