Ushauri na mchanganuo kuhusu biashara ya duka la rejareja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri na mchanganuo kuhusu biashara ya duka la rejareja

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kebi, Feb 13, 2012.

 1. k

  kebi Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kufahamishwa kwa mwenye kujua duka la rejareja la kuuza mchele, juice na kadhalika linaweza kuitaji mtaji kiasi gani

  Ibravo post:
  Habari zenu Wana Jamii Forum,

  Mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa tatu,katika harakati za kujiandaa na kupambana na maisha pindi nitakapohitimu elimu yangu na kurudi mtaani,nimetafuta pesa ikiwa kama mtaji wa biashara milioni moja (1,000,000)hasa ya duka la bidhaa za vyakula.

  Tatizo ni kwamba si mzoefu ktk biashara na ni mara ya kwanza kutaka kuifanya hii biashara kwan matarajio yangu ni kujiajiri mwenyewe.

  Naomba ushauri kwa yeyote mwenye uelewa kuhusu hili kunipa mchanganuo wa bidhaa muhimu zinazotakiwa kuwepo dukani kama vile unga kiasi gani,mchele n.k kulingana na mtaji huo wa Milioni Moja.

  Natanguliza Shukrani zangu.


  ================================================
  MAJIBU KUHUSU BIASHARA HII
  ================================================

   
 2. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  inategemea na unataka kuweka vitu kiasi gani!ila kwa kuanzia milion 2 au 3 inatosha kabisa.
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Mkuu majibu mengine ni simple sana, Fanya hivi

  Chukua kalamu na Note book then neda kariakaoo na kwingineko tembelea maduka ya jumla chukua bei theni ukukaa chini ukipiga mahesabu utapata kila kitu,

  Mkuu ili ufanikiwe katika biashara unatakiwa kuumiza kichwa sana, inatakiwa akili ifanye kazi mara 6 zaidi ya uwezo wake wa kawaida, fanya tafiti mwenyewe mkuu
   
 4. N

  Njele JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukifanya business plan yako itakupa jibu sahihi kuliko kupoteza muda kwamba hapa tutakupa jibu sahihi kesho utakapoenda kutumia majibu ya hapa ukaona kama umedanganywa.
   
 5. u

  ureni JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mie nilimfungulia mama yangu kijijini kwenye frem ya ukubwa wa 3*3 mwanzo wa last year ilinicost jumla ya 3m,I mean niliweka kila kitu kinachostahili katika duka la rejareja.Nafikiri hiyo taarifa inaweza kukusaidia.
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu mtaji alioanza nao Kimario sio lazima na masawe aanze nao huo huo. Halafu mahitaji na gharama yanabadilika kulingana na eneo ulilopo. Kwa mfano kama upo sehemu haina umeme unaweza ukaambulia ushauri uliojumuisha mpaka fridge ya umeme wakati kwako si mufaka.

  Kama ungetaka ushauri halisi basi ungeweka data zote hadharani ili ushauriwe lakini kulingana na maelezo yako mimi ninakushauri uanze na hicho kiasi ulichonacho (kama unaeneo la kufanyia biashara), hivyo vitu vingine utaongeza taratibu baada ya kupata faida au fedha za ziada.
   
 7. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sasa Parachichi, hapa ndipo tunapokosea halafu tunalalamika kwamba biashara ni mbaya. Wewe hupasi kuwa na vitu vyako unavyotaka kuweka dukani. Wewe unapaswa kuwa msilikilizaji tu, na unalisikiliza soko linakwambia nini.
   
 8. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwani wewe ulikuwa na mtaji wa sh ngapi labda tuangalie ni vitu gani vya muhimu vya kuanzia hiyo biashara yako
   
 9. m

  madigida Member

  #9
  Nov 15, 2013
  Joined: Jan 30, 2013
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Salaam zenu wote! Naomba ushauri wenu kwa mwenye uzoefu wa aina hii ya biashara, je ni mtaji kiasi gani unafaa kuanzia, na faida iko je na jinsi ya kutunza kumbukumbu. Siku hizi ajira ndio hiziii!!!!
  Karibuni kwa ushauri
   
 10. J

  JtheTATA JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2013
  Joined: Jun 14, 2013
  Messages: 334
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  ten millions tshs: inatosha kuanzia. faida kiwango ni 10% ya mauzo ya siku
   
 11. Ibravo

  Ibravo JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2014
  Joined: Jan 15, 2014
  Messages: 525
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Habari zenu Wana Jamii Forum,

  Mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa tatu,katika harakati za kujiandaa na kupambana na maisha pindi nitakapohitimu elimu yangu na kurudi mtaani,nimetafuta pesa ikiwa kama mtaji wa biashara milioni moja (1,000,000)hasa ya duka la bidhaa za vyakula.

  Tatizo ni kwamba si mzoefu ktk biashara na ni mara ya kwanza kutaka kuifanya hii biashara kwan matarajio yangu ni kujiajiri mwenyewe.

  Naomba ushauri kwa yeyote mwenye uelewa kuhusu hili kunipa mchanganuo wa bidhaa muhimu zinazotakiwa kuwepo dukani kama vile unga kiasi gani,mchele n.k kulingana na mtaji huo wa Milioni Moja.

  Natanguliza Shukrani zangu.
   
 12. Pelham 1

  Pelham 1 JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2014
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 521
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hongera sana Mkuu karibu ktk ulimwengu wa fikira tofauti kwa wajasiriamali! vizuri ukifanya mwenyewe research kwa wafanya biashara na wenye maduka mbali mbali! ama kama upo tait nipe tenda hiyo Kampuni yangu inadeal na masoko inaweza kukufanyia kwa bei nafuu kabisa! my kampani ni Tangaza Marketing Solutions(TMs)
  karibu sana.
   
 13. Ibravo

  Ibravo JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2014
  Joined: Jan 15, 2014
  Messages: 525
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Shukran mkuu,ngoja nijaribu kufanya research mwenyewe maana pesa ya kutoa tenda kwa utafiti itamaliza capital yenyewe.
   
 14. Miaghay

  Miaghay JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2014
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  coomon man anaweza kuwa na bei nzuri,mfano kuna kampuni moja pale kenya wanakufanyia market research kwahizi biashara ndogondogo kwa gharama haifiki hata elfukumi ya kibongo.wanakupa full infor kuhusu biashara husika,mfano capital ya kuanza nayo,process ya kuanzisha,location inayofaa,rent ya flame,maunjanja katika biashara husika etc.
   
 15. KIDOLEGUMBA

  KIDOLEGUMBA JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2014
  Joined: Apr 17, 2013
  Messages: 503
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  business ndani ya business!!
   
 16. chaUkucha

  chaUkucha JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2014
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 3,223
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  kwa mtaji wa m 1 rent ya flame itamuumiza labda kile cha mbao (movable) pia akikinunua ni poa zaidi.
   
 17. Click Hapa

  Click Hapa JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2014
  Joined: Jan 27, 2013
  Messages: 483
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu Ibravo,
  Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:

  Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.
  Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.
  Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia??? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.
  Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.
  Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana;
  Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.
  Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.
  Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh. 1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
  Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
  Kwa leo mkuu.
   
 18. Kinyengeli

  Kinyengeli JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2014
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Acha tamaa wewe ,kijana ana kimillioni moja tu na wewe unataka upatemo acha upuuzi na roho mbaya, yaani tangu muambiwe mzitumie fursa basi imekuwa nongwa kila fursa mnayo ebo!! Kuwa nahuruma japo kidogo roho mbaya haijengi,.
   
 19. CEOgwamzy

  CEOgwamzy Senior Member

  #19
  Jul 19, 2014
  Joined: Jun 14, 2014
  Messages: 142
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  hii ipo poa sana.
  Na ulilosema brother ni kwel lazma msomi ujasilimali wako uwe wa kisomi na sio bora tu kisa ujasilia mali basi uufanye hata hovyo hovyo
   
 20. Zanzibar Spices

  Zanzibar Spices JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2014
  Joined: Jul 14, 2013
  Messages: 7,543
  Likes Received: 2,021
  Trophy Points: 280
  Hii ni kweli,hembu nipe jina au contact yahiyo Kampuni ya kenya,maana lazima tugawane majukum
   
Loading...