Ushauri: Mume kampiga simu ndugu wa mke, mke anadhani anatembea na mumewe

fijohnas

Member
Mar 20, 2018
23
5
Ndugu habari zenu,

Jamaa yangu wa karibu amepatwa na mkasa huu; nyumbani kwake anaishi yeye, mke, watoto na ndugu wa mke wake jinsia ya kike.

Siku moja alienda safari, kabla ya kurudi alitaka kushonea watoto sare ya kanisani, akampigia mkewe kumuulizia juu ya rangi ya sare, simu ya mkewe ikawa inatumika hivyo akaamua kumpigia yule binti ambaye ni ndugu wa mkewe wanaeishi naye pale nyumbani.

Baada ya kupata rangi ya sare, jamaa alishona zile nguo akaenda nazo nyumbani, alipofika mkewe akamwambia rangi ya nguo siyo inayohitajika kanisani na akahoji ni nani aliyetoa taarifa juu ya rangi ya sare iliyoshonwa, jamaa akasema kuwa ni yule binti, ndugu wa huyo mwanamke.

Mwanamke akahoji tena ni kwanini apigiwe simu huyo binti badala ya yeye(mkewe na jamaa), jamaa akaeleza kuwa alimpigia ila namba yake ikawa inatumika na kwa vile alikuwa na haraka basi akaamua kumpigia huyo binti.

Kuanzia hapo hakuna amani, yule binti(kwa sasa yuko safari)alipigiwa simu na ndugu yake na kuelezwa kuwa hapaswi kurudi pale nyumbani kwa madai kuwa anatembea na jamaa.

Kwa ujumla jamaa anashindwa afanye nini kwa kuwa anasingiziwa kosa ambalo hahusiki kwa namna yoyote ile na anamchukulia yule binti kama sehemu ya familia yake, hivyo anaomba ushauri ili kuondokana na mkasa huu.
 
Shida nikwamba sare iliyoshonwa sio?

Au shida nikwamba shemeji anaenda kwao?

Au shida nikwamba amempigia simu shemeji badala ya mke?

Mimi naona huyo mwanamke hamtaki jamaa
 
Shida ni kwamba mwanamke anamlazimisha jamaa kuwa anamahisiano ya kimapenzi na ndg wa mkewe,jamaa anakataa kabisa kuhusika na hilo
 
Tatizo hapo ni kuwa kwanza mume hakumtaarifu mke wake tena hata kwa msg baada ya kuongea na mdogo mtu,
Pili, mdogo mtu hakumwambia Dada yake kuwa amewachagulia rangi wanae.
Hapo lazima kuna kitu baina yao
Mume asijizungushe kwa masuala mazito yanayotaka majibu
 
Kweli kabisa
Kwani simu inatumika dakika ngapi?
 
ikiwa huyo mwanaume hana mazoea na huyo shemeji yake ya ukaribu na mkewe anamshuku. jambo moja tu anatakiwa alifanye kwa umakini sana kuona kama mkewe hamsaliti. mara nyingi sana mkeo akiwa anakusaliti nafsi inamsuta kuwa na mwanaume pia anamsaliti bila hata kuwa na chembe ya dalili za uhakika. hili nina uzoefu nalo!!!!!hata hivyo mwanaume inatakiwa kuwa mvumilivu na mpole kutafuta suluhisho la tatizo kama hili.
 
Mke anahaki kulaumu, menikumbusha story moja ivi, mke alichukua mdogo wke wa kike alipojifungua ili aje kumsaidia kaz nyumban...matokeo yke Mme kamla mdogo wa mkewe adi kapata mimba...na unaambiwa kipindi chote mke hakuwai kususpect chochote, wala hawakuwa na ukaribu, mdogo MTU kashka mimba na mke ana mimba ya pili ...mdogo MTU akiulizwa mimba ya nan anasema cjui, lol
Miaka 20 baadae mke anakuja kujua mdogo wke kmbe alitembea na mumewe na mtoto juu...yan kaja kugundua baada ya mtoto kukomaa nataka kumjua baba angu ,mama ndo akatoa siri...
 
Tobaaaa!!
 
Sijaona shida hapa,

Mke akitimua nduguye nyumban kwako, unachokasirikia nn. kama angemtimua ndugu wa mume kwa sbb zisizona miguu wala kichwa ndo pangechimbika.

Hapo mume apige miluzi tu, waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba.
 
Ndugu habari zenu,

Jamaa yangu wa karibu amepatwa na mkasa huu; nyumbani kwake anaishi yeye, mke, watoto na ndugu wa mke wake jinsia ya kike.

Siku moja alienda safari, kabla ya kurudi alitaka kushonea watoto sare ya kanisani, akampigia mkewe kumuulizia juu ya rangi ya sare, simu ya mkewe ikawa inatumika hivyo akaamua kumpigia yule binti ambaye ni ndugu wa mkewe wanaeishi naye pale nyumbani.

Baada ya kupata rangi ya sare, jamaa alishona zile nguo akaenda nazo nyumbani, alipofika mkewe akamwambia rangi ya nguo siyo inayohitajika kanisani na akahoji ni nani aliyetoa taarifa juu ya rangi ya sare iliyoshonwa, jamaa akasema kuwa ni yule binti, ndugu wa huyo mwanamke.

Mwanamke akahoji tena ni kwanini apigiwe simu huyo binti badala ya yeye(mkewe na jamaa), jamaa akaeleza kuwa alimpigia ila namba yake ikawa inatumika na kwa vile alikuwa na haraka basi akaamua kumpigia huyo binti.

Kuanzia hapo hakuna amani, yule binti(kwa sasa yuko safari)alipigiwa simu na ndugu yake na kuelezwa kuwa hapaswi kurudi pale nyumbani kwa madai kuwa anatembea na jamaa.

Kwa ujumla jamaa anashindwa afanye nini kwa kuwa anasingiziwa kosa ambalo hahusiki kwa namna yoyote ile na anamchukulia yule binti kama sehemu ya familia yake, hivyo anaomba ushauri ili kuondokana na mkasa huu.
amtafune tu ijulikane moja
 
Sijuiii nkwambiee nn ila nakshaur usipende kujifcha kweny kichuguu kuficha uovu wako,we sema huyo jamaaa ni wewe,anyway Acha uboya
 
Sema ni wewe
Yaan umhangaikie mwenzio shida zake wakati zako zinakushinda.

Hana msimamo huyo jamaa mwambie amfukuze na mkewe.
 
Back
Top Bottom