Ushauri: Mbao nilizotumia kupaua nyumba zinaliwa na wadudu, nipake dawa gani kuzinusuru?

Wiwachu

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
809
923
Habari za wakati huu ndugu na jamaa, mimi ni mhanga wa tatizo la mbao za nyumba yangu niliyopaua miezi 9 iliyopita toka mwezi wa 9 mwaka jana ila kufika leo hii nasikia juu kwenye dali kelele za wadudu kama wanakula mbao asubuhi pia nikiamka naona kuna uchafu wa mbao kuliwa kama unga unga uliotoka juu

Wakati ni nazinunua mbao hizo niliambiwa ni za dawa zishapakwa tayari na zilikuwa ninaonekana na rangi kama kijani kwa mbali kuonesha zina dawa lakini ndo kama nilivowaambia zinaliwa na wadudu,, ni ipi njia nzuri ya kuzinusuru zisiliwe na kuoza mwisho paa la nyumba lisianguke na kupata hasara..

Je, kupaka dudukilker kutasaidia? na je bado ipo madukani hiyo dawa ya mbao ya dudukilker?

Kuna dawa nyingine ya kuweza kupaka mbao zikiwa juu ya paa tayari?

Je, kuna vifaa vya kupaka kwa kupuliza au kupaka kwa brush na lola la kuburuza kama wanavopaka ukuta nk?

Naombeni ushauri wenu kwa mtu mwenye uzoefu au aliyekwisha kutana na changamoto kama yangu.

Karibuni kwa michango yenu.
 
Paka tena dawa hiyo mbao zikiwa hapo hapo kwenye nyumba.
Zipo dawa rasmi za kupakwa zinauzwa maduka ya hardware au tumia Oil chafu. Kwangu mimi ninaona bora oil chafu, kwa kuwa haina ujanja ujanja mwingi kuliko hizo dawa rasmi ambazo unaweza kuuziwa feki kama sio mjuzi.
 
Mkuu oil chafu ndo ile iliyotumika kweny gari au pikipiki??
 
OK vipi ya pikipiki haifai au mpaka ya gari tu wajuvi mnasemaje ni kweli??
Kabla sijapiga bati, fundi alianza kupaka oil ya pikipiki ila nikawa naona kama ni nyepesi, hivyo nikaenda kununua oil ya magari, ni nzito sana, yaani ukipaka inanyong'onyea hadi ndani ya mbao! Mbao inakuwa nyeusi tii, halafu mdudu anakosa kabisa sehemu ya kudonoa mana ubao unakuwa umefunikwa na oil.

Mpaka leo hizo mbao mdudu hasogei.

Kabla ya kupaka oil nilimwambia fundi mapema, kwamba, nitatumia oil chafu hivyo akae analijua hilo, akakubali nikampa kazi.

Mafundi wengi hawapendi kutumia oil kwa sababu ya kuchafuka, ila oil chafu ni kiboko ya wadudu!
 
Paka tena dawa hiyo mbao zikiwa hapo hapo kwenye nyumba.
Zipo dawa rasmi za kupakwa zinauzwa maduka ya hardware au tumia Oil chafu. Kwangu mimi ninaona bora oil chafu, kwa kuwa haina ujanja ujanja mwingi kuliko hizo dawa rasmi ambazo unaweza kuuziwa feki kama sio mjuzi.
Kwenye magarage hua wanauza oil chafu? au zinapatikana wapi
 
Kabla sijapiga bati, fundi alianza kupaka oil ya pikipiki ila nikawa naona kama ni nyepesi, hivyo nikaenda kununua oil ya magari, ni nzito sana, yaani ukipaka inanyong'onyea hadi ndani ya mbao! Mbao inakuwa nyeusi tii, halafu mdudu anakosa kabisa sehemu ya kudonoa mana ubao unakuwa umefunikwa na oil.

Mpaka leo hizo mbao mdudu hasogei.

Kabla ya kupaka oil nilimwambia fundi mapema, kwamba, nitatumia oil chafu hivyo akae analijua hilo, akakubali nikampa kazi.

Mafundi wengi hawapendi kutumia oil kwa sababu ya kuchafuka, ila oil chafu ni kiboko ya wadudu!
Mkuu ulipaka oil chafu mbao zikiwa chini au baada ya kupau..?
Je kama baada ya kupaua haikua changamoto sana wakat wa kuzipaka?
 
Vipi ndugu yangu oil chafu ili kusaidia tatizo lako na Mimi nitumie au kuda sawa nyingine ulitumia?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom