Naomba ushauri na tiba ya kikohozi na mafua kwa watoto

Jaribu hii dawa; Mchanganyiko wa Asali ya nyuki wadogo, kiini cha yai bichi la kienyeji, magadi ya asili (yapo sokoni), binzari, limao, na kitunguu saumu punje mbilimbili ziponde ponde. Changanya kwa kipimo chochote then mpe mtoto kijiko kidogo cha chai kila siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku saba. Pia akilala usimfunike na Blanketi, mfunike na Duveti. Pia asile vitu vyenye asili ya utamu kama lollipop, pipi na banzoka.
 
Dawa na dose kiboko ya hilo tatizo la mwanao ni: 1. mpatie mboga za majani na azile kama mbuzi/ ng'ombe/ sungura, 2. mpatie maziwa ya kutosha, 3. mpatie matunda ya kutosha, 4. mpatie mayai ya kuku wa kienyeji, 5. mpatie nyama ya kuku, ngo'ombe, na samaki mara kwa mara ikiwemo dagaa, 6. anywe maji ya kunywa mengi kwa siku mpaka uone mkojo wake unafanana na maji wala sio kahawa, 7. hakikisha nyumba yako kwa ndani hakuna vumbi, na hachezi kwenye vumbi nje (kama unaweza weka pavement stones kwenye uwanja wa nyumba yako).

asante
 
Jaribu hii dawa; Mchanganyiko wa Asali ya nyuki wadogo, kiini cha yai bichi la kienyeji, magadi ya asili (yapo sokoni), binzari, limao, na kitunguu saumu punje mbilimbili ziponde ponde. Changanya kwa kipimo chochote then mpe mtoto kijiko kidogo cha chai kila siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku saba. Pia akilala usimfunike na Blanketi, mfunike na Duveti. Pia asili vitu vyenye asili ya utamu kama lollipop, pipi, banzoka.....

shukran
 
Nipm kuna vitu nikuulize may be naweza kukusaidia.
mkishatoka mje na huku Jukwaani kwani na sisi tuna watoto waenye Asthma
mm mwanangu kweli ana kikohozi kibaya hasa kwani kinamshika usiku wa manane kuanzia saa nane usiku au saa 11 alfajiri nimetumia dawa zote Coldrill Abdominal hata za miti shamba za huko Meru, za kiarabu, asali, tangawizi nk

  • nakubaliana tujaribu kwanza kuangalia minyoo,
  • Kimeo (kidaka tonge) wanadai kikiwa kirefu kinakereketa
Ni vizuri tukapeana ushauri na kumpa ushauri mwenzetu kwa faida yetu na Post hizi zipo kwingine kwa ufafanuzi na msaada
https://www.jamiiforums.com/jf-doct...kikohozi-kwa-watoto-chini-ya-mwaka-mmoja.html
 
Mimi wa kwangu alipokuwa na miezi 9 alianza kukohoa kwa zaidi ya miezi 4 nikamnywesha madawa ya kifua ya kila aina but nilipoenda hospitali ya mwananyamala kumpima wakasema ana TB inayosababishwa na numonia. Hapo ikabidi aanzishiwe dozi kwa muda wa miezi 6, baada ya kumaliza dozi suala la kukohoa kwake likawa limeisha. Akikohoa basi ni kipindi kile watu wanakuwa wanakohoa wengi napo hupona mara moja.
 
nimekupata
 
Mpeleke Muhimbilia kwa specialist wa koo, amenisadia sana tatizo hilo, mwanangu kwa sasa anaendelea vizuri.

Ni kweli....mtoto huyu atakuwa na shida kwenye koo....anawezekana kabsa anamatezi...waone madaktari wa ent....vinginevyo....hakuna dawa....hapo....nina uzoefu...na hili tatzo....
 
Jaribu hii dawa; Mchanganyiko wa Asali ya nyuki wadogo, kiini cha yai bichi la kienyeji, magadi ya asili (yapo sokoni), binzari, limao, na kitunguu saumu punje mbilimbili ziponde ponde. Changanya kwa kipimo chochote then mpe mtoto kijiko kidogo cha chai kila siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku saba. Pia akilala usimfunike na Blanketi, mfunike na Duveti. Pia asili vitu vyenye asili ya utamu kama lollipop, pipi, banzoka.....

ninayo asali ya nyuki wadogo kama mtu anataka pia
 
Jaribu hii dawa; Mchanganyiko wa Asali ya nyuki wadogo, kiini cha yai bichi la kienyeji, magadi ya asili (yapo sokoni), binzari, limao, na kitunguu saumu punje mbilimbili ziponde ponde. Changanya kwa kipimo chochote then mpe mtoto kijiko kidogo cha chai kila siku asubuhi, mchana na jioni kwa siku saba. Pia akilala usimfunike na Blanketi, mfunike na Duveti. Pia asili vitu vyenye asili ya utamu kama lollipop, pipi, banzoka.....

Duveti ni nini?
 
Pole bbe, mie wa kwangu ana matatizo kidogo yafanane Na ya kwako ila wangu hali vitu solid, anakunywa maziwa special ndio yanamfanya aishi. Akikooa kidogo Ni mpaka atapike ndio aridhike.
Kuhusu mtt wako jaribu yafuatayo
1. Inawezekana Ana allergy Na baadhi ya vyakula mnavyompatia mfano maziwa, mayai, Karanga, au ata mafuta ya kupikia. Kwa hiyo inabd ujaribu kimoja kimoja ili ujue kama kuna isiyomfaa.
2. Jaribu kumlisha vyakula kidogo kidogo ili ata akikooa asitapike. Pia mchunguze ulaji wake labda Ana tatizo wakati wa kumeza ambayo inasababisha chembe chembe ya vyakula kuingia kwenye viriba hewa.
Pia mlishe vyakula vyenye calories kubwa mfano uji wenye siagi ili ata akila kidogo asidhoofike
3.Madawa mengi ya kikohozi Ni useless kwa hiyo jaribu kupunguza dawa unazompatia, usimpe antibiotics unless Dr kakushauri. Jaribu kumpa PIRITON ukiona kikoozi kinamuanza, kama ikisaidia ujue Ana allergy, pia asali limao Na magadi Mara kadhaa kwa siku sio mbaya.
4. Wakati wa kulala mlaze kwa tumbo Na muwekee pillow ili kichwa Na kifua viwe juu kiasi.
 
asante sana
 
Pole dada/kaka . pia wangu alikuwa na hali kama hiyo. Nilipata ushauri kuwa nimpe axline x3 kutwa, panadol na alambe asali mbichi mara kwa mara. Hakika utadhani aliyenishauri hiyo dawa ndiye alikuwa amemroga mwanangu! Ndani ya siku tatu kikohozi kilikoma kabisa na sasa hakohoi tena. Nawe jaribu pia .
 
alianza lini mkuu

maana wangu tangu akiwa mchanga mpaka sasa aisee ana 3yrs kifua chake kikavu
 
Pole dada/kaka . pia wangu alikuwa na hali kama hiyo. Nilipata ushauri kuwa nimpe axline x3 kutwa, panadol na alambe asali mbichi mara kwa mara. Hakika utadhani aliyenishauri hiyo dawa ndiye alikuwa amemroga mwanangu! Ndani ya siku tatu kikohozi kilikoma kabisa na sasa hakohoi tena. Nawe jaribu pia .

asante
 
Wasiliana na specialist moyo asijekuwa na Shida ya kupungua oxygen au infections za moyo.Vipi allergy amechekiwa ?
Pole sana
 
Back
Top Bottom