Ushauri: Mwanamke kutoa ujauzito kwa vidonge vya Misoprostol na kutokwa damu mfululizo

Habari za majukumu wana jf. Nina ndugu yangu alitoa mimba ya mwezi 1 kwa kutumia vidonge vya misoprostol tatizo ni ana bleed Leo siku ya NNE. Atumie nn kukata hiyo kitu?
 
Mi nilimwacha msichana kwa sababu ya kutoa mimba, kiongozi una moyo mpaka leo upo nae. sababu ya kutoa mimba alisema ni nini? Mara nyingi wanakuwaga wamechanganya madesa.

Kwa uelewa wangu hata siku moja binti huwa haombi wala kulazimisha kutoa mimba. Ila atakulazimisha uende kwao ukakamilishe taratibu, kaa chonjo unaibiwa mkuu A.K.A.47
Mkuu wachache tutakuelewa
 
wana jf habari
mpenz wangu alitoa mimba kwa kutumia vidonge(misoprostol).

Sasa hivi anatokwa na damu none stop takriban one consecutive month.

Naomba kwa yeyote anayefahamu madhara ya muda mfupi/mrefu ya vidonge hivi anijuze ili niweze pia kufaham.

NB: nilimkataza sana asitoe hiyo mimba hadi ilifikia tukashirikisha ndugu,jamaa na marafiki lkn alifanya kwa kificho.

Nawasilisha
amevuna alichokipanda,naomba kama ulimuonya muache akale na wakwao!kutoa mimba bila kukubaliana na mpenzi wako ni kumkosea,amekukosea sana,achana naye hyo sio mimba ya kwanza kutoa,amejuaje hvyo vidonge na kazi yake?hajagoogle hyo ni mtaalamu!
 
Hiyo ni dhambi kubwa mmefanya kuua kiumbe ambacho hakina hatia halafu bado mnaona ufahari kuutangazia umma Kama mmetoa mimba usikute siwanandoa na hiyo mimba imepatikan ktk zinaa mrudieni mola wenu Na mumtake msamaha kuna watu wanatafuta walau mtoto mmoja tu nyie mnaona fahari kutoa mimba
 
kutoa mimba nikosa kisheria pia ni dhambi lakin basi tu nisiongee mengi nirudi kuku saidia kama ulivo omba

kwanza naomba ujue hiyo missoprostol c dawa ya kutolea mimba bali ni dawa ya aina flani ya chronic acers vidonda tumbo pia hutumika ktk induction of labour kwa mama waja wazito walio pitiliza wiki za kuji fungua na hawana dalili za uchungu na hii hufanywa na wataaram wa afya tu tena kwa uangalizi mkubwa

kinacho fanyika na mabinti kwa kutumia misso kwa njia zao maana husababisha uchungu kabla ya wakati na kupelekea servix kufunguka (mlango wa uzaz) hivyo mlango wa uzazi huwa wazi na bleed kuendelea
kinacho fanya ableed muda mlefu ni retains ya hicho kiumbe + placenta kama wiki za mimba zilikua zaid ya 12 na uki mwacha ata bleed hadi kufa kwa anemia au kizazi kuoza
Ili kutoa hizo retains na blood clots kuna procedure lazima akafanyiwe hosp. (evacuation) na huduma zingine na ushaur ata patiwa hosp nb:kutoa mimba ni hatari sana una weza kufa kwa kupoteza dam nying au kuharbu kizazi pia nikosa kisheria walai unafungwa maisha kuanzia mtoaji mshauri na mtolewaji wote kikubwa zaidi ni dhambi lazima ukalijibie peponi tubuni na mcrudie
 
Mpo wapi na huyo mpenzio? tafadhali chukuwa hatua haraka mwezi mzima mtu anatokwa tu na damu! dah kuna watu wanavumilia maumivu mpaka inashangaza
kwani nae alitoa mimba?? au ana tumia njia gani ya uzazi wa mpango?? au nitatizo lake la muda kidogo?

andika kiswahili we mzee vipi, mbona unataka kutuchanganya!!? "whitish meatlish" ndio nn
 
wana jf habari
mpenz wangu alitoa mimba kwa kutumia vidonge(misoprostol).

Sasa hivi anatokwa na damu none stop takriban one consecutive month.

Naomba kwa yeyote anayefahamu madhara ya muda mfupi/mrefu ya vidonge hivi anijuze ili niweze pia kufaham.

NB: nilimkataza sana asitoe hiyo mimba hadi ilifikia tukashirikisha ndugu,jamaa na marafiki lkn alifanya kwa kificho.

Nawasilisha
Katubuni Mkuu Kwa Dhambi uliyoshiriki ... And Never Let it happen Again kwa Mtu Yeyote
 
even my wife anamenstruate ni 3 week now inanitisha sana sometimes pieces of somesort just like whitish meatlish
Kwa huyo aliyetoa aende hospital akasafishwe mapema na aeleze ukweli alichokifanya Marie stopes yoyote aende kuna Mwenge Africa Sana,kimara Bucha, Temeke sokota na Mabibo mwisho.Na atafute choya(Roselle) achemshe anywe kama juice kwasababu ya damu aliyopoteza na akipata pia ubuyu wa unga ule mweupe achanganye.


Baba wiki 3 ni nyingi Kama mkeo anatumia sindano kama njia ya uzazi wa mpango na ndo mara ya kwanza huwa inatokea mpaka mwili uzoe na kama hatumii mpeleke kwa gyno labda ni hormonal imbalance inayopelekea PCOS ambayo daliili ni hiyo heavy menstruation na kupata vibonge vya damu,kutokupata kabisa au kupata kidogo.Pia atumie hiyo therapy hapo juu arudishe damu yake.
 
Kama Criminal abortion hiyo angalia asipate Septic abortion

Hizo miso alimeza au aliingiziwa?

Kuna uchafu umebaki ndani(incomplete abortion)

Kwa usalama wako mpeleke hospital akasafishwe kizazi hicho na kupima uwingi damu

Asije kupata shida ya heart failure kutoka na upungufu wa damu

Asije kurudia tena Sheria ikiamua kuchukua mkondo wake ni Kesi hiyo asee(criminal abortion)
 
hizi dawa kwa kweli ni mbaya sana,"thanks"!on the way to hospital now!
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa miso ni dawa ya ku induce uchungu kwa mama mjamzito. Wanatumbukiza kwenye njia ya uzazi. Sasa yy sinui alikunywa au alitumbukiza. Daah poleni sanaa.
 
Back
Top Bottom