Ushauri: Nahitaji kufungua library ya kuuza movies kwa bei ya jumla

muvika online

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
374
283
Habari wadau wa JF,

Nilikuwa naomba msaada + Ushauri wenu,

Nina Pc, Printer pamoja na kamtaji kadogo lengo kubwa ni kutaka kuwa msambazaji na muuzaji wa movies pamoja na series kwa bei ya jumla jumla yaani nachukua cd moja natoa copy hata 50 kisha nikuwa nawauzia wale wanao kodisha CD, sasa nilikuwa naomba ushauri kuhusu hii biashara je itanikwamua kimaisha au ndo nitaishia hewani

UPDATES
*Nahitaji Ushauri, maoni, pendekezo na vyote vilivyo sahihi kuniambia, kejeli na dharau sihitaji
 
Nachokiona utaishia jela kwani huo ni uvunjaji WA haki miliki mzee Nape akikukuta we ni WA keko mkuu
Najua utasema movie za nje bado kimsingi hatutakiwi kukopy ndio manaa matorrent yanafungwa kila siku kwakuwa kudownload free stuffs sio legal.
 
Library (maktaba) huwa wanauza au wanakodisha? Au ulimaanisha duka la kuuza movies? Au pengine mimi sijaelewa vizuri!...
 
Nachokiona utaishia jela kwani huo ni uvunjaji WA haki miliki mzee Nape akikukuta we ni WA keko mkuu
Najua utasema movie za nje bado kimsingi hatutakiwi kukopy ndio manaa matorrent yanafungwa kila siku kwakuwa kudownload free stuffs sio legal.
asante kwa ushauri mkuu
 
Ni bora ukanunue original movie kwa bei ya jumla halafu uuze kwa rejareja, kununua cd moja na kuipiga copy ni kosa kisheria..utafungwa jela mkuu.....
na pia kuhusu series/season ni bora ukanunue kwa bei ya jumla kwa wale ma-djs wanaozitafsiri au hata zile ambazo hazijatafsiriwa pia...Nadhani hii ndio itafaa zaidi
 
asante mkuu kwa ushauri wako, madjs wanalinga sana mkuu nimeisha wasiliana nao wananizungusha kila mala
 
asante mkuu kwa ushauri wako, madjs wanalinga sana mkuu nimeisha wasiliana nao wananizungusha kila mala
inategemea na eneo ulilopo..ungekuwa moshi au Arusha tungefanya business connection na ungefaidi..kama upo Moshi au Arusha embu nitafute tuongee zaidi
 
Back
Top Bottom