USHAURI: Mengi amuajiri Tido Mhando kama MD wa ITV/Radio One | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Mengi amuajiri Tido Mhando kama MD wa ITV/Radio One

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EL+RA=UFISADI, Jan 4, 2011.

 1. E

  EL+RA=UFISADI Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali imeamua kumtoa Tido Mhando kama director-general wa Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) kama adhabu kwake kutokana na kuruhusu midahalo ya wagombea Ubunge na Urais wa vyama vya upinzani iendelee TBC baada ya CCM kujitoa yenyewe.
  Eti kina Makamba wa CCM wanamlaumu Tido kuwa alitoa airtime kubwa kwa wagombea wa upinzani na kuifanya CCM ipoteze viti vingi vya ubunge na kura za Urais.
  Tido alisimama kidete na kusema kuwa lazima midahalo itaendelea pamoja na CCM kuamua kujitoa wao wenyewe.

  Kwa kipindi alichokuwepo TBC, Tido ameleta mabadiliko makubwa na mafanikio ya hali ya juu kwenye TV na radio ya serikali. Tido ameleta a broadcasting revolution kutokana na professionalism ya kazi ya uandishi aliyosimamia na aina ya utangazaji wa habari na vipindi vingine. Amefanya TV zote kubwa ziige mfano wa TBC. Kwa ubunifu wake, waandishi wote mahiri wa broadcasting wamehama kutoka private sector kwenda TBC.

  ITV imekuwa ikiongozwa vizuri na MD wake Joyce Mhaville. ITV inasemekana kuwa imekuwa ni chombo pekee ndani ya IPP Media ambacho kinaendeshwa kifanisi na kibiashara chini ya uongozi wa Mhaville.
  Hata hivyo, chochote kizuri hakikosi kasoro. Wakati Mhaville amesimamia vizuri mapato na matumizi ya ITV/Radio One, quality ya habari na vipindi imekuwa ikiporomoka kutokana na waandishi wazuri kukimbia na kubaki na sub-standard journalists.

  Mhaville anajua kusimamia vizuri mapato na matumizi ya kampuni, lakini wafanyakazi wa ITV/Radio One wanasema ni mtu mgumu sana kufanya naye kazi kutokana na attitude yake na PR yake na watu.
  Kwa msingi huo, wakati ITV/Radio One zimestawi kifedha na kuwa na mitambo ya kisasa chini ya uongozi wa Mhaville, vyombo hivi vimekuwa vikidumaa professionally.

  Unfortunately, hivi sasa ITV/Radio One is in serious decline in terms of the quality of news bulettins, programmes, viewership, etc kutokana na kuwa na waandishi ambao si professional na wenye low morale.
  Solution hapa ni kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kumuajiri Tido Mhando kama MD mpya wa ITV/Radio One ili alete mapinduzi yale aliyoyapeleka TBC.

  Mengi ampe promotion Mhaville ya mshahara na title na kumfanya chairperson wa IPP Media, mwenye kazi ya overall supervision ya media zote za IPP akitilia mkazo The Guardian Limited ambayo ina matatizo makubwa ya uongozi, kifedha, professionalism na mengineyo.

  Tido Mhando akipewa free hand kuiendeleza ITV/Radio One, anaweza kuleta mapinduzi makubwa sana, haswa ukizingatia sasa tunaelekea kuungana zaidi chini ya East African Community (EAC).

  Serikali ina lengo la kumuweka mtu kama Clement Mshana wa Maelezo kuwa DG mpya wa TBC ambaye atakuwa pro-CCM, pro-government and anti-opposition. Matokeo yake ni kuwa watazamaji wataikimbia TBC kwa mamilioni na kuhamia private TV stations. Huu ndiyo wakati wa kuwakamata watazamaji na MD mbunifu kama Tido.

  But, Mengi has to act fast, nasikia Edward Lowassa anataka kumuajiri Tido kwenye TV yake huko Arusha.
   
 2. njoro

  njoro Senior Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umenena jomba,hata mimi nilikuwa na wazo hilo hlo
   
 3. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tido ajiajiri....kuajiriwa kumetosha...atumie ujuzi na taaluma aliyonayo naye kuajiri.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bora ajiajiri mpaka hapa alipo fikia inatosha nayeye aanzishe kampuni yake sasa lakini nawasiwasi jamaa wanaweza kubana
   
 5. n

  nndondo JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna program gani ya TBC mnayoizungumzia kwa kutia fora na kupendwa na watu? Tido yeye yuko radhi amuajiri mtu yoyote ili mradi katoka ITV. Tido hana viwango vya ITV mwacheni Mhavile aliyekijenga hicho chombo afanya kazi yake. Hivi mnaongelea Tido kuibadilisha TBC mbona mnafumbia macho madudu yake kibao. hebu tuelezeni TBC imesogea vipi? Inamaana hamkusoma taarifa ya mkaguzi mkuu? hamjui kwamba hakuna mishahara mpaka wanakopa kwenye SACCOS? kampuni imebaki ya watu wawili yeye bwana mkubwa na susan mungy hata safari za ma broadcaster bwana mkubwa na bibie wanatinga, wamegeuzai TBC kiosk chao cha kufurahia dunia. TIDO aliingia na kuchochea makundi na kuvunja kabisa ushirikiano na ITV, hakuna nafasi kwa TIDO huko labda aende STAR na Channel Ten kwa mafisaki.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tido hawezi kufanya kazi chini ya Mengi.
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Usiaje mbachao kwa msala upitao!
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sure ustadh,its better akijiajiri maana hata sector binafsi watamzingua,si unaona jinsi watendaji walivyokimbia ghafla pale ITV/RADIO ONE,
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Kwanza alituibia the comedy huyu bwana.
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  tido na ITV thubutu, mmesahau sakata la kuonyesha FA and Europa League na kwa kiasi kikubwa tido amefanya aliloweza kuicripple ITV na sector binafsi ya habari. sidhani kama itawezekana kwenda huko.
   
 11. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tido hawezi kufanya ITV/Radio one,
  Ningependekeza Tido angeenda pale Star tv, maana nadhani baada ya uchaguzi kimekuwa ni chombo hakiegemei upande wowote. Kwa ilivyo star tv angeipeperusha vilivyo na inge-lead other tv stations in the country.
   
 12. sbilingi

  sbilingi Senior Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi unadhani tido aliboresha tbc kwa pesa zake, aliwezeshwa ndo maana akaweza kufanya aliyofanya. alifanya kwa gharama ambazo nadhani serikali iliamua kuwekeza kwayo. ukitaka kuamini hili mengi amuajiri tido kama ataweza kuifanya itv kama tbc. inahitaji pesa baba.
  bwana tido alihitaji kulipwa mil. 14 na serikali je mchaga ataweza kumpa kitita kama hicho?
   
 13. sbilingi

  sbilingi Senior Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakuunga mkono na hii itadhihirisha kama kweli tido ndiyo aliyeboresha tbc au fedha za serikali ndizo zilizomuwezesha kufanya hivyo.
   
 14. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  arudi zake bbc
   
 15. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  RM hawezi kumuajiri TM kwa sababu tayari pale kuna Mhavile na zaidi ya yote vyombo vya habari vya IPP havijui kukaa na wafanyakazi wake ndio maana mnawaona wako huku mara kule.
   
 16. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  mbona Clauds wameweza akope million mitano aanzishe Redio yake tutaipenda kama ilivyokuwa BBCna TBC1, yeye bado kichwa na aneshimika kimataifa, au aende TV Mlimani kwa wasomi maana Mengi walishakorofishana na mgogoro wa kuonyesha Mipira ya kimataifa , najua mengi anaweza sahau maana alishawishika na ela za RA ndio maana saga ya Ze Komedi RAalihusika sana
   
 17. nyondoloja

  nyondoloja Senior Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  wasomi wetu tz wajifunze kutumiwa vibaya wakimwagwa wanakosa pakukimbiria wengiwamesomakwakodizetu wararahoi wakipatamadaraka wanatusahauwanyonge sikuwakimwagwa tunakuwanao inatakiwambadirike tunawategemeawasom irabadomunatuperekasiko muwewatetezi wa wanyonge msiwe chanzo cha kunyonga wanyonge cheoni....... Nawasii wenyevyeo (ukipatakazi iwenisehem yakujengamahusianomazuri na jami usigeuze mahara pakujengachuki najam wakimwagwautakosapakuanzia
   
 18. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mengi hawezi kumuajiri Tido kwa kuwa Mengi anapenda cheap. Watumishi wake kila siku wanamkimbia kwa kuwa hawalipi vizuri. In short, Mengi ni Kabaila katika sekta ya habari. Kazi mtafanya, malipo mpaka mumlambe miguu. Hukumbuki sakata lake na SAKINA DATOO?
   
 19. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Eti Tido aliletwa TBC na Lowassa? Kama ndivyo si rahisi kwenda ITV.

  Naunga mkono wanaosema ajiajiri. Akope benki aanzishe kituo cha Redio au TV. Wabongo wamezoea kupenda kuajiriwa tu.

  Iwe challenge kwake...
   
 20. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi watu mnamsifu Tido kwa sababu katoka TBC au utendaji wake ulikuwa mzuri? Mimi binafsi naona hakuonesha professionalism kwa kubanwa na system. hivyo ni sifa za marehemu mtu akifa sifa zote mnampa.
   
Loading...