Ushauri: Mume wangu amenikataa baada ya kupunguzwa kazi, kwa madai kwamba alioa mwalimu na si mama wa nyumbani

Kweli ndoa nyingi watu wanatafutaga nafasi tu ya kubadilisha mke/mme huwa watu wanavumiliana tu ila washachokana kabisa.
 
Huo ni ujinga uliopitiliza kwani kazi ni ya kuajiriwa tu, kweli huwezi kuanzisha mradi wowote wa kuingiza hela, hadi umwambie mwenzako ondoka, nimekuwa bored sana, utadhani mie ndio muhasika
 
Huyo MUMEO itakuwa alikuwa na yake ya MOYONI tokea zamani.

Hiyo yote imekuwa kama ni sababu ya kukutosa kiulaini.

Mumeo ilibidi awe na wewe Bega kwa Bega kwa kipindi hiki, ikiwemo kupeana msaada wa kimawazo.

Kazi za kuajiriwa utakaposimamishwa haina maana ndio mwisho wa Maisha yako.

Huyo MUMEO akumbuke kuna kitu kinaitwa Miradi.

Hata Miradi midogo midogo sio mbaya ukianza nayo, na baadae mambo mengine yatafuata
 
Pole sana ndugu, moja ni kuikubali hali ya kuwa c mwajiliwa tena, jichanganya kivingine mtaani ili kupata riziki ya familia yako huyo jamaa atarudi tu ni stress tu!
 
Hilo swali silipendi kabisa ,na kama niliisave namba yake naifuta kabisa......... Afu hawajuagi wanawake sisi ni waropakaji ipo siku nitaongea tu kulalamika so haina haja ya wao kuuuliza such question
Mara nyingi wa hivyo ni wazee wa vitonga, a.k.a mariooooo
 
Pole sana, ulimtoa wapi huyo mwanaume? maana hafai hata kwa bure, Usiondoke goma, ukiondoka tu, kesho yake anaingizwa mwingine
 
Wakuu habari!! Bila kuwapotezea muda kilicho nisibu ni hiki hapa. Baada ya miaka 15 ya ndoa nikiwa ni mtumishi idara ya elimu nimejikuta napata ajali kazini kwa kupunguzwa kazi katika sakata la vyeti feki, katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto watatu.

Kilichonifanya niombe ushauri kwenu ni kwamba baada ya kupunguzwa kazi mwanaume amenikataa katakata kwa madai kwamba alioa mwalimu na si mama wa nyumbani.

Licha ya kuwashirikisha wazazi wa pande zote mbili lakini bado mume wangu ameendelea kushikiria msimamo wake kuwa yeye alioa mwalimu na si mama wa nyumbani.

Na anasisitiza kwamba nichague chochote ninachotaka niondoke nacho maana yeye hayupo tayari kuishi na mama wa nyumbani.

Mpaka sasa nipo njia panda, naombeni ushauri wenu wakuu.
Basi sawa mwambie akupe talaka
 
Pole sana dada nafikili ni wakati sahihi wa wewe kuanzisha safari nyingine ya maisha ukiwa alone a.k.a jeshi la mtu mmoja, huyu mumeo kashakuonesha ni jinsi gani akuhitaji katika maisha yake na alitafuta sababu tu ya yeye kukumwaga.

Mtangulize Mungu katika hiki kipindi kigumu kwako na naamini kupitia yeye utapata njia ya kuyashinda haya majaribu
 
....Hiyo ni nyumba yenu, ahame yeye, siyo wewe!,..maisha siyo kuajiriwa tu, unaweza fanya shughuri nyingine ya kukuongezea kipato...Jiamini na utaweza.
Upo sahihi. Yeye ndio anapaswa kuhama maana yeye ndiye alikukataa. Ww baki nyumbani mwako, infact ukiona anakunyanyasa nenda mahakamani uzeni nyumba mgawane mlichochuma kila mmoja aendelee na maisha yake, binafsi singependa mfikie hatua hii natamani ndoa yenu irudi katika amani.

Lkn pia kama mumeo hakuwahi kujua kuwa una cheti feki inaonekana amepatwa hasira kuwa ww ni mtu hatari sana umewezaje kuitunza siri kubwa namna hiyo kwa miaka 15!!

Pia inatia mashaka mapenzi yake kwako! Maana yake hakukuoa wewe bali alioa ualimu! Binafsi nilidhani huu ni wakati muafaka wa kuonesha upendo wake kwako kwa kukupa faraja na kukuonesha fursa nyingine zilizo nje ya mfumo wa ajira. Nachelea kusema kuwa inawezekana mumeo alikutegemea ww zaidi kuliko yeye binafsi katika gharama za maisha ya nyumbani.

Mwisho nakupa tumaini jipya kuwa zipo fursa nyingi nzuri nje ya mfumo wa ajira kuliko kwenye ajira. Ukikomaa na kumtegemea MUNGU unaweza tengeneza pato zuri hivi sasa kuliko kipimdi cha miaka 15 ulichokuwa mtumishi wa umma. Usihuzunike, kilichokupata ni matokeo ya kile ulichokichuma kwa mikono yako maana ww mwenyewe ndiye uliyepanda, Karma!
 
Pole sana mkuu ndoa nyingi watu wanaoana kupata backups na sio kwa sababu ya upendo ila kuna maisha nje ya ajira ,fanya hata biashara ya kuchoma chapati badae utajikuta unafungua mgahawa ,anza kwa chochote kile kidogo unachoona kinafaa ukiwa na nia utafanikiwa Mungu akufanyie wepesi.
 
Wakuu habari!! Bila kuwapotezea muda kilicho nisibu ni hiki hapa. Baada ya miaka 15 ya ndoa nikiwa ni mtumishi idara ya elimu nimejikuta napata ajali kazini kwa kupunguzwa kazi katika sakata la vyeti feki, katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto watatu.

Kilichonifanya niombe ushauri kwenu ni kwamba baada ya kupunguzwa kazi mwanaume amenikataa katakata kwa madai kwamba alioa mwalimu na si mama wa nyumbani.

Licha ya kuwashirikisha wazazi wa pande zote mbili lakini bado mume wangu ameendelea kushikiria msimamo wake kuwa yeye alioa mwalimu na si mama wa nyumbani.

Na anasisitiza kwamba nichague chochote ninachotaka niondoke nacho maana yeye hayupo tayari kuishi na mama wa nyumbani.

Mpaka sasa nipo njia panda, naombeni ushauri wenu wakuu.
Kamana watoto wa tatu basi wewe usiondoke sehemu yoyote ile na wala usithubutu kufanya hivyo anavyotaka

Huyo atakuwa alitafuta sababu muda mlefu alikini alizikosa na inaonekana wewe ni smart sana mpaka sababu alikosa


Kwa kujisimamia huko

Mwambie huendi sehemu na yeye kama hakutaki kwa kuwa yeye ndio anakosa furaha ya wewe kuwepo, basi mfungukie bila kupepesa macho na umwambie aondoke yeye akaitafute furaha kwa hao walimu,

Mwambie hutoki tena kibabe, simama kama mama, kwa muda uliokaan naye unatosha kabisa yeye kukupisha ukalea wanao.

Narudia tena ajiri uliyoipata siyo hiyo ya kazi bali ni mwanaume asiye mume.


Lakini:-
Kama uliwahi kuitumia nafasi ya kazi yako kumnyanyasa, sasa hivi utanyanyaswa na nafsi yako, manayake akili zenu mnazijua wenyewe
 
Mpeleke mahakamani omba mgawane mali mlizochuma, custody ya watoto na matunzo kwa watoto mtu akikukataa usilazimishe atakuja kukuua
Hapa hakuna haja ya kugawana kwa sababu aliyechoka ni mwanaume anapaswa aipishe familia hapa anapaswa awe na roho ngumu tuu mwanamke hajawahi shindwa kwa mwanaume
 
Nafikiri kwenye asset mlizonazo mchango wako pia ni mkubwa hivyo kwa kuwa yeye hakutaki basi cha muhimu akupe mgawo wako ujipange upya na maisha yako ukishapata mgawo wako fanya namna upate mtaji uanzishe biashara na in shaa allah nahakika utatoboa kikubwa ni uwe na determination kuhusu watoto pata msaada wa kisheria ili na yeye ashiriki katika mahitaji ya watoto.
 
Pole sana dadaangu sasa ndo amekuwa halisi mwanzon na yeye alikuwa feki na kwakuwa alikuwa na upendo feki mpe na ajali kwenye mapenzi wanaume wa hivo wako wengi ambao hawawezi kuhudumia familia zao jipange upya anza maisha mapya kuna maisha mengine pasipo yeye na ajira ya serkali .Mungu wa mbinguni akutie nguvu.
 
Yule sio mariooo maana hela alikuwa ananipa vizuri tuuu ..... nadhani hakuwa comfortable kuona nipo tu nyumban nasubir ajira!
Akutafutie kazi kukuacha sio uamuzi sahihi maisha hayapo hivyo anavyo yachukulia yeye kwamba kazi ndio msingi wakilakitu biashara pia inalipa
 
Back
Top Bottom