Ushauri mzuri wa kujenga kwa wana jamii forum wote kuhusu mh. Zitto na viongozi wengine wengine

Status
Not open for further replies.

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Nimekuwa nikifuatilia mijadala tele humu jamvini kuhusu viongozi wa chadema na kwa kifupi mijadala mingi imekuwa ikimuhusu mh.Zitto na viongozi wa juu wa cdm haswa mh.Mbowe na Dr.Slaa.Mingi ya mijadala inayomuhusu mh.Zitto imekuwa very negative(yaani haijengi chama)na imekuwa ikionyesha trend ambayo kwa mtu makini anayefuatilia siasa za upinzani tz inaweza kumfanya aone kuwa ahaaa! kumbe tz hamna upinzani wa kweli.Nasema hivi kwa kuwa mijadala hii, ambayo mingi(nahisi)inatoka kwa wana chadema,hainyoshi kukiimarisha chama bali kukivunja kwani kumekuwa na mitazamo ya udini,ukabila,ukanda(i mean who is from where!)n.k.

Pia mijadala hii mingi imekuwa ya kuendeleza maswala ya fitna na chuki tena baina ya viongozi wa chadema.Jamani tuulizane,leo hii hawa ccm wanatapatapa kwa kuwa tayari kuna mipasuko mikubwa ndani ya chama iliyosababishwa na hayo hayo niliyotaja hapo juu,tena wanashindwa kupata njia mbadala ya kujisafisha,hivi iweje wana chadema nao muanze kufata trend hii ya kuharibu chama ambacho tayari kimeonyesha kupendwa na wananchi?


Mbona hatujifunzi toka tulikotoka kuwa hapajawahi kuwa na upinzani wa kweli kwa kuwa vyama vingi vimekuwa na mipasuko ya ndani kwa ndani? Leo hii ningetegemea hata kama mwana cdm ameona mh.Zitto kuna mambo anafanya hayakubaliki(sijui yapi?),vipi tena muanze kumuingiza kwenye misuguano na viongozi wake?,kama sikosei mh.Zitto ni mmoja wa kiongozi wa chadema,sasa kama mnasemana heshima kwa viongozi wenu inatoka wapi?alafu hili swala halileti picha nzuri hata kidogo nje ya chama,mnawapa mwanya vyama vingine wajipange kuiangusha chadema.


Mi nilitegemea mwana chadema asimame imara kukilinda chama na viongozi wake kwa kupambana na hoja za wapinzani kama ccm, na vyama vingine vidogo visivyo na tija wala si kuleta au kujanga hoja za fitna,udini,ukanda,ukabila n.m ambazo mwisho wa siku zitakidhoofisha chama. Nategemea malalamiko kwa viongozi wa chama yatatatuliwa na vikao vya chama na hilo nadhani viongozi wote wa chadema wanalifahamu.


Kama wote tujuavyo viongozi wanaweza kuwa na mapungufu kama walivo binadamu wengine na haya yanazungumzwa vikaoni.

Inashangaza kuona pale ambapo chama cha chadema kimekubalika na jamii alafu eti wanachama wanawalalamikia baadhi ya viongozi wakati chama hata bado hakijachukua dola,kwa mtindo huu itakuwa kuwapa ccm dola kila uchaguzi


Pia kwa viongozi wa chadema,nategemea yanapotokea malalamiko nyie mnayasikia,basi ni vizuri haya mambo mkawa mnayaweka wazi kwa wanachama wenu ili kuweka wazi dhana ya uwazi ambayo mnaifagilia. Na pale ambapo kiongozi analalamikiwa basi ajirekebishe kwa kuondoa mapungufu kwani mi bado naamini chadema ni chama makini sana kwa kuwa na viongozi makini wanaoweza kuleta mabadiliko ya kweli kwa nchi hii(na mh.Zitto akiwemo).


Safari ndo kwanza imeanza si vema kutumiana maneno,hii si nzuri kwani nakumbuka mh.Zitto alivyokuwa anapambana bungeni na kina mh.Mdee na Slaa peke yao na wakawa wanasikilizwa kwa uchache wao mkubwa.Kumbukeni Zitto alifukuzwa bungeni kwa ajili ya kutetea hoja za maslahi ya nchi!!sasa leo inakuwaje anakuwa mjadala humu jamvini?


Kuna dhana imo kwa jamii kwamba mtu anapobadili mtindo wa maisha kwa kuwa labda na mali ua vile basi huonekana kama ameasi. Yawezekana Zitto kabadili mtindo wa maisha kwa namna moja au nyingine basi achukuliwe hivyo kwani yeye is still one of the party leaders. Haya mambo ya kusema chama sijui cha wachaga yanatoka wapi?inasikitisha sana kuona wana cdm wanajadili mambo kwa mitizamo hii.


Nategemea viongozi wote wa chadema na wanachama wao watakuwa mstari wa mbele kupambana na hizi hoja hasi kutoka vyama vingine vyote vya upinzani(ambao wanaongea hovyo sana kuhusu chadema)na pia ccm ambao watatumia malumbano hasi dhidi ya chadema kujijenga kama ambavyo wamekuwa wanatumia hoja na sera za chadema(hata kama wamezipinga hadharani)kujisafisha kwa umma.


Nategemea kuwaona wabunge wa chadema wakiwa kitu kimoja popote pale haswa bungeni kutetea maslahi ya nchi hii ambayo imeshauzwa kwa wageni.Sitegemei kuwaona wabunge wa chadema wakipingana kwa hoja kama wanavyofanya ccm. Nategemea wabunge na viongozi wa chadema huwa wanakutana na kujadili wapi wamekosea na kurekebishana kama timu moja inapokuwa inakaa kutafuta ushindi na si kulumbana au kutupiana lawama ambazomwishi wa siku zinabomoa badala ya kukijenga chama.


Mwisho,dola haiwezi kuchukliwa kwa lelemama ndugu zangu bali kwa sera,hoja,mshikamano na uongozi imara utakao wavuta watanzania wote kuamka siku ya uchaguzi na kusema sasa enough is enough ngoja tuwape hawa chadema dola kwani tumechoka kutaabika na dhiki wakati tuko kwenye nchi yenye kila neema ya raslimali na utajiri.


Angalizo:

Haya ni maoni yangu binafsi na sijawa inflenced na mtu yoyote kusema haya.Mimi ni kati ya watanzania tunaoishi kwa jasho letu huku tukiangalia nchi hii inavyoporwa na walaghai.Naomba kuwasilisha............
 
nderingosha

Ingawa hii nyuzi yako ni ya zamani lakini leo imepata majibu kutoka chadema. Zitto hakubaliki kwa kuwa hataki posho na viongozi wengine wa chadema wanataka posho.

Hapo sasa!
 
Hivi hili ni jukwaa gani? Zitto ni mwenzetu sina tatizo naye.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom