Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

Jibu sahihi ni la pale juu....

Jamaa wamebanwa saana mambo ya kodi na pesa zingine.

Kampuni inaenda kufirisika.. Wanachokifanya sasa ni kurudisha pesa zao tu...

Ukilipa ndio baasi.... La msingi km wanakudai we kausha tu usiwalipe teena hawana watu wazuri wa kudeal na iyo situation.

Ugomvi wao na tra haukutakiwa uwaaffect wateja....


Tuwatapeli tu na sisi
Kufa kufaana.....!!!!!
 
Mm wameniwashia moto juzi wamenipigia simu sema ni mdada nikaogopa ila namba nimechukua lazma nikaimbishe Mungu akinijalia kulipa sio kwa biti zile
 
Nimeamka tu nakutana na ujumbe huu.

Je wewe ni mmoja kati ya waliotumia vibaya kitambulisho kujisajili kwenye mfumo wa kukopa pesa Tala Tanzania. na kukaidi kurejesha? Jukumu letu la kukumbusha na kukutahadharisha kuhusu mkopo wako tumelitimiza ipasavyo. Tala Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka husika na vyombo vya habari hatutosita kukutangaza kama Mdaiwa Sugu, Tapeli na kukuchukulia RB, hii itakuchafua Hadhi na Taswira yako kwenye Jamii, Lipa deni ndani ya masaa 24 kuepuka fedheha hii.

Nina Deni lao Kama 170k vyuma vmekaza siwezi kurudisha njia gani kuwakwepa wanatishia amani
 
Mkuu mimi nilikuwa ninadaiwa 140k sasa ikawa kwenye kurejesha nazidisha kiwango ili mkopo wangu ukue,waliponichafua ni pale nimewalipa 160k nikitegemea ntaikopa tena lakini wapi.
Walilomba pesa yote na mkopo hawakunipa.
Nasemaje,km hauna usiwalipe ila km unayo ya mchezo walipe.
 
Mkuu mimi nilikuwa ninadaiwa 140k sasa ikawa kwenye kurejesha nazidisha kiwango ili mkopo wangu ukue,waliponichafua ni pale nimewalipa 160k nikitegemea ntaikopa tena lakini wapi.
Walilomba pesa yote na mkopo hawakunipa.
Nasemaje,km hauna usiwalipe ila km unayo ya mchezo walipe.
Mkuu hapa nimejificha chini ya kitanda . Sina mawe
 
Mikwara tu hiyo..
Mimi deni lao limebaki 180,000/=
ila sijatumiwa ujumbe wowote na muda wa kulipa umepitiliza..

Nimeamiaa Tigo nivushe, nako nawavutia Maji marefu..

Watu wanasema deni halimfungi mtu.
Hali tete watuvumilie ila sio kutishana
 
Utajisikiaje majina yako yote kuorodheshwa kama mdaiwa sugu?...
Madhara yake yanaweza kua makubwa sana kwako. Deni lako dogo la tala lisikuharibie kazi, biashara,familia au utu wako.
LIPA jioni hii kuepuka fedheha
Namba ya kampuni mpesa 888111
Tigo pesa 888000
Namba ya Kumbukumbu Ni Namba Uliyo Jisajilia TALA
Wananidai 130k
 
, utajisikiaje majina yako yote kuorodheshwa kama mdaiwa sugu?...
Madhara yake yanaweza kua makubwa sana kwako. Deni lako dogo la tala lisikuharibie kazi, biashara,familia au utu wako.
LIPA jioni hii kuepuka fedheha
Namba ya kampuni mpesa 888111
Tigo pesa 888000
Namba ya Kumbukumbu Ni Namba Uliyo Jisajilia TALA
Wananidai 130k
Haaaah haaaah haaaah Mimi nadaiwa 150k wametuma meseji hadi wamechoka sasa wananiomba niwe nalipa kwa installments kwamba kila siku 15k eti kwa siku 10 niwe nimemaliza deni
 
Ndg yangu katumiwa huu ujumbe na tala. anadaiwa sh 45,000 kama mkopo wao.

""TALA,Leo tarehe 16/05/2019 tumetuma na kutangaza taarifa za wadaiwa sugu wenzako na wadanganyifu wa TALA watano kati ya 30 kwenye mabenki 52,saccos,vicoba vyote vilivyoko Tanzania,na kuwatangaza kwa watu binafsi wasikopeshwe tena daima. wewe na wenzako 25 mliobaki tumepewa ruhusa na tuna RB kwa ajili ya kuwashughulikia kikamilifu ikiwemo kuwafilisi kabisa.LIPA DENI LOTE LEO HII UKIFIKIWA NA ZOEZI HILI HATUTAKI LAWAMA KAMA WENZAKO WALIOKWENDA MAHABUSU. REJESHAMALIPO LEO""

My take:
Mwanzo wakati tala inaanza niliwapa taadhari juu ya wabongo hawakusikia. lakini hivi tala kwa nini wasitumie mbinu mbadala ya kutumia wasaka madeni wao?

Nimemuuliza jamaa yangu kwa nini halipi hicho kiasi kidogo anadai kuwa tala kama vile wamegawanyika,kwamba wanaomtumia meeesgae ni kupitia no 5 tofauti na wengine wanasema alipe kwao direct hali inayoonesha kuwa tatizo kwao wenyewe maana walisitisha huduma za kukopesha kabisa,hawana communication platform inayooleweka. huwezi wapata kwa njia ya email,simu au barua wanataka utumie app tu kuchat nao au wakupigie wao wanapotaka.
 
Wamekupigia wakasemajee
Akasema yeye ni muwakilishi toka unajua kuwa tunakudai hivyo Leo hii tunataka ulipe akaniambia nitajie Leo utalipa saa ngap nikamdanganya saa 8 akasema Fanya hvyo bila hivyo tutachukua hatua
 
Akasema yeye ni muwakilishi toka unajua kuwa tunakudai hivyo Leo hii tunataka ulipe akaniambia nitajie Leo utalipa saa ngap nikamdanganya saa 8 akasema Fanya hvyo bila hivyo tutachukua hatua


Hajapiga tena mpaka saizi kweliii
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom