Ushauri: Mwanaume anataka kuishi na mimi lakini wazazi wasijue

maimatha

Senior Member
Mar 2, 2013
129
161
Naombeni mawazo yenu na ushauri pia,

Nilikuwa na mchumba na mahali alitoa ilibaki ndoa tu nikapata mimba kabla ya ndoa jamaa akasema mpaka nijifungue ndio tufunge ndoa kumbe alikuwa kampa binti mimba na alikuwa anampenda kuliko mimi, jamaa alinitesa sana kihisia.

Nyumbani nikafukuzwa nikaenda kwa jamaa alinifanyia visa pamoja na kuongea na wanawake usiku kucha tumelala pamoja, nikashindwa nikarudi nyumbani nilijifungua nikamwambia hata hongera hamna.

Baadae akaanza kutuma hela ya matumizi kama kawaida mtoto anamiaka karibia tu, yule mwanamke kaolewa na mwanaume mwingine mwezi uliopiata,
Juzi kaja ooooh! Nimsamehe bado ananipenda na bla bla! Kibao eti tuishi pamoja lakini wazazi wake wasijue na bila ndoa.

Jamani huyu kaka mzima kweli, binafsi nilikua natamani sana mzazi mwenzangu arudi tuishi pamoja lakini sio kwa staili hii, kweli anania kwanini hataki wazazi wajue?Naombeni ushauri wenu wapendwa.
 
ngoja nipost ya mwisho kabla haijazimwa.. ulivyomuuliza kwanini wazazi wasijue akasemaje?
 
Kuwa mwangalifu sana na huyo jamaa. Hata kama ni mzazi mwenzio. Dizaini ameamua kukufanya wewe ni kipozeo chake tu.

Usipokuwa makini atakudunga mimba ya pili na kukuacha ukiwa umetoa macho kama umebanwa na mlango. Kama kweli ana dhamira ya dhati kwako kwanini anakuja na hoja ya aina hiyo? Anataka kuficha kitu gani? Do your homework vizuri bidada least utajuta tena baadae
 
msemo wa uswahilini "Kazi Ya Moyo Ni Kusukuma Damu Kupenda Ni Kilanga" yani hapo ulipo we mwenyewe jibu unalo la nini cha kufanya juu ya huyo mwanaume, sasa kinachokushinda usifanye maamuzi ni nini? kupenda gani huko kwa upuuzi-upuuzi, yani mi nashindwaga kuelewa mnalishwaga vitu gani na wenzi wenu hadi mnakuwa watumwa hivyo hata kwenye kufanya maamuzi binafsi ya kukusaidia wewe? ebu acha ujinga, MTEME!
 
  • Thanks
Reactions: irk
Mabinti mnahitaji kufanya toba sana ili musiangamie na upofu wa madhila ya vijana wahuni. Pole sana binti Mimi sina cha kukushauri zaidi ya haya nilokwambia.
 
naomben mawazo yenu na ushauri pia...
nilikua na. mhumba na mahari alitoa ilibaki ndoa 2....
nikapata mimba kabla ya ndoa jamaa akasema mpaka nijifungue ndio tufunge ndoa.....
kumbe alikua kampa Bint mimba na alikua anampenda kuliko Mimi....jamaa alinitesa sana kihisia...Nyumban nikafukuzwa nikaenda kwa jamaa alinifanyia visa pamoja na kuongea na wanawake usiku kucha 2melala pamoja
nikashindwa nikarudi nyumban....nilijifungua nikamwambia hata hongera Hamna...
baadae akaanza ku2ma hela ya matumizi kama kawaida mtoto anamiaka karibia 2....yule mwanamke kaolewa na mwanaume mwingine mwezi uliopi ata
juzi kaja ooooh nimsamehe bado ananipenda na bra bra kibao ....e. t 2ishi pamoja lakini wazazi wake wasijue na bila ndoa....
jaman huyu kaka mzima kweli...
binafsi nilikua natamani sana mzazi mwenzangu arudi atuishi pamoja. lkn sio kwa staili hii
kama kweli anania kwanini hataki wazazi wajue?????
naombeni. ushauri wenu wapendwa
Kimbia.. Usikubali
 
Achana nae huyo hana mpango nawewe na kumbuka kaja kwako baada ya kipenzi chake kuolewa so dadangu huyo mwanaume hakufai we kua nae kwa jili ya kulea mtoto hayo mengine achana nayo.
 
Mahari kalipa nawewe umeshazaa sasa mtaishije kwa siri??ukiona hivyo ujue ana mke mwingine huyo.
 
Back
Top Bottom