Ushauri: Mume aiacha familia yake mwaka mpya na kwenda kwa mchepuko

David Harvey

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
2,633
5,038
Habari za mida hii wana JF?

Kuna mfanyakazi mwenzangu hapa ofisini ameniomba ushauri wa matatizo yao ya ndoa yeye na mume wake.

Mume wake ni mfanyakazi wa umma hapa jijini lakini mwaka mpya ulivyoanza hakwenda nyumbani kwake kusherekea na familia yake badala yake alienda kwa kimada.

Alikuwa safari ya kikazi alivyorudi usiku ule wa mwaka mpya hakushinda nyumbani kwake na familia yake alitimka usiku ule ule kwenda kwa kimada kusherekekea mwaka mpya na mbaya zaidi leo hii kamwambia mke wake yupo kwenye kikao cha kikazi kwa mkuu wa wilaya.

Je hivi anavyofanya ni sahihi?
Je mtu kama huyu anayeiacha familia yake katika sikukuu nzito kama hii ya kuupokea mwaka na kupanga mipango ya familia, badala yake anakimbilia kwa mchepuko je nafasi yake katika kijamii ni ipi?
Ni baba anayejitambua kweli?

Naombeni mchango wenu wa kimawazo kumsaidia huyu mfanyakazi mwenzangu coz ameshakata tamaa.
 
Mwambie akae atulie, mwanaume yuko kwenye utaftaji,je hakuna chakula nyumbani,hajalipa karo ya watoto,kodi ya nyumba?

Kama hivyo vyote anafanya yeye huyo mama shida yake nini,huyo njiwa ni wa kwake atarudi tu nyumbani giza likiingia.

Ni kweli kabisa kua sasa watumiahi wa umma wanafanya kazi sana hadi sikukuu, jamaa yuko kazini anaandaa ripoti ya taarifa ya utekelezaji wa miradi ampe mkuu wa wilaya ili mkuu wa wilaya aikabidhi kwa waziri mkuu maana wana ugeni wa waziri mkuu.
 
Kuna mwaka mpya wa kichina nadhani unaanza April, labda jamaa anausubiri huo kujumuika na familia yake?
 
Kusikiliza upande mmoja ni tatizo tu.

Huyo mwenyewe anajua chanzo cha hayo yote na yeye Ndo mwenye power ya kurekebisha hakuna cha kumshauri mume ni wake na ndo anaemjua ni yeye.
 
Mwanamke anakuelezea wewe mwanaume matatizo yake ya ndoa!
Wewe una mke??

Kuna kitu anataka huyo
Kuwa mwangalifu
mbona una mawazo hasi wewe?? kwani kuna tatizo gani? kutoa ushauri kuna ubaya gani?
 
Daaah ! Wanaume hawa jamani mbona mpo hivyo
kwani tumekuaje ,toka dunia kuumbwa tuko hivyo ,huyo mwanamke kama hakupewa pesa ya sikukuuu hapo sawa ,lakini jambo la mzee wa nyumba kukaa nyumbani siku ya sikukuu wakati huko nje kuna maua mazuri huo ni uboya kiwango cha Phd, nyumba ndogo zimekuwepo toka dunia imeumbwa, nabii suleiman alikuwa na wake kma 300 na michepuko kam 700, unakaa na mume mna lala kitanda kimoja jan-dec asipoonekana siku moja tu roho zinawauma,acheni wivu bana kizuri kula na mwenzio
 
je hivi anavyofanya ni sahihi??
je mtu kama huyu anayeiacha familia yake katika sikukuu nzito kama hii ya kuupokea mwaka na kupanga mipango ya familia ,badala yake anakimbilia kwa mchepuko je nafasi yake ktk kijamii ni ipi?
Ni baba anayejitambua kweli???


Anavyofanya sio sahihi'
Baba anayejitambua anajali familia kwanza kupita vitu vingine vyote

Mwambie mfanyakazi mwenzio kwanza asikate tamaa maana nasikia watu wanadai ndoa ina changamoto nyingi
mbona una mawazo hasi wewe?? kwani kuna tatizo gani? kutoa ushauri kuna ubaya gani?

Nisamehe mkuu kwa mawazo yangu hasi
 
Hivi ni vitu vya kawaida mwanaume kuwa na wake zaidi ya mmoja angalien wazazi wetu na mababu zetu. Tuache wivu mume hukuzaliwa naye.
 
kuna mawili jamaa alikuwa na masela wanapokea mwaka au alikuwa na kimada na masela wanapokea mwaka.. cha kufanya mwambie ampotezee maisha yaendee akianza kukimbizana naye ataumia yeye mwisho wa siku.. kama ameshamuuliza jibu alilopewa ndiyo liwe jibu sahihi na asilete ugomvi kwa majibu anayofikiria yeye ana aendelee kuchunguza wapi anakosea na wapi mwenzie anakosea .. bila kutoa hukumu ajirekebishe yeye pole pole mwenzie atajirudi tu .. ila akigeuza nyumba moto kwa lawama , gubu na maugomvi ya kila siku lazima hali iwe ngumu .. .. na wewe kuwa mbali na wapendanao
 
huyo mwanamke hajitambui tuu..... ndoa ni ya watu wawili tuu......mwanaume kazaliwa kuwa MWANAMUME.
 
Mwanamke anakuelezea wewe mwanaume matatizo yake ya ndoa!
Wewe una mke??

Kuna kitu anataka huyo
Kuwa mwangalifu

You are so on point!

mbona una mawazo hasi wewe?? kwani kuna tatizo gani? kutoa ushauri kuna ubaya gani?

Mkuu wewe unaona ni sahihi kuombwa ushauri wa namna hii?

Nakushauri umshauri kwa nia nzuri ajadili hili jambo na mume wake, na wewe pia acha kujipendekeza kwa huyo mama.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom