Wapi nitapata kiwanja cha milioni 3 kwa Dar?

Wakuu habarini za muda huu

Kwa Dar es Sallam ni wapi naweza kupata kiwanja cha milioni 3?

Namaanisha kiwanja cha milioni moja,mbili hadi tatu mwisho iwe tatu maana ndo uwezo wangu

Kwa Dar napendelea maeneo yote isipokua tu maeneo ya kilwa Road

Kwa 3M au 2M au chini yake ni wapi naweza pata kiwanja?Umbali kutoka barabara kuu iwe kutembea hata kwa mguu isizidi dakika 20 au dakika 25

Pia naomba kujuwa kwa milioni 3 si naweza kupata walau kiwanja kikubwa cha size ya kati?Au vya 2M 2.5M au 3M mara nyingi huwa ni ukubwa gani kwa wajuzi wa humu?


Pia naombeni kujua ni taratibu gani za kufuata ili kumiliki kiwanja maana ndugu yenu nikiri kuwa mimi sijui procedure zozote za kumiliki kiwanja naogopa kupigwa sana, kutapeliwa pia naogopa kununua kiwanja chenye mgogoro jee nifate taratibu gani?

Natanguliza shukrani
Karibu Chanika ninavyo vizuri sanaa
No longolongo ni vyangu mwenyewe
 
Tajiri usiforce sana DSM kuna maeneo ya jirani (PWANI) mfano kibaha mlandizi bagamoyo na fukayosi

La muhimu kuliko lote Nunua Kiwanja kilichopimwa na kabla hujanunua hakikisha umeona ramani ya mipango mji ya hilo eneo

Kingine cha kuzingatia ni kununua katika makampuni ya real estate yaliyosajiliwa na yana leseni inayowaruhu kuuza Ardhi

Hati miliki kutoka wizarani ni muhimu sana

Usiogope gharama ... km umedhamiria kununua kiwanja fata procedure zote utakuja kunishukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mkuu!ikiwa kama upo serious nipigie kwa namba hii 0783721337 ninaviwanja vingi tu maeneo ya kitonga kata ya msongola wilayani ilala,kuhusu usafiri upo na wa uhakika na umbali kutoka barabarani sasa hapa inategemea ni vizuri ukafika na ukajionea.

Kuona sio kufanya biashara,unaweza kuona na kama hujaridhika unaweza kuondoka na kwenda kuangalia sehemu zingine....!!

Pia ninakiwanja chanika zingiziwa kipo karibu na shule.
 
Wakuu habarini za muda huu,

Kwa Dar es Saalam ni wapi naweza kupata kiwanja cha milioni 3? Namaanisha kiwanja cha milioni moja, mbili hadi tatu mwisho, iwe tatu maana ndiyo uwezo wangu. Kwa Dar napendelea maeneo yote isipokua tu maeneo ya kilwa Road.

Kwa milioni 2 au 3 au chini yake ni wapi naweza pata kiwanja? Umbali kutoka barabara kuu iwe kutembea hata kwa mguu isizidi dakika 20 au dakika 25.

Pia naomba kujua kwa milioni 3 si naweza kupata walau kiwanja kikubwa cha size ya kati au vya milioni 2, 2.5 au 3 mara nyingi huwa ni ukubwa gani kwa wajuzi wa humu?

Pia naombeni kujua ni taratibu gani za kufuata ili kumiliki kiwanja, maana ndugu yenu nikiri kuwa mimi sijui taratibu zozote za kumiliki kiwanja. Naogopa kupigwa sana, kutapeliwa, pia naogopa kununua kiwanja chenye mgogoro. Je, nifate taratibu gani?

Natanguliza shukrani.
Njoo nkuuzie malamba mawili kwa banana Zoro.... Nnacho 15 kwa 13
 
Habari ndugu!
Katika kuelekea kufungua mwaka 2022 Tunakuletea miradi ya Mashamba yaliyopo Pingo Chalinze kwa Bei nafuu,
Maeneo yote yapo karibu na makazi ya watu,Huduma za maji na Umeme zipo.
🅰️Mradi wa kwanza upo Pingo umbali wa kilomita mbili na nusu kutoka barabara kuu ya Morogoro road,Zinapatikana zaidi ya heka 20 sehemu moja.
BEI: Tsh Milioni moja na nusu kwa heka.
🅱️Mradi wa pili upo Pingo barabarani kabisa jirani na kiwanda Cha Tiles.,Zipo heka 35.
BEI:Tsh Milioni ishirini na mbili kwa heka(maongezi kidogo yapo)
hili eneo linafaa kwa uwekezaji wa kiwanda nk
Kwenda kuona miradi hii Ni jumamosi hii,Kama utakuwa tayari Tuwasiliane WhatsApp +255625234332
 
Nenda nje ya mji huko kibamba vipo vingi tuu.

Au mailimoja, kibaha, kiluvya nk

Maeneo hayo ni sawa na kuwa mjini tuu maana mwendokasi imefika huko.
Kwa hiyo 2mil utapata porini sana. Labd 3 had 4, mwendo wa mguu 1 hour kutok mail moja kibaha unapata vingi tu
 
Njoo mtaa wa muheza Kara ya maili moja halmashauri ya kibaha mji.. Utashukia Kibamba shule arafu una chukuwa boda boda 1500..
 
TUNAUZA VIWANJA KWAAJILI YA MAKAZI
1.KILUVYA MADUKANI--BEI 8M (UKUBWA 20*20)
2.KIGAMBONI AVICK TOWN--BEI 12.4(UKUBWA 30*25)
3.BAGAMOYO FUKAYOSI--BEI 395,000/=(UKUBWA 20*25)
4.VIGWAZA BANDARI KUU--BEI 580,000/= (UKUBWA 20*20)
5.KIBAMBA eneo lipo barabarani--BEI 50M(UKUBWA HEKA 1 NA ROBO)
6.CHALIZE PINGO--BEI 1.5M KWA HEKA.
7.CHALINZE eneo lipo barabarani--BEI 17M KWA HEKA
Mawasiliano WhatsApp +255625234332
 
Mwambie kabisa ni BUYUNI Alafu. Mkubushe ni Km ngapi Toka Fery,pia lami inakaribia Avic kwenda huko ni kama unaenda Mkoani Maana hamna lami.Kama ana mishemishe town mara 1000 aende Kibaha.
Sure ni huko kimbiji ndani ndani sana

50+ km kutoka ferry...Bado n rough road

Ila mji wa kigamboni unakua kwa kasi sana adse

Ila lazima tuseme ukweli kwa sasa ni bora mtu anunue kibaha kuliko kigamboni coz kibaha ni rahisi sana kufikika compare to kigamboni
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom