USHAURI: Msishiriki Uchaguzi mdogo ujao iwapo..... | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Msishiriki Uchaguzi mdogo ujao iwapo.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Nov 30, 2017.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 17,472
  Trophy Points: 280
  KAMA Rais anawaagiza returning officers wa Tume ya Uchaguzi NEC (maDED) kuwa asisikie DED anamtangaza mpinzani kashinda kwa vile anamlipa mshahara, anampa ulinzi na gari juu.

  KAMA viongozi wa CCM wakiwemo wabunge wanawaagiza wafuasi wa CCM kuwafuata wapinzani kuwapiga na kuwakata mapanga huku wakisema polisi ni yao na mahakama ni yao tena mbele ya polisi bila kuchukuliwa hatua zozote.

  KAMA polisi anatumika kumpiga na kumbruta nje ya chumba cha kuhesabia kura wakala wa Chadema ili abaki wakala wa CCM pekee.

  Na KAMA matokeo yanatangazwa kwa kutumia hesabu zao wanazozipanga wenyewe pamoja na dosari zote kuripotiwa bado NEC inabariki.

  Kuna haja gani ya kusumbua wanachama na mashabiki wenu kufanya kampeni huku mkijua hata mshinde hamtatangazwa washindi?


  Kuna chaguzi ndogo zinakuja za Wabunge majimbo ya Longido, Singida Magharibi na Songea Mjini, najua kabla kutakuwa na mikutano kati yenu na NEC, wapinzani (CHADEMA) waje na RESOLUTION moja ya kuwakataa maDED kuwa returning officers huku mkijenga hoja yenu kutokana na kauli ya rais.

  IWAPO NEC itakataa ushauri huo, kuliko kupeleka watu wakavunjwe miguu na polisi, wakadhalilishwe pengine kuuawa. Mimi nashauri huku nikijua kabisa faida na hasara za kususia uchaguzi, tumejifunza kwa CUF ya Maalimu Seif na juzi tumejifunza kwa NASA ya Raila Odinga, bora mjitoe kwenye uchaguzi huu, ili muanze mikakati mipya ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na matukio hayo mapema kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019.

  Mengi yatasemwa, ila najua watu watawaelewa kuwa mmeepusha maafa kama yaliyotokea kwenye uchaguzi uliopita wa Madiwani, na vile vile mtakuwa mmepeleka 'clear message' kwa watawala na mataifa kuwa kinachofanyika Tanzania sio uchaguzi bali ni mfumo wa kudanganya watu na mataifa yadhani kuwa wako madarakani kihalali na wamechaguliwa na wananchi.
   
 2. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #21
  Nov 30, 2017
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,845
  Trophy Points: 280
  Wanakowanyima kura
   
 3. b

  brazaj JF-Expert Member

  #22
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 26, 2016
  Messages: 444
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 80
  Huu ushauri kuntu. Kimsingi ilikuwa muhimu kuwafahamisha mapema tu hakuna haja ya uchaguzi wowote tena katika status quo. Jitahada ziwekezwe kwenye kupata umoja zaidi wa wapinzani kushinikiza katiba mpya yenye kuweka terrain sawa sawa. Hali ya sasa hivi hailipi maana ni udhalimu mtupu.
   
 4. kalistus komba

  kalistus komba Member

  #23
  Nov 30, 2017
  Joined: Nov 22, 2017
  Messages: 16
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 5
  Kikubwa ni udicteta ndo tukitu tunaendeshwa nacho
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #24
  Dec 11, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 17,472
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana UKAWA kwa kusikiliza ushauri wangu kama NEC hawataki kujirekebisha waacheni wawatangaze wagombea wa CCM kuwa wamepita bila kupingwa.

  Chadema tuko pamoja.
   
 6. c

  chikundi JF-Expert Member

  #25
  Dec 11, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 8,248
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Unachosema kinaweza kuwa sahihi lkn nini kifanyike?
   
 7. c

  chikundi JF-Expert Member

  #26
  Dec 11, 2017
  Joined: Oct 16, 2016
  Messages: 8,248
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Ashinikizwe kwa njia gani? Wakati njia inatafutwa upinzani uendelee kushiriki uchaguzi ama la?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...