Ushauri: mfanyakazi mwenzangu kamtia mimba mdogo wangu

Msigazi Mkulu

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
4,110
3,269
Nilimleta mdogo wangu wa kike toka kijijini ili ajifunze masuala ya ufundi veta. Sasa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni jirani yangu pia kamtia mimba wakati tayari ameshaoa na watoto wawili. Nahisi kuchanganyikiwa kwakweli. Naamini nitapata ushauri mzuri hupa.
 
Duhhh pole mkuu. Nahisi ushauri mzuri ni kumuita huyo jamaa na kukaa nae chini na kumwambia kuwa hauna mpango wa kuitoa hiyo mbimba so anatakiwa kusimamia gharama zote za ufundi za dogo na anatakiwa kutoa matunzo yote ya huyo dogo hadi pale atakapojifungua

ila kama ataweka ngumu basi hilo swala utalifikisha kwenye familia yake, akikataa basi huna budi kumweleza mke wake ukweli wa mambo ulivo na pia wazazi wake kama wapo karibu

Baada ya kumpa hizo options then mwachie muda aamue nini cha kufanya maana haiwezekani we umtunzie mke alafu ye anakula tu
 
Umechanganyikiwa kivipi mkuu?? Haujui taratibu za kufata au
 
Nilimleta mdogo wangu wa kike toka kijijini ili ajifunze masuala ya ufundi veta. Sasa mfanyakazi mwenzangu ambaye ni jirani yangu pia kamtia mimba wakati tayari ameshaoa na watoto wawili. Nahisi kuchanganyikiwa kwakweli. Naamini nitapata ushauri mzuri hupa.
Mdogo wako ana miaka mingapi
 
Mkuu, huyo siyo rafiki, wala.mfanyakazi mwenzako au jirani. Jirani na mfanyakazi mwenzio hawezi kufanya ujinga kama huo kwako.

Amemwaga ugali , wewe mwaga mboga hadi maji ya kunawa.

Unless otherwise , kama umewahi kufanya ufusika kama huo kwingine naye anajua siri zako basi kaa kimya kufa na tai shingoni ila kama your innocent aisee yaani mwagu tu mboga na maji ya kunawa.
 
Unless ulimpatia huyo mdogowako kwa ridhaa yako (kituambacho ni almost impossible) tofauti na hapo huyo mfanyakazi mwenzako hakuheshimu hivyo basi muonyeshe jamaa kwamba kagusa pabaya and atakua responsible accordingly mpaka pale future ya dogo itakapokua stable
 
Duhhh pole mkuu. Nahisi ushauri mzuri ni kumuita huyo jamaa na kukaa nae chini na kumwambia kuwa hauna mpango wa kuitoa hiyo mbimba so anatakiwa kusimamia gharama zote za ufundi za dogo na anatakiwa kutoa matunzo yote ya huyo dogo hadi pale atakapojifungua

ila kama ataweka ngumu basi hilo swala utalifikisha kwenye familia yake, akikataa basi huna budi kumweleza mke wake ukweli wa mambo ulivo na pia wazazi wake kama wapo karibu

Baada ya kumpa hizo options then mwachie muda aamue nini cha kufanya maana haiwezekani we umtunzie mke alafu ye anakula tu
Asante sana kwa mawazo mazuri.
 
Usimuite tena mfanyakazi mwenzio ni shemeji yako
Mkuu kuna shitaka lolote la Kubakwa Mdogo wako alishawahi kukuletea? au Kuna lalamiko lolote mdogo wako alishakuletea ? Umejuaje kama ni mjamzito au ana mimba ya Jirani yako na Mfanyakazi mwenzako? Kaka najua utachanganyikiwa kuulizwa maswali haya ila tambua huyo mdogo wako kafanya hayo kwa ridhaa yake kikubwa msaidie ila usifanye uamzi wake kama alikosea au kurubunikja na ukitumia nguvu nyingi kuliko busara unaweza mfanya Mdogo wako kuwa kilema ? Siyo kile cha maumbile ila kilema cha kuweza kupambana na hali yake maisha yake yote bado nipo macho nahitaji maoni yako
 
Back
Top Bottom