Ushauri: Mke wangu hataki tukaishi kwa wazazi wangu ili tubane matumizi tujenge

Saif Mohamed

Member
Oct 2, 2013
49
49
Vipi mambo wakuu,

Wazazi wangu ni watu wazuri saana sio kama nawasifia ni watu wenye kupenda watu sana kupita kiasi na wala hawana issues na mtu yoyote wala hawana mpango na issues. Hata ndugu zangu ni watu wazuri vile vile hawana matatizo na mtu yoyote yule.

Brother wangu kanipa flat ili nikaishi pale bure, chini wanaishi wazee wangu mimi nimepewa juu ni flat ya kutosha na my brother yuko upande wa pili na family yake.

Sasa wife wangu hataki tukaishi pale kila nikifungua hii topic hataki hata kusikia kila nikimuuliza hanipi jibu namwambia twende tukaishi pale kwa mda ili tuweze ku save pesa ili tujenge nyumba yetu yote hayo hataki.

Naomba ushauri wenu wakuu bila jokes please.
 
Mkuu wazazi wako na mke wako wote ni binadamu na sio wakamilifu. Idea ya kukaa kwenu ni nzuri, ila kwasababu umeshaoa inabidi mkomae kutafuta vya kwenu tu. Unaweza kujijkuta unaleta ugomvi usiokuwa wa lazima.
By the way, ukiwa hapo unapolipa kodi utapata hasira za kujenga yenu tofauti na ukiwa kwenu unaweza kubweteka koz huna kurupushani za kulipa kodi.
 
Ameona kitu ambacho wewe hujakiona... Msikilize mkeo... Ikiwezekana muulize vizuri na akupe jibu kwa kina...

Wale ni wazazi wako hawawezi kukuzushia wewe maneno na hata wakifanya hivyo utawavumilia, ila kwa mkeo ni mtihani sana...


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom