USHAURI: Msishiriki Uchaguzi mdogo ujao iwapo..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Msishiriki Uchaguzi mdogo ujao iwapo.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Nov 30, 2017.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 17,483
  Trophy Points: 280
  KAMA Rais anawaagiza returning officers wa Tume ya Uchaguzi NEC (maDED) kuwa asisikie DED anamtangaza mpinzani kashinda kwa vile anamlipa mshahara, anampa ulinzi na gari juu.

  KAMA viongozi wa CCM wakiwemo wabunge wanawaagiza wafuasi wa CCM kuwafuata wapinzani kuwapiga na kuwakata mapanga huku wakisema polisi ni yao na mahakama ni yao tena mbele ya polisi bila kuchukuliwa hatua zozote.

  KAMA polisi anatumika kumpiga na kumbruta nje ya chumba cha kuhesabia kura wakala wa Chadema ili abaki wakala wa CCM pekee.

  Na KAMA matokeo yanatangazwa kwa kutumia hesabu zao wanazozipanga wenyewe pamoja na dosari zote kuripotiwa bado NEC inabariki.

  Kuna haja gani ya kusumbua wanachama na mashabiki wenu kufanya kampeni huku mkijua hata mshinde hamtatangazwa washindi?


  Kuna chaguzi ndogo zinakuja za Wabunge majimbo ya Longido, Singida Magharibi na Songea Mjini, najua kabla kutakuwa na mikutano kati yenu na NEC, wapinzani (CHADEMA) waje na RESOLUTION moja ya kuwakataa maDED kuwa returning officers huku mkijenga hoja yenu kutokana na kauli ya rais.

  IWAPO NEC itakataa ushauri huo, kuliko kupeleka watu wakavunjwe miguu na polisi, wakadhalilishwe pengine kuuawa. Mimi nashauri huku nikijua kabisa faida na hasara za kususia uchaguzi, tumejifunza kwa CUF ya Maalimu Seif na juzi tumejifunza kwa NASA ya Raila Odinga, bora mjitoe kwenye uchaguzi huu, ili muanze mikakati mipya ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na matukio hayo mapema kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019.

  Mengi yatasemwa, ila najua watu watawaelewa kuwa mmeepusha maafa kama yaliyotokea kwenye uchaguzi uliopita wa Madiwani, na vile vile mtakuwa mmepeleka 'clear message' kwa watawala na mataifa kuwa kinachofanyika Tanzania sio uchaguzi bali ni mfumo wa kudanganya watu na mataifa yadhani kuwa wako madarakani kihalali na wamechaguliwa na wananchi.
   
 2. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #2
  Nov 30, 2017
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 9,114
  Likes Received: 9,359
  Trophy Points: 280
  Yaani hii nchi inajiita ipo katika mfumo wa vyama vingi, lakini practically ni kama tupo kwenye mfumo wa Chama kimoja
   
 3. j

  johnthebaptist JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2017
  Joined: May 27, 2014
  Messages: 10,657
  Likes Received: 8,627
  Trophy Points: 280
  Tatizo " Ruzuku", unajitoaje huku fweza unaitaka?!!!
   
 4. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2017
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Hakuna kitu kibaya katika nchi kama kuwafanya wananchi watambue kura zao hazina maana
   
 5. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 5,293
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Quinine, umeandika maneno kuntu na yenye busara na tija kwa wenye hekima na wasikivu. Quinine ni dawa na in vema tuitumie.

  Moja ya mambo ya msingi ni kufanya a scientific study into what really happened on November 26, 2017. Tujue kwa kina changamoto na makosa yetu yalikuwa yapi? Kamati tendaji ifanye hii kazi ikisaidiwa na wataalamu, ikiwezekana hata wa kimataifa. Mwisho, Chadema/Ukawa waje na strong action points.

  Binafsi nina amini ukawa/chadema ilifanya makosa makubwa kuahirisha UKUTA. We need to go back to the drawing board!
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2017
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 11,000
  Likes Received: 4,044
  Trophy Points: 280
  Hebu tuwekee hiyo clip ya mheshimiwa Rais akitoa maelekeza kwa ma DED maana sijawahi kuisikia mbali na kuona tu watu waki comment. Sidhani kama mh. Rais anaweza kutoa kauli hiyo
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 17,483
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, what needed is a surprise and unpredictable strong action.

  Mfano kauli ya MH Mbowe kusema wanachama wa Chadema waanze kujilinda kwa namna yeyote ile ilikuwa strong lakini ilichelewa, kauli kama hiyo ilitakiwa itolewe wakati wa kampeni uwaandae watu kama ni kuvaa bukta wavae mapema au washone, sasa yeye anatoa kauli siku ya kupiga kura lakini nafikiri amejifunza kitu, let us close our fingers.
   
 8. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 5,293
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kuwa alishasema mabaya zaidi ya haya wenye akili tumeelewa. Wewe ngojea clip!
   
 9. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2017
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,913
  Likes Received: 7,482
  Trophy Points: 280
  Aliyeshinda kashindwa, aliyeshindwa kang'ara
  Aliyeshinda katendwa, Aliyeshindwa kapora
  Aliyeshinda kapondwa, Aliyeshindwa hongera
  UCHAGUZI USO HURU, THAMANI YA KURA NINI?
   
 10. Slowly

  Slowly JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 7, 2016
  Messages: 1,072
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  FB_IMG_1507150289722.jpg
   
 11. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2017
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Odinga alivyosusia uchaguzi Kenya kwa sababu kama hizo alitukanwa na bavicha, na ushindi wa Uhuru ukashangiliwa kwa nguvu zote. Bavicha ni kama hayajielewi yanachosimamia..
   
 12. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2017
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Mngeanza kukemea alichokifanya rafiki yenu Uhuru kule Kenya. Double standards at best
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,263
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni huyu dikteta uchwara anayejifanya anaunga mkono mfumo wa vyama vingi nchini lakini wakati huo huo hataki viwe huru kufanya shughuli zake za kisiasa nchini bila yeye kuviingilia. Ashinikizwe huyu aamue kimoja ama mfumo wa vyama vingi au kimoja badala ya kuendeleza unafiki wake ambao unaweza kuwa chanzo cha umwagaji mkubwa wa damu nchini.

   
 14. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 5,293
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Sasa tumeshajua na hatuhitaji kuambiwa tena. From the word go we should be ready for all eventualities. Hii nchi ni yetu sote na hata kama tuko wachache lakini askari ni wachache zaidi. Udhalimu lazima ukomeshwe!
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 17,483
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo CCM imejifunza kutoka Kenya kuwa kama Uhuru alipora kura na CCM ipore.
   
 16. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2017
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 5,293
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Hii katuni nayo nzuri ila usije shangaa 2020 ikawa kinyume chake au ngoma droo. Uvumilivu, upole, woga, utulivu furaha na amani vyote huwa vinakuwa vya kupita na kurudi. Maisha yataendelea tu.
   
 17. Slowly

  Slowly JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 7, 2016
  Messages: 1,072
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtu wa kumwaga damu nyie...mmelewa konyagi...kunyweni maji mpunguze frustration...kama ngome muhimu ya chadema (Arusha na Moshi) imeingiliwa kirahsi hvyo tofauti na 2011 watu walikuwa wanajitoa mhanga....huko namtumbo sasa au tandahimba watasemaje
  ...uzee unawaendea vibaya
   
 18. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2017
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Kama unashangilia jirani yako kuibiwa, na wewe jifunze kuvumilia ukiibiwa. Kama ni kweli mnahisi mnaibiwa..

  Lakini huku mtaani hakuna anayewaelewa tena
   
 19. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 17,483
  Trophy Points: 280
  Mtaani ni wapi?
   
 20. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2017
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 12,867
  Likes Received: 17,483
  Trophy Points: 280
  Ngome imeingiliwa na nani, kama na polisi sawa lakini CCM Arusha mitaani haipo.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...