Aventus
JF-Expert Member
- Mar 8, 2013
- 1,914
- 1,977
Habari za mida hii?
Kama kichwa cha habar kinavojieleza.
Kabla ya kuomba ushauri wacha nitoe habar kamili.
Nilifanya uchunguzi mfupi na kugundua Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Bariadi iko na wakulima wachache sana wa kilimo cha umwagiliaji hasa kwenye kilimo cha mboga mboga na matunda.Basi nikacheki nini kinaweza kulipa katika kilimo hicho cha umwagiliaji.kwa ushauri wa watu wa karibu tukaona tikiti maji ndo linalipa.
Kwa target ya haraka ni kulima kipindi cha mwezi wa tano kwenda wa sita ambapo mvua ndo zinaishia.Ili wale wanaolima kwa kutegemea mvua wakivuna na mazao yangu ndo yanakaribia kukomaa.na wale wa kumwagilia ambao wanaanzaga kupanda mvua zinapokwisha wao wakipanda mimi nakuwa niko karibu na mavuno hivo sokon tunakua wachache.pia huo ushauri niliupata toka kwa KILIMO MAARIFA.TAJIRI(namshukuru) kama sikosei.
Asikwambie mtu yale mahesabu na motisha zinazowekwa hapa ni tofauti na ukiingia shamba.tegemea kilimo kitakua na gharama zaid ya unavofikiri.
Kwa kuwa ni kilimo cha kumwagilia nikalima karibu na mto.Kwa bahati mbaya mvua za juzi zilikuwa kubwa mpaka maj yakajaa mto na kutoka nje kuingia mashamban na kuondoka na miche yote.
KILIMO KINA CHANGAMOTO SANA NA CHANGAMOTO ZAKE NDO HIZI ILA SIJAKATA TAMAA..
Nina nia ya kurudia.Gharama zilizopotea ni LAKI 9 NA 40.
sasa naomba ushauri je
Ni sahihi nikipanda mbegu upya kwa kipindi hiki ama nisubiri mpaka mvua zikome kabisa?
Mwanzo nilinunua mbegu za Balton Tanzani nilipanda 3 kila shimo na ziliota kwa 90%.sasa hivi sasa mfuko hauko vyema naweza kutumia mbegu zilizokusanywa kienyej?
Ushauri wowote wenye maslai napokea