Ushauri: Mshahara wa 800k naweza kumudu haya yote?

co fm

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,415
2,140
Wakuu nimepata chimbo jipya la kazi kwa muhindi huko baada ya kutoka kwenye sehemu yangu ya awali ambayo nilikuwa nalipwa 1M bila makato.

Sasa nafikiri kwa huu mshahara wa take home ya 800k kuishi.Binafsi mambo kadhaa.

Moja, kutuma wa wazee 100k kwa mwezi.

Mbili, kodi 200k.

Tatu, Nataka ninunue gari japo hela ipo ila mafuta per day 6k x30=180k.

Nne,Chakula 300k and other expenses…

Je nitatoboa? Au nifanye amendments zipi.

Note:Nipo Dar(Sinza, kazi Posta)
 
.
JamiiForums1510998594.jpg
 
Nenda kwanza kazini, ukishaanza kazi sasa ndio utajua njia nyingine za kuongeza kipato au ukipata sehemu nyingine utavunja mkatapa si unaangalia masilahi! Usiache kazi kabla haujapata kazi! Sasa kama 800k unasema haujui kama utatoboa it means ni bora kukaa loosely kuliko kuanza nayo hiyo!

Nenda kwanza job upige kazi hafu what next utajua unaweza ukabana na matumizi kulingana na hela iliyopo pia.
 
Hama tafuta sehemu unayoweza lipa kodi 60k kwenda chini, mshahara laki 8 kisha chumba kodi laki 2 kwa mwezi ni matumizi mabaya ya uwezo wa akili.

Unahisi ni muhimu zaidi kununua gari kwa sasa? Hiyo hela ya gari unayosema ipo hebu fikiria kuifanyia utaratibu wa kimradi iendelee kuzaliana hata kama ni kwa kidogo kidogo ili siku ukiwa tayari kununua gari ununue bila kujiingiza mtegoni, ila hapa sijui kama utanielewa! nina mashaka sana maana mtu kununuaga gari ya kwanza anakuwaga na mcheche mno!
 
Wakuu nimepata chimbo jipya la kazi kws muhindi huko baada ya kutoka kwenye sehemu ysngu ya awali ambayo nilikuwa nalipwa 1M bila makato...
Ndug watu wanalipwa laki tatu au chini yake na wanaishi, unashindwaje kuishi kwa mshahara laki nane? Ninachokiona hapo unataka kuishi maisha ambayo hayatakusaidia kujiajiri na hatimaye kujitegemea
 
Halafu wachaga wakipata maendeleo oooh ni wezi, matapeli n.k
Sasa mpuuzi kama huyu mshara wa lak 8 anaishi nyumba ya laki 2 na anawaza kununua gari.
Utakuwa mtumwa wa kudumu
Muache ajichanganye juu...kodi ya laki 2 na ukute anaishi Dar ni balaaa aisee maisha yapo juu utajikuta una madeni kuhudumia gari
 
Avatar yako usibadili, kama utatoboa au lah, mfikirie mlinzi, mama ntilie, muokota chupa za plastic, wanaofanya kazi kwenye viwanda vya wachina kama pale EPZA external na wafananao, kisha fikiria tena.

Tsh 25,000 kwa siku inakutosha kuishi kama malaika mzee.
 
Sina mkuu ila natarajia
Kama ni hivyo unaweza kujibana huku ukitafuta kazi yenye kipato kizuri zaidi ili uweze kuishi maisha mazuri. Nakushauri suala la gari liweke kando kwa sasa kwani gharama ya uendeshaji ni kubwa zaid ya ulivyoweka hapo 6k kwa siku.
 
Back
Top Bottom