USHAURI NA MSAADA: Wapi nitapata kiwanja cha milioni 3 kwa Dar?

mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,697
1,525
Wakuu habarini za muda huu

Kwa Dar es Sallam ni wapi naweza kupata kiwanja cha milioni 3?

Namaanisha kiwanja cha milioni moja,mbili hadi tatu mwisho iwe tatu maana ndo uwezo wangu

Kwa Dar napendelea maeneo yote isipokua tu maeneo ya kilwa Road

Kwa 3M au 2M au chini yake ni wapi naweza pata kiwanja?Umbali kutoka barabara kuu iwe kutembea hata kwa mguu isizidi dakika 20 au dakika 25

Pia naomba kujuwa kwa milioni 3 si naweza kupata walau kiwanja kikubwa cha size ya kati?Au vya 2M 2.5M au 3M mara nyingi huwa ni ukubwa gani kwa wajuzi wa humu?


Pia naombeni kujua ni taratibu gani za kufuata ili kumiliki kiwanja maana ndugu yenu nikiri kuwa mimi sijui procedure zozote za kumiliki kiwanja naogopa kupigwa sana, kutapeliwa pia naogopa kununua kiwanja chenye mgogoro jee nifate taratibu gani?

Natanguliza shukrani
Karibu chanika ninavyo vizuri sanaa
No longolongo ni vyangu mwenyewe
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
3,145
4,235
Tajiri usiforce sana DSM kuna maeneo ya jirani (PWANI) mfano kibaha mlandizi bagamoyo na fukayosi

La muhimu kuliko lote Nunua Kiwanja kilichopimwa na kabla hujanunua hakikisha umeona ramani ya mipango mji ya hilo eneo

Kingine cha kuzingatia ni kununua katika makampuni ya real estate yaliyosajiliwa na yana leseni inayowaruhu kuuza Ardhi

Hati miliki kutoka wizarani ni muhimu sana

Usiogope gharama ... km umedhamiria kununua kiwanja fata procedure zote utakuja kunishukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 

chrisbleez

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
646
947
Habari mkuu!ikiwa kama upo serious nipigie kwa namba hii 0783721337 ninaviwanja vingi tu maeneo ya kitonga kata ya msongola wilayani ilala,kuhusu usafiri upo na wa uhakika na umbali kutoka barabarani sasa hapa inategemea ni vizuri ukafika na ukajionea.

Kuona sio kufanya biashara,unaweza kuona na kama hujaridhika unaweza kuondoka na kwenda kuangalia sehemu zingine....!!

Pia ninakiwanja chanika zingiziwa kipo karibu na shule.
 

Fkm2020

Member
May 19, 2020
70
50
Wakuu habarini za muda huu,

Kwa Dar es Saalam ni wapi naweza kupata kiwanja cha milioni 3? Namaanisha kiwanja cha milioni moja, mbili hadi tatu mwisho, iwe tatu maana ndiyo uwezo wangu. Kwa Dar napendelea maeneo yote isipokua tu maeneo ya kilwa Road.

Kwa milioni 2 au 3 au chini yake ni wapi naweza pata kiwanja? Umbali kutoka barabara kuu iwe kutembea hata kwa mguu isizidi dakika 20 au dakika 25.

Pia naomba kujua kwa milioni 3 si naweza kupata walau kiwanja kikubwa cha size ya kati au vya milioni 2, 2.5 au 3 mara nyingi huwa ni ukubwa gani kwa wajuzi wa humu?

Pia naombeni kujua ni taratibu gani za kufuata ili kumiliki kiwanja, maana ndugu yenu nikiri kuwa mimi sijui taratibu zozote za kumiliki kiwanja. Naogopa kupigwa sana, kutapeliwa, pia naogopa kununua kiwanja chenye mgogoro. Je, nifate taratibu gani?

Natanguliza shukrani.
Njoo nkuuzie malamba mawili kwa banana Zoro.... Nnacho 15 kwa 13
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom