Uchaguzi 2020 Ushauri mujarabu kwa CHADEMA kuhusu kutumia mapungufu/ makosa katika kuongea kwa Mgombea wa CCM

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,198
3,566
Ukifuatilia kauli za mgombea wa CCM ndugu Magufuli kwa muda mrefu tangu aingie madarakani amekua ana makosa mengi sana kwenye namna ya kuongea na kuwasilisha hotuba zake,amekua na kauli nyingi sana zinazokinzana zenyewe.

Hii ni moja ya mapungufu makubwa ya mgombea wa CCM na CHADEMA wanaweza itumia kama karata ya kuongeza kuamini na kuwafanya wananchi wajue ni mtu wa aina gani.

Mfano wa mambo yanayokinzana ni:

- Issue ya uzazi wa mpango, inakinzana kabisa Vs elimu ya uzazi tunayopewa kila siku

- Issue ya kuwaita Barrick mabeberu na wezi Vs kuwaita wanaume

- Kusema yeye amesafiri sana nje ya nchi akiwa waziri Vs juzi kusema yeye hajawahi kabisa kusafiri nje ya nchi

- Kusema hakumtuma mtu kwenda kugombea vs kusema alimtoa kitila mkumbo aende kigamboni mwigulu abaki singida

- Kusema wasaliti wananakiwa kuuawa Vs Lissu kupigwa risasi masaa mawili baadaye

Hiyo ni mifano michache, ambayo cha kwanza wananchi wengi huwa wanasikia tu vijiweni bila kumsikia live, sasa ushauri wangu ni huu...

CHADEMA irekodi zile audio zoteee zenye kuonesha utata wa kauli za Magufuli, baada ya hapo hizo audio ziwekwe wakati wa mikutano ya kampeni ili watu wasikia kwa masikio yao. Yaani wakati Lissu anahutubia anaposema magufuli alikosea hiki au hiki basi zile audio au hata video ziwekwe live na zitolewe ufafanuzi hapo hapo, ni afadhali kuliko kusema maneno tu kwamba alisema hiki akasema hiki.

Pia wanaweza kutumia audio au video za mwalimu Nyerere zinazoashiria kwamba CCM ya sasa siyo ile aliyoitaka na kuiacha yeye.

Kampeni zinataka ubunifu,siyo kufanya kwa mazoea kama wananchi wanaenda kushangaa wasanii basi CHADEMA waje na kitu cha kuwafanya watu wavutike kuja kwenye mikutano yao ya kampeni.

Kampeni ni Uchonganishi,kutafuta mapungufu ya mwenzio uyatumie kama credit kwako,tafuta mapungufu kadri unavyoweza sababu nina hakika hakuna kipindi zaidi ya hiki CHADEMA watapata wasaa wa kuongea haya,siku tu tume imemtangaza magufuli tangazo lake la kwanza litakua kuzuia tena siasa hadi 2025 wakati wa uchaguzi,kama ilivyokuwa 2015.

CHADEMA kazi ni kwenu,huo ni ubunifu kwenye kampeni
 
Ziko kauli nyingine nyingi sana za kuwatonesha vidonda

- kubomolewa nyumba zao
- mimi sishauriki
- sikulete tetemeko
- mfe tu na mimi nasema eehh mfe
- sileti maendeleo kisa mnachagua upinzani

Rekodi hizi weka upya watu wasikie upya,wtoneshe vidonda....kulingana na eneo husika,wasikie upya waone ni kiasi gani aliwasemea vibaya
 
- Issue ya uzazi wa mpango, inakinzana kabisa Vs elimu ya uzazi tunayopewa kila siku

- Issue ya kuwaita Barrick mabeberu na wezi Vs kuwaita wanaume

- Kusema yeye amesafiri saaana nje ya nchi akiwa waziri Vs juzi kusema yeye hajawahi kabisa kusafiri nje ya nchi

- Kusema hakumtuma mtu kwenda kugombea vs kusema alimtoa kitila mkumbo aende kigamboni mwigulu abaki singida

- Kusema wasaliti wananakiwa kuuawa Vs Lissu kupigwa risasi masaa mawili baadaye

- kubomolewa nyumba zao
- mimi sishauriki
- sikulete tetemeko
- mfe tu na mimi nasema eehh mfe
- sileti maendeleo kisa mnachagua upinzani
 
Mambo yote uliyoyaainisha hapo hayawezi kumsaidia Lissu kushinda uchaguzi hata mwenyewe anafahamu hilo ndio maana anajikita sana kwenye tukio lake la risasi na ndio linalowafanya watu kwenda kumuangalia namna alivyojaa vyuma mwili mzima.
 
Mambo yote uliyoyaainisha hapo hayawezi kumsaidia Lisu kushinda uchaguzi hata mwenyewe anafahamu hilo ndio maana anajikita sana kwenye tukio lake la risasi na ndio linalowafanya watu kwenda kumuangalia namna alivyojaa vyuma mwili mzima.

Tena hili ndio alitumie saaana sababu hawapendi kabisa kulisikia ndio maana wanaanza kuropoka hadi tusiowategemea kama mama Samia

yaani Lissu akamate hapo hapo alipokamata sababu inawaumiza upya kusikia ni mzima na anawasema.

Akae kimya kwa sababu gani?
 
tena hili ndio alitumie saaana sababu hawapendi kabisa kulisikia ndio maana wanaanza kuropoka hadi tusiowategemea kama mama Samia

yaani lissu akamate hapo hapo alipokamata sababu inawaumiza upya kusikia ni mzima na anawasema....
Wananchi wanahaki ya kuelezwa kuwa Chadema wanampango gani na mustakabali wa maendeleo yao ,

Sio mambo ya Risasi,

Au risasi za Lisu zipo kwenye ilani ya Chadema ya Uchaguzi.
 
Wananchi wanahaki ya kuelezwa kuwa Chadema wanampango gani na mustakabali wa maendeleo yao ,

Sio mambo ya Risasi,

Au risasi za Lisu zipo kwenye ilani ya Chadema ya Uchaguzi.

wewe inakuuma nini?!
 
Kama hii ya;
"-sileti maendeleo kisa mnachagua upinzani"

Huku kodi zao anazichukua na serikali yake ya ccm...!!
 
Na alivyo hajielewi mara utasikia akijimwambafai,

" Maendeleo hayana Chama...."
 
IMG_4205.jpg
 
Back
Top Bottom