Ushauri: Mume wangu kampa mimba msichana wa kazi

bablon6

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
629
565
Mume wangu kabadilika sana siku hizi, kwanza hanigusi tena kitandani. Pili, akampa msichana ya ndani mimba. Sasa naamua tu nimuue.

Nachunga ushauri wako kwa haraka kabla sijammaliza.


e55eca59a92dec760f620641822ace91.jpg
 
Kama umesalitiwa kihivyo, mshukuru Mungu kwani imeandikwa; Shukuruni kwa kila jambo. Huwezi kujua ingelikuwaje hiyo mimba kama ungeliibeba wewe..
Jambo jingine, unalalamika ati hakugusi tena kitandani. Je, wewe unamgusaga?? Msingojee kuguswa tu, nawe mguse. Akikaa kimya muwahi kabla hamjazima taa, umwulize; Unataka nijisikieje?
 
Unaomba ushauri juu ya kuuwa?/ OK tumia sumu ya panya mpige juju au mwendee kwa kalmanzira

nakutania.. kuua mtu sio suluhisho LA matatizo yako adui yako ni huyo binti wa kazi na pengine kuna uzembe wako kidogo timua huyo binti
 
Inaonekana mna migogoro siku nyingi hadi hamgusani!!!! tena inawezekana chanzo ni wewe. Rudisha mkanda nyuma ujue chanzo cha yote hayo. Rekebisha na timua House girl.
 
Mume wangu kabadilika sana siku hizi, kwanza hanigusi tena kitandani. Pili, akampa msichana ya ndani mimba. Sasa naamua tu nimuue.

Nachunga ushauri wako kwa haraka kabla sijammaliza.


e55eca59a92dec760f620641822ace91.jpg
Asallalleh!

Ndo maana unaitwa bablon, yaani mwenye maamuzi ya ajabu ajabu. Wewe umehakikisha kiasi gani anakugisa? Yaani house girl amekushinda hadi unataka kuua? Masuala ya kumpikia mmeo, kufua nguo za mmeo hadi za ndani, kusafisha chumba na kutandika kitanda vyote afanye house girl kwanini asionewe huruma!

Uue ili uhukumiwe kunyongwa! Ni ujinga! Hata Mungu kawaleta watumishi wake kama akina Tito wa Dodoma kuja kutanzua hiyo shida, wewe unarudi kule tulikotoka! Muue afu tukuhoji!
 
  1. Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema. WARUMI 12:21
  2. kubali mtoto azaliwe hustahili kuua na pia kumlea
  3. liangalie tatizo kwa kuangalia madhaifu yako kabla ya kuhukumu wapi ulikosea.
  4. angalia mazuri aliyotenda mumeo ukilinganisha na uovu wake
  5. angalia pia madhara yanayoweza kutokea kwa watoto kwa maamuzi ya kijinga utakayofanya.
  6. mwisho ukishindwa jipange kama unatengeneza mpango kazi jinsi utakavyishi jela kwa maisha yako yaliyobaki na ujioji je unaweza kuhimili kwa mpango unaokusudia kuutekeleza?
 
Sasa umeshaamua kumuua ushauri wa nini tena? Muue tu tutakuja kukutembelea segerea
 
Mume wangu kabadilika sana siku hizi, kwanza hanigusi tena kitandani. Pili, akampa msichana ya ndani mimba. Sasa naamua tu nimuue.

Nachunga ushauri wako kwa haraka kabla sijammaliza.


e55eca59a92dec760f620641822ace91.jpg


USHARURI:

1. Wewe ndo umesababisha anafanya hivyo.
2. Unalotaka kufanya ni ujinga ila ni maamuzi yako.
3. Two wrong don't make it right.
4. Do what you think is right, who cares? who will go to Jail?
 
Fikra zako za kumchoma kisu hazitakusaidia.. labda kama unataka maisha yako ya baadae yawe jela.

Sali Mola akufungulie uamuzi mzuri na wakukupa wewe furaha.

Lingine kwa hiyo binti wa kazi bado unaishi nae?
Na inawezekana ana watoto wengine ambao hauwafahamu.
 
Yawezekana hujui kucheza michezo ya beki 3 imemchanganya mzee jifunze kucheza mechi dk90 za nguvu ataacha
 
Back
Top Bottom