Ushauri : Nahisi nimeambukizwa ugonjwa wa zinaa

gonamwitu

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
703
707
Habari wana jamiiforum wiki kama mbili zilizopita kuna mwanamke nilifanya nae mapenzi bila kinga baada ya kufanya nae mapenzi after one week kuna mabadiliko kadhaa yamejitokeza na ninahisi kaniambukiza ugonjwa wa Zinaa

1: Nikikojoa nasikia maumivu sana na baada ya kumaliza kukojoa nikikaa kuna vitu kama usaha vinatoka kwenye tundu langu la uume.

2: Uume ukisimama unauma au nikiubinya unauma.

Wadau kwa dalili nilizozitaja hapo juu je ni dalili za gonjwa gani la zinaa? Na je tiba yake ikoje na gharama zake? Je naweza tibiwa kwenye hata dispensary za mtaani? Je naweza kupata dawa kwenye maduka ya dawa nisaidieni mdogo wenu.

NB: Nimekoma kupiga mechi bila ndomu na nikipona nitatumia ndomu kwa kila tendo, eenh Mungu nisaidie.
 
Pole sana mkuu Kwa uzoefu wangu utakua Una gonorrhoea au Chlamydia. Usione aibu wahi sana. Yani narudia tena wahi sanaaa hospitali . Usiende pharmacy wala Duka la dawa nenda hospitali mapema sana yanatibika vizuri Tu wala usiwe na hofu. Kua makini siku nyingine na pole
 
Gono bahati ya mtu tu kuponyoka ila inaambukiza kirahisi zaidi ya ngoma ... haya madude kama mafua tu unaweza vaa ndom ukikosea kuichomoa kama demu analo unalivaa
 
Kapime tu, hiyo inauwezekano mkubwa ni Gonorrhoea. Sasa hivi ugonjwa unaotisha ni COVID-19 haya mengine wala hospitali hawawezi kukutenga.
 
Gono bahati ya mtu tu kuponyoka ila inaambukiza kirahisi zaidi ya ngoma ........haya madude kama mafua tu unaweza vaa ndom ukikosea kuichomoa kama demu analo unalivaa
Ndo ivo mkuu muda mwingine unavaa na condom Ila bahati mbaya inatokea
 
Wacha nikutowe wasi wasi, unaposema unahisi kuwa umeambukizwa gonjwa la zinaa, hakuna haja ya kujihisi au kuwa na wasiwasi kwani ni 100% hakika umelikwaa gonjwa la zinaa.

Pili umenichekesha eti mola nisaidie, sasa ndio unamkumbuka mola enhe? Halafu hapo hapo unaahidi ukipona kuendelea kuzini ila yu utatumia condom! nimeshindwa kutocheka. Kwa taarifa yako tu condom haizuii aina ya ugonjwa wowote wa kuingiliana kimaumbile 100%, soma small prints zilizopo katika box yake.
 
Yes nimesoma some articles on google it's gonorrhea buddy,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom