Ushauri: Mhitimu nimepata wazo la kujiajiri jamani

Kama unapenda ulichosomea nadhani itakua vyema kujiendeleza kupitia hicho kuliko kuanza career mpya.
Hapo ulipo tayar una mtaji wa ujuzi ulopata chuoni.

Ushauri: Tafuta jinsi ya kuendeleza career yako.
Amesomea mambo ya afya. Sasa atajiajiri vipi ktk sekta hii? Unajua bei ya vifaa tiba wewe? Mwenyewe kasema kuwa ana laki 2 tu
 
Habari Wakuu.

Mjmi ni Graduate wa Diploma Ya Afya ila kwa kipindi chote nilichowahi kuwa shule nimekuwa nikiwaza ajira isije ikawa sehemu kubwa ya Maisha yangu.

Ninachomaanisha Hapa ni kuhusiana na suala la kufanya biashara na kilimo (kwa mbeleni) ila suala ninalowaza kwa sasa ninahitaji kufanya biashara Hadi Muda huu nina Laki 2 niliyoitafuta kwa jasho langu.

Kuhusiana na kufanya kazi kwa fani niliyosomea Sijawaza bado.

Naombeni Mawazo Yenu wakuu nifanye biashara gani!?

Japo nimewaza nifanye biashara zifuatazo.

1.Ninunue Brenda nianze kuuza Juice pamoja na matunda ya kuuza na kuchanganya.

2.Nimewaza niuzie viatu vya Spesho au vya mtumba(Mbezi Luis stend mpya ya mabasi)

Nimewaza Haya.

VIJANA TUKAJIAJIRI
Ideas ni trial and errors.

Jaribu idea zote unazopta,utapata the perfect idea from your own imagination.
 
Hasubiri serikali ndio maana kajiongeza, wanaosubiri serikali wapo wamerelax wanapitia pitia pages za ajira mitandaoni

Huyu kaamua ajiongeze, ajiajiri, unataka kuniambia kwa hiyo pesa yake aliyonayo kwa hicho alichosomea kinatosha nini?

Mleta Uzi ukipata sehemu nzuri kabisa juice ni Bora zaidi kuuza hasa wakati huu wa joto Kali

Ukikosa hiyo, wazo la pili ni jema Sana
Asante mkuu..

Hata hapa kwa sasa nafanya biashara ila sio yangu na ndio maana nimefikiria kuanzisha yangu kwa kuwa nimepata experience kidogo ya biashara so najua pakuanzia

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
 
Asante mkuu..

Hata hapa kwa sasa nafanya biashara ila sio yangu na ndio maana nimefikiria kuanzisha yangu kwa kuwa nimepata experience kidogo ya biashara so najua pakuanzia

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
We unajichelewesha kupata faida, au hasara namaanisha kuchoma mtaji na experience, anza mzigo wakoo mbona kama upo sure na unachoenda kufanya then unahitaji tena ushauri ushauri. Ushauri wangu ni huu usipokee Sana ushauri
 
Back
Top Bottom