Ushauri: Mume hataki kufanya mapenzi na mimi, anataka mtoto niliyezaa kabla ya kunioa

dahaa hata kuvumilia cjui utavumilia mpk lini pole sana jaribu kuongea nae kwa Mara nyingine uone
 
Alikuwa anatafuta mlezi wa watoto wake,umeshaifanya hiyo kazi wako chuo sasa hana shughuli na wewe.
Pole.
 
nakushauri ukae na binti yako vizuri ujue kama kweli alishamwingilia, na ukidhibitisha, chukua hatua muafaka, ama la hajafanya hivyo lakini alimtaka kimapenzi, dada naomba uondoke unaishi na mnyama wala sio mwanadamu, mimi siwezi kumvumilia mwanaume ambaye nimezaa naye pia awe na hisia za kimapenzi kwa mwanangu, hapana, ondoka mapema dada, wewe hafanyi mapenzi na wewe anawatamani wa nje kuna ndoa hapo? naona unashauriwa eti ujifunze kukatika na nini sijui, chaaa hebu ondoka huyo mtu ameniboa alipotamani mwanao, mapenzi ni trust, kama trust imetoweka sidhani hata usugue goti utahalalisha kumtaka mwanao no way ! leave now
 
Alikuwa anatafuta mlezi wa watoto wake,umeshaifanya hiyo kazi wako chuo sasa hana shughuli na wewe.
Pole.

You are very right very very right, that's absolutely what this scoundrel wanted in this honest woman......
 
Naombeni ushauri wenu,

Mawazo ya wengi ndio nitakayoyafanyia kazi. Nimefunga ndoa na mwanaume mwenye watoto 4 wawili wakike wawali wa kiume. Mama yao alifariki kwa ajali ya gari aliwaacha wadogo wakiwa primary.

Na mimi niliolewa nikiwa na mtoto mmoja wa kike ambae kiumri analongana na mtoto wake watatu. Kusema ukweli mwanzoni iliniwia ngumu sana kukubali ombi lake hasa nikifikiria kulea watoto wa mama mwingine wanikubali, je, vipi kuhusu huyu nilienae?

Baada ya muda kupita na kukolea kimapenzi nilijubaliana nae tukafunga ndoa tukaunganisha familia wote wakawa kitu kimoja. Mungu akabariki tujaliwa kupata mtoto mmoja. Kiukweli niliwapenda sana hawa watoto, niliwalea kama wangu.

Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuwafanya wasijione wakiwa. Kama zawadi nk nilitowa mezani bila kubagua sikupenda kuweka makundi na hili shahidi ni Mungu pekee. Watoto watatu wapo chuo kikuu na mmoja wa kwake yupo form six.

Katika ndoa yangu kulikua na migongano upande wa tendo la ndoa, kabla ya ndoa tukiwa kwenye stori za mapenzi niliwahi kumweleza mwenzangu kuwa mimi sio mtundu sana upande wa sex ivyo ningependa yeye awe mwalimu kwangu kwani tangu mwanaume wa kwanza anidanganye na kunipa ujauzito sikuwa tena kuwa na byfriend.

Akiniambia sawa. Tulipoingia kwenye ndoa mwenzangu alianza kubadilika wakati mwingine alikaa hata miez 8-10 bila kutaka sex.Nikimuuliza husema amechoka au hajisikii.

Hata huo muda anaokaa mpaka mimi nimchokoze na hii nikutakana na kushindwa kuvumilia. Kuna wakat aliamua kuniambia ukweli kuwa sijui mapenzi, niliumia ila nilikubali kuwa ni kweli sijui ila anisaidie kujua.

Hakufanya ivo. Ilifikiwa wakati nikaona ngoja nikae nisimsumbue ila nilijiuliza nitaishi hivi mpaka lini na kusaliti ndoa siwezi. Nilimwomba Mungu sana anipe uvumilivu ila pia Mungu aseme na mimi juu ya hii ndoa.

Mungu ni mwaminifu. Baada baada ya maombi ya zaidi ya mwaka mke wa shemeji yangu alileta malalamiko kuwa mume wangu amekua akimsubua sana kimapenzi ikiwa ni pamoja nakumtumia picha za ex.

Niliziona hakuishia hapo akasema hata hawa wadada wa kazi huwa anatembea nao. Nilipowabana waliopo na walioondoka walikubali na kunipa ushahidi. Mbaya zaidi hata huyu mwanangu alishamtaka kimapenzi sina uhakika kama alifanikiwa au la.

Ninaumia sana sana. Mtaani ndoa yangu imekua mfano wa kuigwa hio ni kutokana na jinsi tunavoonekana kwa watu. Lakini hii yote onatokana na jinsi nisivopenda watu wajue mambo ya ndani. Ninampenda, ninamheshim, ninamjali.Siruhusu nguo au chakula cha mume wangu afanye mwingine nikiwepo.

Hata kama tumegombana nisingependa yoyote ajue, nilijitahidi sana, kuwa mtiifu na mnyenyekevu kwake. Hii nikutokana na malezi niliyolelewa. Hata kama amesafiri watoto watajua baba anarudi kwakua wataniona jinsi ninavokua busy jikoni na kuandaa juisi na matunda.

Ushauri wenu muhimu sana kwangu

Asanteni

Uwiii pole..mungu akutie nguvu hamna linaloshindikana kwake
 
Na kwel atakuwa anau wozo mbaya wa tabia ambapo anatafta vjsabab vy hapa na pale aondoke il hal watt wake amesha walea na kukua
Ushauri ni wa busara huyo mama aufanyie kazi..! kama ndo tabia za huyo bwana huenda huyo mkewe marehem alikufa na siri nzito sana moyoni kwani hiyo tabia cyo ya ghafla
 
Ngumu sana hii ila huyo kujirudi ni ngumu.Kuna thread hapa ya ma sex toys waweza pita huko ujielimishe :angry::angry:
 
Nimepata nguvu sana kuliweka hili kwa jamii mahisi km nimepona. Nilikua mgonjwa kabisa kwa kuwaza, nimepata madonda ya tumbo. Kila siku nikitoka kazin nimekua mtu wa kujifungia ndan na kulia tu. Ila tangu juz nasijisikia aman sana. Nilikua nimebeba mzigo mzito moyoni ninawashukuru sana wote kwa mawazo yenu mazuri. naomba nijibu baadhi ya maswali kuna rafiki aliulira umri wa ndoa ni miaka 8 na miez kadhaa. jamaa si mlev wa pombe wala sigara lkn ana ulev wake. Mtoto nimempeleka kwa bibi yake mama angu ili akaongee nae. Inavoonekana kuna ukweli ndani yake. Mama anahofia kuniweka wazi sana kwakuhofia hali yangu. Hata bint hana raha.. inasemekana kuna wakat nilikua safar kikaz na bint alikua anaumwa sana homa. Alimpeleka kwakutumia gari yake hapo ndipo alipotimiza adhima yake. unaweza kujua ni kias gani inauma. Kiukweli bint alikua anaumwa sana alirudishwa toka shule ili afanyiwe matibabu. Watoto wake wananipenda na kuniheshimu sana, nawapenda pia.Ila ninachoamin ni kuwa huwenda alitaka mama wakulea wanae au ni tabia yake na kumbadilisha itakua kz kubwa. Nazidi kuwashukuru wote.
 
Sehemu pekee ya kumteka mmeo ilikua ndani ya 6 kwa 6. unataka ushauri wa nini wakati amekua honest, kuna njia za kujifunza mapenzi bila hata kuchepuka. tembelea ata majukwaa ya wakubwa[not porn sites] utapata head start, it is never too late,

au endelea kukomaa na kumfulia nguo na kumuandalia juice......


hahaha una maneno
 
Ushauri ni wa busara huyo mama aufanyie kazi..! kama ndo tabia za huyo bwana huenda huyo mkewe marehem alikufa na siri nzito sana moyoni kwani hiyo tabia cyo ya ghafla

Kiwindo;
Yaani kule kwetu wanawaita watu wenye kuona ka weye "Manabii". Yaani umeona kile likichomtoa huyo marehemu duniani kabisaa. Huyu si mtu, ni hasara tuu
 
Pole ndugu yangu, mambo ya utundu kwenye kwenye mechi, huko siingilii sana kwani kuna mazoea,tamaduni,mitindo na mengine ya mkondo huo, kwani wapo makabila ambao wenza wao ni wa asili ya maeneo yanayoaminika yamebobea kwenye hiyo fani na ujuzi lkn wanapuyanga na kupagawa huku mitaani kama hawana skili nzuri, tena kwa utafiti talaka na kutorokana ni nyingi kuliko mikoa 'maamuma' kwenye hilo hbr. Hivyo kupuyanga ni tabia inayotokana na tamaduni,fikra potofu kuwa na partiner wengi we ndiyo kidume,mfumo dume,ushamba na ulimbukeni lkn pia tusipuuzie kuna pepo la ngono linalotokana laana ya ngono kwa ndugu,mtoto wa wako au ndugu wa karibu, dada,shemeji yaani wale muhali kwako! Kama vile laana ya mnyea njiani, atarudia tu, ndivyo lilivyo hilo pepo.Ushauri; Kuachana siyo solution, wala kumuondoa bint si kutatua tatizo. Nenda hizo tailor made shule za mahanjamu, wapo wengi tu wa kukodi, watu kibao wanawafahamu,omba sana Mungu arekebishe maumbile ili yafanane na anavyitaka ili apate 'kukujia' tena, lkn wakati huo nenda kwenye makanisa ya kiroho yenye kuhubiri au huduma ya ukombozi wa Nafsi, waambie Wstumishi wspakwa mafuta na Bwana ili hilo pope litolewe kwake. Najuhakikishia kana utapata huduma sahihi utakuja kutoa ushuhuda humu. Mungu Akutie Nguvu. Ukinihitaji nipo.
 
nitafute nikufundishe mautundu usijali ukirudi kwa mmeo utakuwa poa ila uwe tayari kusaliti ndoa
 
Back
Top Bottom