Ushauri na maoni yangu kuhusu Bandari ya Bagamoyo

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
USHAURI NA MAONI YANGU KUHUSU BANDARI YA BAGAMOYO.

Ilikuwa Octoba 21 katika taarifa ya habari ya Channel Ten nilimsikia Mgombea Urais wa Ukawa,Mh Edward Ngoyai Lowassa akisema kwamba Serikali yake itaangalia jinsi ya kuuvunja mkataba wa bandari ya Wachina Bagamoyo, Alisema haoni mantiki ya kutumia mabilioni kujenga bandari moja Bagamoyo wakati bandari za Tanga na Mtwara ziko ovyo,kama kawaida pengine kisiasa tungesema anatafuta kura za Wananchi wa Tanga.

Lakini Rais aliyeshinda Uchaguzi huo wa 2015 Hayati Rais John Pombe Magufuli alikuja kuuvunja kweli mkataba huo wa Bandari ya Bagamoyo,Kwa msio fahamu kuna umbali wa kilomita 1200 kutoka Tanga mpaka Kampala (Uganda) ukilinganisha na kilomita 1500 kutoka Mombasa (Kenya) mpaka Kampala,Lakini Waganda wanatumia bandari ya Mombasa sana kwa sababu Tanga hamna kitu,Sasa tuanzie hapa.

Nafikiri tatizo sio eneo la kujenga hiyo bandari ya Bagamoyo kwani hata bagamoyo sio shida na bado faida itapatikana tu,tatizo hiyo bandari tunaijengaje?? Kwa gharama zipi na wapi zinatoka hizo fedha za kujenga bandari hiyo? Tumeona makosa ya Angola na Wakenya ambapo ujenzi unafanywa na mikopo kutoka China na namna ya kulipa ni mateso makubwa,je kwetu ikoje? tuna akili za Waindonesia? Kwa maana ya technology transfer? au ndio utopolo!! Ebu tuangalie faida za Bandari ya Bagamoyo.

1. Wachina wataitumia kama central hub ya
mizigo yao yote kwa Kenya,Uganda,Malawi,
Zambia,Sudani,Tanzania nk maana ikumbukwe wachina wanabiashara nyingi sana ukanda huu.

2. Mkoa wa pwani utanyanyuka kiuchumi.

3. Msongamano dar utapungua kama si kwisha.

4. Wachina wanaweza kutujengea railway line bure kufika sehemu mbalimbali kwenye border ili biashara zao ziende haraka na
wapate faida ya haraka na kubwa.

5. Wanawake wengi wapwani watachanganya damu kwa kutuzalia watoto wa kichina wengi maana hawa jamaa watakaa sana hivyo basi angalau tutakuwa tumeleta akili mpya kwenye hiki kizazi.

6. Ajira nyingi zitatengenezwa hapa.

7. Bado makusanyo ya kodi yataongezeka maana kwa namna moja nyingine hii bandari itakuja na investment nyinginezo nje ya bandari yenyewe..

8. Tunaweza kuwabana 60% wafanyakazi wawe wazawa na kiwango cha mishahara kiwe kizuri.

9. Tunaweza kupata bajeti ya kukarabati bandari ya tanga pia na tukawashawishi wakizidiwa tanga port ikawa backup yao...

-Wazo la kwanza

Uganda wanatumia Bandari ya Mombasa kwa sababu za Kihistoria, Wazungu walijenga Reli ya kutoka Mombasa mpaka Uganda kupitia Industrial area ya Uganda, Jinja mpaka Ziwa Victoria na ndio maana inaitwa Uganda Railway hivyo kuwafanya Waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa na kutumia ya kwetu siyo rahisi na kujenga Bandari ya Tanga tu peke yake haitoshi ni lazima pia tujenge Reli mpya ya kuunganisha Tanga na Uganda mpaka Jinja sasa hiyo siyo kazi rahisi kwani hai make economic sense yaani kutumia mabilioni ya Dola za Kimarekani kwa ajili tu ya soko la Uganda? usisahau pia kujenga Bandari mpya Ziwa Victoria n.k sasa uwekezaji wote huu kwa mizigo gani ya gani Uganda inayo import na kuexport?Import Volume ya Uganda ni kiasi gani mpaka iweze kutufanya kufanya uwekezaji mkubwa kiasi hicho?

-Wazo la pili

Tatizo lipo hivi bandari ya Dar inatumika hadi kwa mizigo ya kaskazin yaani ni kama bandari ya Tanga imekufa,vivyo hivyo na ya mtwara kwa kusini wanatumia bandari ya Dar,Sasa matokeo yake tunagawana watumiaji wa kaskazin mwa Tanzania Mombasa na dar kitu ambacho ni kosa,kumbuka kaskazini kuna uwekezaji mikubwa tuu na kuna miji mikubwa na ukiwa Arusha bandari ya Mombasa ni karibu kuliko Dar na Bagamoyo,Sasa kwanini tusiendelee kuboresha Tanga kwa ajili ya kaskazini mwa Tanzania na Mtwara kusini mwa Tanzania? maana faida ni nyingi kuliko hasara,faida ya kwanza ni umbali mfupi pili gharama ya ujenz mpya wa bandari unakuwa hamna.

Watanzania tufahamu kuwa kuna utafiti uliofanyika na wataalamu kutoka Japan na ambao ulikwishawakilishwa kwenye wizara ulionyesha kuwa Bagamoyo hapafai kujenga bandari,Sababu kubwa ni kuwa Bagamoyo ni shallow waters (kina kidogo sana). Ili kujenga bandari ni lazima ichimbwe sana kuongeza kina,sijui kama walikuwa sahihi,kwa bahati mbaya sana huwezi kuchimba kirahisi sababu Bahari ya Bagamoyo ina mwamba mgumu sana unaonekana hata kwa macho tu,hivyo gharama ya kuvunja mwamba ili kuongeza kina ni kubwa mno,ni sawa na kujenga Bandari mbili.

Wajapani walipendekeza kupanuliwa kwa bandari ya Tanga ambayo Mungu alikwishaijenga ikiwa na kina kirefu,huhitaji kuchimba,Isitoshe, Hayati mwalimu Nyerere alishajenga reli kuunganisha Bandari hii na mtandao wa reli nchini,Kwanini tujenge Bagamoyo? Hii tabia ya kujipendelea nyumbani kwa gharama kubwa ya taifa haikubaliki kamwe.Watanzania tukatae upuuzi huu.Lowassa upo sahihi sana kufikiria kuvunja mkataba huu wa kipuuzi.Waambie wachina wakapanue bandari za Tanga na Mtwara.

-Wazo la tatu

Bandari ya Mtwara ni uti wa mgongo kwa mikoa ya kusini,Uchumi ungekuwa mara dufu katika biashara za kimikoa na nchi jirani kama Zambia na malawi na zingine,Tungepunguza kwa asilimia kubwa population ya wahamiaji walio kimbilia Dar,kwa Tanga vile vile bandari hizo zingesaidia katika kusafirisha bidhaa za biashara kwa wakazi wa mikoa ya kaskazini na nchi jirani na kuondoa matabaka katika ukuaji wa uchumi kimikoa,Hii ya kujenga Bandari kubwa Bagamoyo imekaa kinafiki nafiki na kiushabiki wa kwamba mimi nimewafanya nini wakaazi wangu,hatutaki vijana na ndugu zetu waendelee kujazana Dar es salaam na Bagamoyo.

Kama professionalism ingekua inaheshimiwa, huwez kuiacha project ya Mtwara Corridor halafu kipaumbele kikawa ni kuanzisha bandari mpya wakati ile ya corridor la kusini ambako traffic congestion pale bandarin na hata barabaran ni ndogo na hivyo ni rahisi kusafirisha bidhaa. Bagamoyo bado ni shida kwani iko jiran na Dar es Salaam na hivyo baada ya miaka 10,shida ya msongamano wa magari itajitokeza kwa haraka. Political Will ndiyo mpango mzima!

-Ushauri Vs Maoni

1. Hapa tunaongelea Bandari ambayo inasafirisha Mizigo in bulk ya Uganda, kuwafanya Waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa badala yake watumie yetu ni kama haiwezekani kwa maana hatuwezi kufanya huwo uwekezaji, elewa viwanda vikubwa Uganda viko Mji wa Jinja na hapo katikati ambapo ndipo Uganda Railway ilikopita ikitokea Mombasa na inakwenda mpaka Ziwa Viktoria ambako pia kuna Bandari inayoshusha mizigo na kusafirishwa kwa meli, sasa ili kuwafanya watumie Bandari yetu nilazima tufanye uwekezaji wote huwo, sasa kwa mizigo ipi ya maana ya ambayo Uganda wanayo?

2. It makes alot of sense kudevelop Northern Corridor ya Tanzania (reli na barabara kutoka Tanga mpaka kanda ya ziwa kupitia Moshi-Arusha).Uganda wamegundua mafuta na wanataka kuyaexport kupitia bandari ya Tanga, hivyo bomba pia litajengwa.Tufanye research kidogo,Uganda ni nchi inayoimport goods worth over $4 billion per year, na kuexport $3.2 billion,Je hizo ni ndogo ?Je hiyo corridor itakuwa inatumiwa na Uganda pekee?

3. Tanzania hatuna fedha ya kuwekeza kwenye Ujenzi wa Reli mpya ya kutoka Tanga mpaka Uganda pamoja na Bandari ili kukidhi soko la Uganda, hayo maneno yote unayosikia ya Bandari ya Bagamoyo hizo siyo fedha zetu ni fedha za kutoka Uchina na mtoa fedha ndiyo anaamua ni wapi aweke fedha yake sasa kama wamechagua Bagamoyo wana sababu ingawaje sizijui sababu zenyewe!

Kama ukiniuliza mimi Tanzania kwa sasa hatuhitaji reli mpya ya kutoka Tanga kwenda Uganda bali tunahitaji kwanza kuzijenga upya Reli zetu tulizonazo Kama ambavyo Rais John Magufuli alizifufua ili zifanye kazi kwa full capacity kama Reli ya kati iende sambamba na kufufua Bandari ya Kigoma ambayo ilikuwa inashusha mizigo kutoka kwenye treni na kuipakia kwenye Meli kwenda Zambia,Kongo na Burundi, kufufua na kuijenga upya reli ya kutoka Dar kupitia Ruvu na nyingine kutokaTanga mpaka Arusha, hivyo tunapaswa kuanzia hapo kwanza kabla ya kufikiria kujenga Reli ambayo haipo kabisa sijui mpka Uganda!

4. Wakati Wachina wanaitumia bandari bure na kukomba maliasili,sisi tutakuwa bize tunalipa riba za madeni waliotukopesha kwa benki zao...mikataba mingine bana!wana himiza mradi wa bandari ambayo hata hatuihitaji kwa sababu wanataka kucontrol bandari kwa kusafirisha bidhaa zao na wanataka kutuweka kwenye madeni na nchi zao ili wachukue riba zetu vizazi na vizazi vijavyo! yale yale wanayofanya World bank.

Mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi,Edward Lowasa alisema tutaanza kujitegemea wenyewe bila kutegemea misaada a.k.a mikopo kutoka nchi za nje, huo ni mkakati mzuri sana,tujiunge na nchi nyingine za africa mashariki na Africa kwa ujumla kuendeleza uchumi wetu, tusaini mikataba ya gesi na madini yenye faida kwa nchi, tushughulikie wakwepa kodi kubwa kubwa, tuondoe misamaha ya kodi asiyekubali aondoke....tutafika tu, sio haya magumashi ya kuuza kila kitu na kugawa maliasili kama karanga halafu kwenda kuomba omba misaada na mikopo kwa hao hao tunaowapa maliasili zetu kwa bei za bure,Niseme wazi haya mawazo ya Edward Lowassa yalichukukiwa kama yalivyo na kufanyiwa kazi na Rais John Pombe Magufuli.

-Wasiwasi

Kwa uelewa wangu bandari ya Bagamoyo inajengwa kwa fedha za Wachina,wataimiliki bandari hiyo mpaka watakaporudisha fedha zao ndiyo itakuwa mali yetu,mimi tatizo langu na bandari ya Bagamoyo ni uwezekano wa bandari hiyo kuiua bandari ya Dsm. vilevile inaonekana hatujajipanga kuhakikisha tunafaidika na uwekezaji huo ambao ni mkubwa kufanyika hapa Tanzania,ningependa mamlaka yetu ya bandari iwe na significant amount of shares katika mradi wa Bagamoyo ili tuweze kufaidika na mapato yanayotokana na bandari hiyo. pia kuna eneo la huduma kwa bandari hiyo mfano upakiaji na upakuaji ambayo inaweza kufanywa na mamlaka yetu ya bandari.

Sekta ya usafirishaji itakuwa kwa kiasi kikubwa ikiwa mradi wa Bagamoyo port utakamilika. vilevile ukumbuke kwamba Oman Fund wanawekeza ktk eneo la viwanda linalounganishwa na bandari hiyo,sasa hapo napo tujipange na siyo kuanza kuupinga mradi huu,kwa bandari ya Tanga, labda tungekuwa wabunifu kidogo kwa kuifanya iwe kituo kikuu cha kuteremsha Mafuta nchini. vilevile Tanzania ipiganie bomba la Mafuta toka Uganda liishie katika bandari ya Tanga,kuhusu bandari ya Mtwara; eneo la kusini, pamoja na nyanda za juu kusini kuna miradi ya gesi, chuma, na makaa ya mawe, hivyo bandari hiyo inapaswa kuwa mahsusi kwa usafirishaji wa madini hayo, pamoja na bidhaa zitokanazo.

Sisi raia wa kawaida ambao hatujui huo mkataba inabidi mtufafanulie sintofahamu zilizokuwepo hadi kuwekwa kapuni na sasa kutolewa kapuni. Mkituelewesha cc hatuna shida hasa mambo haya: 1. Mkataba original ulisainiwa lini na nani (pre-signoff)? Je, ulifanyika uhakiki na kujiridhisha (Feasibility study/due diligence)? Tume ya watu wangapi ilihusika? Ulipaswa kuanza lini na kwa nini uliwekwa kapuni, zilikuwa sababu za kisiasa au uzalendo? 2. Mkataba ni wa miaka mingapi? Gharama ya mradi wote ni sh ngapi? 3. Pay back (Return on Investiment- (ROI) ni miaka mingapi? 4. Risk assessment.

Je, ni kweli bandari nyingine (Dar, Mtwara, Tanga nk) inabidi zisiendelezwe? Nini faida na madhara (Pro and Cons)? Je, hakuna mwingiliano na objectives za SGR na bandari ya Dar? 5. Je, ni kweli kwamba mapato yote ya bandari yatasimawia na mchina (no revenue visibility)? 6. Je kuna project kama hii ilishanyika na Mchina hapa Africa ikawa na matokeo chanya au hii ya Tz ndo ya kwanza? 7. Na hoja nyingine kutoka kwa wadau wengine kama zipo. Nafikiri iundwe tume kama ilivyokuwa tume ya KATIBA, ikiwa na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo na vyama vya upinzani wafanye uchambuzi kisha waje na majibu.

Nimalizie kwa kusema hata kama una shida kiasi gani usikubali mtu anaye taka kukupa msaada wa kukujengea nyumba kuleta masharti ya kulala na mkeo akiweka sharti dogo la kutofungua mlango akiwa chumbani na mkeo.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Jiwe alitia nuksi kwenye mradi huu. Lkn ni wazo jema sana kujenga bandari ya Bagamoyo.
 
Awamu ya Saba ikija iuvunje mkataba utakaoingiwa na awamu hii Kwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.
 
Mimi nakubali andiko lako yaani Ndugai,Kikwete na Samia watuambie huo mkataba unakitugani naona akina MANGUNGO wanahaha
Miradi ya ccm sio ya kukimbilia kuna mradi wa kunguru tuliambiwa kwamba watakuwa wanakusanya taka nakusafisha mitaa tangu waletwe sijawaona kunguru wana kula taka wala kusafisha mitaa zaidi ya wizi hadi wanabebea simu
 
Maslahi ya nchi yakisimamiwa vema na tukaweka uzalendo mbele bila kutanguliza maalahi binafsi basi mradi utatufaa lakini tukitenda kinyume (sio cha maumbile) TUMEKWISHA...!!!
 
Maslahi ya nchi yakisimamiwa vema na tukaweka uzalendo mbele bila kutanguliza maalahi binafsi basi mradi utatufaa lakini tukitenda kinyume (sio cha maumbile) TUMEKWISHA...!!!
Yule aliyepita hakuwa hata na sabb ya kuzuia huo mradi, kwasabb 2. Moja, Chato hakuna bahari kwahiyo hata sabb za ubinafsi hazikuwepo. Mbili, fedha za mradi haitoi serikali ya Tanzania, kwahiyo hata sabb za kwamba alikuwa anaokoa fedha za walipa kodi hazikuwepo.

Nini kilimfanya azuie? Alitaka kumchafua JK ili yeye avune sifa. Alitawaliwa na roho ya kutu, ya kinyama, ya wivu, ya kupenda sifa, ya kuuwa. Alikuwa na roho mbaya tu.

Akadai eti mradi huu ni hasara kwa taifa. Zile hifadhi za Burigi, international airport ya Chato, sports arena ya Chato, n.k vina tija gani kwa taifa?

"Ukiwa na roho mbaya unakufa mapema" by Sexless
 
Yule aliyepita hakuwa hata na sabb ya kuzuia huo mradi, kwasabb 2. Moja, Chato hakuna bahari kwahiyo hata sabb za ubinafsi hazikuwepo. Mbili, fedha za mradi haitoi serikali ya Tanzania, kwahiyo hata sabb za kwamba alikuwa anaokoa fedha za walipa kodi hazikuwepo...
Nini kilimfanya azuie? Alitaka kumchafua JK ili yeye avune sifa. Alitawaliwa na roho ya kutu, ya kinyama, ya wivu, ya kupenda sifa, ya kuuwa. Alikuwa na roho mbaya tu.
 
Nini kilimfanya azuie? Alitaka kumchafua JK ili yeye avune sifa. Alitawaliwa na roho ya kutu, ya kinyama, ya wivu, ya kupenda sifa, ya kuuwa. Alikuwa na roho mbaya tu.
Mzee mwenzangu Jiwe alikuwa na roho ya ajabu sana naomba Mungu asitokee mmoja Wa wanae akabeba hiyo roho,nawaombea wanae wabebe roho ya upendo ya Mana Janeth.

Mzee mwenzangu kumbe na we we in nocturnal kama Mimi....
 
Mzee mwenzangu Jiwe alikuwa na roho ya ajabu sana naomba Mungu asitokee mmoja Wa wanae akabeba hiyo roho,nawaombea wanae wabebe roho ya upendo ya Mana Janeth.

Mzee mwenzangu kumbe na we we in nocturnal kama Mimi....
Hakuwa Mtz kwa asili...!!!!
 
Back
Top Bottom