USHAURI: Mbowe, Lema wajisalimishe ubalozi wa Marekani

0
 
Sote tunajua uhasama uliopo kati ya Jeshi la polisi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na sote tumesikia matamshi ya pande zote mbili:

Kuwa, CHADEMA wanawatuhumu polisi kuhusika na ulipuaji bomu Arusha trh. 15/6/2013, na kuwa mara kwa mara polisi wamekuwa wakiingilia uhuru wa wananchi kukusanyika hasa wanachama wa CHADEMA, na kuwa CHADEMA hawana tena imani na jeshi hilo, kwa vile badala ya kuwalinda limekuwa likiwaumiza na kuwaua wanachama wake.

Na kwa upande mwingine Jeshi la polisi kupitia kwa mkuu wa oparesheni wa polisi Chagonja limekuwa likijitetea kuwa halihusiki na madai yanayotolewa na CHADEMA, na kuwa hii si mara ya kwanza CHADEMA kulituhumu jeshi hilo.

Kwa hiyo basi, kwa vile Jeshi la polisi linalotuhumiwa ndilo linalounda tume ya kuchunguza tukio hilo chini ya Chagonja, kwa akili ya kawaida tu CHADEMA haiwezi kuliamini na hata kutoa ushirikiano, na basi sioni mantiki ya Mbowe, Lema na wengine kuwapelekea ushahidi au kujisalimisha kwa watu wanaowatuhumu kuwaua.

Ushauri wangu binafsi, Mbowe na Lema ambao inaoneka walikuwa walengwa wakuu wa lile bomu kwa maana ya kuuwawa, wakaombe uhifadhi kwenye balozi za Marekani au British High Commission hadi watakapohakikishiwa usalama wao.

Naomba kuwasilisha.

"Tafadhali MODS naomba msiunganishe thread hii ili nipate maoni ya wana JF"

Kwa nini sio Ubalozi wa Indonesia au Brazil?
 
All local/international correspondents of international media are being on handouts from ccm that is why no news is available on such media.....

Duh yani pamoja na kuongea kiingereza kwenu koote bado tu Wazungu wanawachunia, kweli mwaka huu mbaya kwenu, sasa itakuwaje, kwa maana kwa Wazungu nako wanawapotezea, kwa wananchi nako wameshaanza kuwashtukia, Serikali nayo inabana, Bungeni Spika Makinda hamuelewani naye, Polisi wanaopaswa kuwalinda mnawashutumu kwa mauaji!

Sasa nyinyi huko mbele mtakuwa wageni wa nani?
 
Back
Top Bottom