USHAURI: Mbowe, Lema wajisalimishe ubalozi wa Marekani

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Sote tunajua uhasama uliopo kati ya Jeshi la polisi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na sote tumesikia matamshi ya pande zote mbili:

Kuwa, CHADEMA wanawatuhumu polisi kuhusika na ulipuaji bomu Arusha trh. 15/6/2013, na kuwa mara kwa mara polisi wamekuwa wakiingilia uhuru wa wananchi kukusanyika hasa wanachama wa CHADEMA, na kuwa CHADEMA hawana tena imani na jeshi hilo, kwa vile badala ya kuwalinda limekuwa likiwaumiza na kuwaua wanachama wake.

Na kwa upande mwingine Jeshi la polisi kupitia kwa mkuu wa oparesheni wa polisi Chagonja limekuwa likijitetea kuwa halihusiki na madai yanayotolewa na CHADEMA, na kuwa hii si mara ya kwanza CHADEMA kulituhumu jeshi hilo.

Kwa hiyo basi, kwa vile Jeshi la polisi linalotuhumiwa ndilo linalounda tume ya kuchunguza tukio hilo chini ya Chagonja, kwa akili ya kawaida tu CHADEMA haiwezi kuliamini na hata kutoa ushirikiano, na basi sioni mantiki ya Mbowe, Lema na wengine kuwapelekea ushahidi au kujisalimisha kwa watu wanaowatuhumu kuwaua.

Ushauri wangu binafsi, Mbowe na Lema ambao inaoneka walikuwa walengwa wakuu wa lile bomu kwa maana ya kuuwawa, wakaombe uhifadhi kwenye balozi za Marekani au British High Commission hadi watakapohakikishiwa usalama wao.

Naomba kuwasilisha.

"Tafadhali MODS naomba msiunganishe thread hii ili nipate maoni ya wana JF"
 
Wazo zuri,polisi na serikali ndio wauaji hawawezi kuwatendea haki,maana wana hasira nao baada
ya kuwakosa juzi'
 
Kiongozi!

Hizo nchi zote ulizo zitaja, zinafukuzia maslahi ya maliasili ya Tanganyika kwa udi na uvumba. Hivyo hakuna lolote watakalo saidia zaidi ya kuwaambia kwamba sababu zao hazija jitosheleza. Kumbuka ni juzi kati hapa, hao jamaa wame mpa promo FastJet kwa tuzo kibao kuhusu Demokrasia na mazaga zaga mengine. Ili mradi kumvimbisha kichwa jamaa aweze kuachia maliasili ki-ulaini,

Kwa mimi nisinge shauri hivyo.

Afadhali hata na balozi za skandinavia au Ujerumani.
 
kwa hiyo nani atawahakikishia usalama wao kama si hao hao polisi? ufumbuzi wa kudumu ni kuwa Mbowe na Lema waombe radhi kwa jeshi la polisi na wananchi kutokana na usumbufu uliojitokeza. pia wajisalimishe polisi ili wafikishwe mahakamani mapema iwezekanavyo ili wapate staili yao
 
Kiongozi!

Hizo nchi zote ulizo zitaja, zinafukuzia maslahi ya maliasili ya Tanganyika kwa udi na uvumba. Hivyo hakuna lolote watakalo saidia zaidi ya kuwaambia kwamba sababu zao hazija jitosheleza. Kumbuka ni juzi kati hapa, hao jamaa wame mpa promo FastJet kwa tuzo kibao kuhusu Demokrasia na mazaga zaga mengine. Ili mradi kumvimbisha kichwa jamaa aweze kuachia maliasili ki-ulaini,

Kwa mimi nisinge shauri hivyo.

Afadhali hata na balozi za skandinavia au Ujerumani.

si utaje tu kuwa nchi za waliberali?
 
Naomba kujua kama hizo Balozi/Nchi zina/zitakubali Chadema iingie madarakani, kwani navyojua CDM inapiga ufisadi na ikiingia madarakani mikataba yote ya kifisadi itafutwa.
Je Wanaweza kwenda pia ubalozi wa China?
 
Wazo zuri,polisi na serikali ndio wauaji hawawezi kuwatendea haki,maana wana hasira nao baada
ya kuwakosa juzi'

naona chadema mnaweweseka sana baada ya jana kutunguliwa na mabomu mpaka wengine wakawa nguruwe jana
 
Sote tunajua uhasama uliopo kati ya Jeshi la polisi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na sote tumesikia matamshi ya pande zote mbili:

Kuwa, Chadema wanawatuhumu polisi kuhusika na ulipuaji bomu Arusha trh. 15/6/2013, na kuwa mara kwa mara polisi wamekuwa wakiingilia uhuru wa wananchi kukusanyika hasa wanachama wa Chadema, na kuwa Chadema hawana tena imani na jeshi hilo, kwa vile badala ya kuwalinda limekuwa likiwaumiza na kuwaua wanachama wake.

Na kwa upande mwingine Jeshi la polisi kupitia kwa mkuu wa oparesheni wa polisi Chagonja limekuwa likijitetea kuwa halihusiki na madai yanayotolewa na Chadema, na kuwa hii si mara ya kwanza Chadema kulituhumu jeshi hilo.

Kwa hiyo basi, kwa vile Jeshi la polisi linalotuhumiwa ndilo linalounda tume ya kuchunguza tukio hilo chini ya Chagonja, kwa akili ya kawaida tu Chadema haiwezi kuliamini na hata kutoa ushirikiano, na basi sioni mantiki ya Mbowe, Lema na wengine kuwapelekea ushahidi au kujisalimisha kwa watu wanaowatuhumu kuwaua.

Ushauri wangu binafsi, Mbowe na Lema ambao inaoneka walikuwa walengwa wakuu wa lile bomu kwa maana ya kuuwawa, wakaombe uhifadhi kwenye balozi za Marekani au British High Commission hadi watakapohakikishiwa usalama wao.

Naomba kuwasilisha.

"Tafadhali MODS naomba msiunganishe thread hii ili nipate maoni ya wana JF"

MKUU kwanini unakuja na wazo hili unaona nini mbele yao mh.lema na mbowe ufafanuzi tafadhali
 
Naomba kujua kama hizo Balozi/Nchi zina/zitakubali Chadema iingie madarakani, kwani navyojua CDM inapiga ufisadi na ikiingia madarakani mikataba yote ya kifisadi itafutwa.
Je Wanaweza kwenda pia ubalozi wa China?

mie naona waende tu kwenye mabanda ya kiti moto watasalimika kama alivyofanya lema jana. over
 
MKUU kwanini unakuja na wazo hili unaona nini mbele yao mh.lema na mbowe ufafanuzi tafadhali

kambi ya dr slaa na zito kabwe wamejipanga kuwalipua kwa mabomu kutake advantage ya ugomvi wa watu hao na polisi. si unajua kuwa ukikubali kula lazima ukubali pia na kuliwa?
 
Bepari hana cha afadhari eti afadhari ujerumani! Unawajua ujerumani wewe?
 
Bado hatujafikia kuomba hifadhi, maana ya hilo unalosema maana Mbowe na Lema wametishiwa maisha ma serikali kitu ambacho si kweli kwa sasa. Bado tuna muda pia kwa pande zote mbili kujisahihisha couz kila upande unamapungufu makubwa sana. Hasa jeshi la polisi, wamekuwa na Tuhuma nyingi ambazo hazina majibu dat while sometime hao viongozi wa CDM wanapoteza imani kabisa na jeshi la polisi.
 
Mbowe, lema wajisalimishe ubalozi wa Marekani= Al qaeda, Al Shabaab wajisalimishe ubalozi wa Marekani.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
mie naona waende tu kwenye mabanda ya kiti moto watasalimika kama alivyofanya lema jana. over

Waweza ktupatia CV yako hapa maana ninaona mawazo yako ya ajabu ajabu hutofautiani na Mwigulu, Npe na mafisadi wengine wengi. Au nawe uko kwenye Lumumba project.
 
MKUU kwanini unakuja na wazo hili unaona nini mbele yao mh.lema na mbowe ufafanuzi tafadhali
Kwanza, ukiangalia kwa umakini lile bomu lililenga kumuumiza au kumuua kabisa Mbowe na ukirejea sms ya mkuu wa mkoa Arusha kuwa atamtafuta Lema kwa njia nyingine, basi utakubaliana na mimi kuwa anaweza kufanywa chochote na serikali hii.

Pili, kujisalimisha kwenye balozi si woga bali ni strategy moja ya kisiasa ya kuujulisha ulimwengu kuwa kuna kitu kinafanyika Tanzania kuliko kulia huku umejifungia chumbani, kwa njia hii wapinzani wengi kutoka nchi mbalimbali wamefanikiwa kuyarubuni mataifa makubwa kuingilia kati na kusaidia panapohitajika.
 
ngoja tuangalie inavyokuwa , kuna mwendawazimu ameshaingia humu kuchakachua maudhui ya hii thread kwahiyo nawaomba msimjibu kwa lolote. kama unaoga mtoni kichaa akakimbia na nguo zako huwezi kumkimbiza uchi ,ukifanya hivyo wewe utaonekana ndiyo kichaa zaidi.
 
Ubalozi utawakabidhi polisi kiulaini sana, wamarekani sio wapumbavu mpaka wakaharibu uhusiano wao kwaajili ya Mbowe na Lema. Tanzania ni muhimu sana kwao kuliko hao wawili. Hii ni serikali ya Kikwete bana.
 
Nashauri wakimbilie ubalozi wa Urusi. Hao uliowataja wana interest kubwa na Serikali/CCM hivyo hawatatoa ushirikiano mzuri.
 
Back
Top Bottom