Ushauri: Nahitaji kuanzisha biashara ya maziwa fresh na mtindi

Ibn Abasi

Member
Jun 24, 2016
21
10
Habari zenu wadau wa jf.

Mimi ni kijana umri miaka 25, nipo Dar es salaam. Nimepata wazo la kuanza kusambaza kwa reja reja mitaani maziwa ya ng'ombe ya fresh na mtindi yanayotengenezwa viwandani mfano Asasi, Tanga fresh, Dar Fresh n.k. Nina Kadell kadogo kanachoweza kuchukua maziwa 45 hadi 50. Naomba ushauri wenu kuhusu wazo hili.

Ni aina gani bora ya maziwa kati ya hayo niliyotaja na mengineyo yanapendwa zaidi, na Je, ni wapi soko lipo zaidi la uhitaji wa bibhaa hii MAZIWA FRESH NA MTINDI.

Ntafurahi kama nitafahamishwa mahala kwa kuyapata kwa jumla na bei nzuri. NATANGULIZA SHUKRAN ZA DHATI KWENU, @ Ibn Abasi
 
Back
Top Bottom