Ushauri muhimu: Serikali izime kabisa mtandao wa twitter, unatumika vibaya kipindi hiki tunapopambana na Covid 19

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kuna upotoshaji mbaya sana unaofanywa na watu wasio na nia njema na taifa hili na kusababisha taharuki kwa watanzania.

Mtandao wa Twitter unatumika vibaya sana na watu ambao ni wapuuzi na siku zote hawana nia njema na Tanzania kwa sababu zao ambazo hazina mashiko.

Kila mtu anajua sasa hivi kila Taifa lipo kwenye changamoto ya kupambana na Covid 19 new variant.

Lakini inakuwa sio vizuri kuona wapuuzi wachache ambao wanazusha vifo vya uongo, wanazusha kuwa ugonjwa umetapakaa mithili ya wingu zito.

Kiuhalisia bado tuna hali nzuri. Hivyo tuchukue hatua kudhibiti kuenea zaidi, Mungu atatusaidia.

My opinion; TCRA wafungieni Twitter kwa mwaka mzima mpaka hali itulie. Pia VPN zifungiwe ili njia za panya zisitumike kupotosha na kuzua uongo.
 
Tiba ya mawazo kinzani sio kuzima mitandao na kuziba watu midomo.

Tiba ni kusema ukweli na kusahihisha upotoshaji.

Last i checked, wanaotumia mitandao wako milioni 24-30. Ni watu wengi sana.

Hauwezi kukimbizana na kila kichaa anayeropoka mtandaoni.

Be a man and stop crying. WAJIBIKA.
 
Tatizo sio twitter bali uadui walionao watu dhidi ya serikali,
Kama serikali ingekuwa inawatendea wema watu wote hata wale walio kinyume nao huu uadui ungepungua walao kwa kiasi chake.

Lakini pia watu wengi ambao hawakupendezwa na serikali haswa ya ccm walipaswa linapokuja swala la dharura kama hili kwa maslahi mapana ya nchi yetu hii, huo uadui tungeuweka pembeni na kuungana na hata na serikali katika kuangalia namna ya kukabiliana nalo katika mazira yetu.

Matatizo haya ya afya na magonjwa hayakuanza leo wala jana na wala hili halitakuwa la mwisho, leo hii wao hawapo madarakani lakini kesho wanaweza wakawepo je watastahimili matukano yote yatakayo elekezwa kwako na watu wenye mtazamo tofauti na wao.

Siku ambayo tutacha kuhusisha kila kitu na siasa nadhani hapo ndipo utakapo kuwa mwanzo wa hatua yetu kuyasogelea maendeleo.
 
Ona hii hii mbuzi inaandika upuuzi hapa. Serikali inakimbia wajibu wake kwa kujidanganya hilo tatizo halipo.
Kwa akii yako unadhan TCRA inaweza fungia VPN?

Kufungia Twitter ndo kunaleta ahueni ya Corona?
Mumeo ana kazi sana.
Lack of education leads to stupidity
 
Kuna upotoshaji mpaya sana unaofanywa na watu wasio na nia njema na taifa hili, na kusababisha taharuki kwa watanzania.

Mtandao wa Twitter unatumika vibaya sana na watu ambao ni wapuuzi na siku zote hawana nia njema na Tanzania kwa sababu zao ambazo hazina mashiko.

Kila mtu anajua sasa hivi kila Taifa lipo kwenye changamoto ya kupambana na Covid 19 new variant.

Lakini inakuwa sio vizuri kuona wapuuzi wachache ambao wanazusha vifo vya uongo, wanazusha kuwa ugonjwa umetapakaa mithiri ya wingu zito.

Kiuhalisia bado tuna hali nzuri. Hivyo tuchukue hatua kudhibiti kuenea zaidi, Mungu atatusaidia.

My opinion; Tcra wafungienTwitter kwa mwaka mzima mpaka hali itulie. Pia VPN zifungiwe ili njia za panya zisitumika kupotosha na kuzua uongo.
Hujitambui wewe! Kwa hiyo unadhani wanasema uongo vifo vinavyotokana na corona siyo vingi?

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Great thinker
Anaanza na muhimi

Anamalizia kwa kusema kuna Covid-19 wakati mkuu wa nchi anapinga hilo, kisha anakuambia tunapambana na covid-19, kwa tahadhari zipi zilizochukuliwa??

My take
Wewe ni great thinker kweri kweli, Karibu chattel.
 
Back
Top Bottom