Ushauri murua kwa UKAWA kuelekea uchaguzi mkuu 2020

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,113
2,000
Kabla ya kufikia mwaka 2020, chukueni idadi ya majimbo yote ya ubunge nchini mapema, yawekeni mezani kaeni mapema vyama vyote vinavyounda UKAWA! Pangeni mikakati na hata namna ya kuzikabili hujuma za wizi wa kura mapema kwa namna yeyote ile. Hili linawezekana kabisa provided kila jimbo wasimamizi ni mawakala wa CCM, Wapiga kura ni raria wenyewe na sio wahujumu hao,hivyo mnaweza kulikabili hilo. CUF Waliweza kule unguja na Pemba nanyi huku bara inawezekana.


Nendeni vyuoni, kwenye taasisi za umma na binagsi chukueni vijana jasiri na wasomi muwashawishi na kisha Wavuteni kwenu wasimamisheni kwa kila jimbo kugombea ubunge,Ikiwezekana undeni timu yenye watu makini ya kuwapata watu hao kwa namna yeyote ile. Sehemu ambazo zinaonekana kua na wakongwe wa CCM waliokaa miaka mingi na wale watakaowapa changamoto wataftieni muarobaini yake, wagombea watambulisheni mapema wajulikane kwa kila jumbo.Yaani msiachie jimbo hata moja na msiwe na huruma na mtu.


Mkishinda majimbo mengi mkaizidi CCM, Mkuu wa nchi hatakua na la kufanya kwenye maamuzi, hatoweza kusaini mswaada wowote wa sheria bungeni bila kupitia kwenye mikono yenu. Nzuri zaidi kipo kipendele cha sheria kinachosema kua kiongozi yeyote kama hamjaridhika na utendaji wake mnaweza kupiga kura za kumuondoa kwa sababu akidi mtakua nayo ninyi.


Mtambue kua kwa wingi wenu huo mtakua na spika wa bunge na naibu spika wake, mtakua wenyeviti wa bunge, mtakua Waziri Mkuu na Muhimbili mzima wa bunge utakua chini yenu.


Nawajakishieni kua mkiliweza hilo, mkaweka ubinafsi na uswahiba pembeni mkatazama uwezo wa mtu, hakika mtakua mmejitwalia madaraka na nafasi ya kiti cha urais kabla ya 2025.
 

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,731
2,000
Mimi kawaida mkimsimamisha
Lowassa mimi na kundi langu
Tutafanya juu chini kuhakikisha
Ikulu anaiona kwenye tv tu na
Upinzani nchi hii hatuwezi
Kuwapa nchi Lowassa mwambieni
Hatokuja kuwa rais wa nchi hii hana sera wa hoja hana mikakati ya kuongoza
 

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,113
2,000
Mimi kawaida mkimsimamisha
Lowassa mimi na kundi langu
Tutafanya juu chini kuhakikisha
Ikulu anaiona kwenye tv tu na
Upinzani nchi hii hatuwezi
Kuwapa nchi Lowassa mwambieni
Hatokuja kuwa rais wa nchi hii hana sera wa hoja hana mikakati ya kuongoza
Iwe hivyo hivyo na ubunge mkuu.
 

mwandikitabu

Member
Dec 8, 2016
66
95
well said mkuu,watu ukawa waufanyie kazi ushauri huu, waache ubinafsi,waungane kweli kweli na watambue kuwa damu ya watz iliyomwagika wakati wa harakati za kuimarisha upinzani bado haijakauka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom