Ushauri: Msaada kuhusu tabia ya wizi iliyokubuhu kwa kijana wangu

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,175
22,576
Wakuu,

Naamini kila mtu huwa anakosea, lakini linapokuja swala la kukosea mara kwa mara huwa linatia hasira sana.

Huyu mtoto wangu anasoma darasa la 6 ,ni mtoto wa Kaka yangu alimleta hapa kwangu ili asome,

Sasa kinachozidi kunipa wasiwasi ni tabia yake ya wizi uliokubuhu!

Yaani kwa umri wake na vitu anavyoiba nabaki mdomo wazi kabisa.

Sijawahi hata kumuadhibu lakini jana imenipasa baada ya yeye kuuza simu tatu kwa bodaboda tatu wakuu!

Bora hata angeuza bei kauza elfu 7.

Alishasema mara nyingi harudii lakini ni yale yale nimempiga na leo hawezi kutembea wa kwenda shule amelala tu.

Alishaiba hela sana ndani huwa nina tabia ya kuweka noti ndogo ndogo kwenye dressing table pale, so anapokuja asubuhi kuomba hela ya kula shule namwambia achukue buku yeye anapita nazo zote huwa nanyamaza tu.

Alishaiba baiskeli ya wenzie shule wakamfuata mpaka huku nyumbani kwangu niliskia aibu sana nilipoambiwa hilo.

Aliiba laptop ya mwalimu! Najiuliza aliwezaje nayo pia walimdaka nayo.

Vingine ndani vitu anauza mfano aliingia Store akauza pampu, aliuza charge ya simu, flash disk yangu pia yenye documents muhimu sanaa aliuza!

Sasa chai anakunywa asubuhi, pesa ya kula shule ninampa, lakini bado anaiba nimekosea wapi? Nikimwambia kaka yangu huko kwake ananilaumu na ndugu wengine kuwa nimemuharibu mtoto wake.

Kuna jirani alisema nimpeleke dogo polisi, hili haliingii akilini polisi kufanyeje sasa kwa mtoto mdogo kama huyu? Si nitamuharibu zaidi?

Mbaya zaidi na kanisani huwa anaenda kila Jumapili.

Nahofia kanisani atakuja kuiba sadaka.

Aliwahi pia kuiba pesa za wageni wangu 65k nikamsachi na kumkuta nazo, imagine aibu niliyoipata!

Nilimnunulia mpira na viatu vya kuchezea soka, lakini cha ajabu aliuza huo mpira, viatu mpaka kijazio!

Hii shida ya kulea mabao ya watu ni ushenzi sana!

Nishauri wakubwa.

UPDATE :
Leo kutakuwa na kikao hapa kwangu ndugu wengi wamekuja wengine hawajafika akiwemo baba wa huyu dogo.
Lengo lao likiwa ni kujadili namna ya kumsaidia lakini mimi binafsi nimenyoosha mikono juu niko radhi kuwaambia ukweli kwamba amenishinda hivyo baba yake aondoke naye mpaka mwisho wa kikao tutajua.
 
Kumlelea mtoto mzazi mjinga yaani unamwambia mwanae ni mwizi(huyo sio mdokozi tena)alafu anatetea ujinga

Chukua zigo rudisha kwao kama swala ni kusomesha chukua mwingine

Dah, hilo ni jambazi tyari na kuacha hawezi yani
 
Kumlelea mtoto mzazi mjinga yaani unamwambia mwanae ni mwizi(huyo sio mdokozi tena)alafu anatetea ujinga
Chukua zigo rudisha kwao kama swala ni kusomesha chukua mwingine
Dah,hilo ni jambazi tyari na kuacha hawezi yani
Tatizo kaka zangu hawawezi na hawataki kusikia ili wanaamini nina uwezo wa kumtunza huyu dogo,
sijui nifanyeje?
 
Back
Top Bottom