Ushauri: Mapenzi yake huvunjika kwa sababu ya kuwa mbali

kabon14

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
1,233
867
Habari wakuu,

Ni kijana smart tangu mwonekano, tabia na fikra pia ni mdogo kwangu kiumri hivyo Mara nyingi amekuwa akihitaji msaada wangu wa ushauri kila anapokuwa na tatizo na mimi kwa kadri ninavyoweza nimekuwa nikimpa msaada nikiwa kama kaka yake lakini kwa hili la Leo nimeshindwa kumpa msaada kwa wakati.

Anadai kuwa amewahi kuwa na mahusiano na zaidi ya msichana mmoja lakini kila anapoanzisha mahusiano mapya hutokea jambo ambalo humlazimisha kusafiri hivyo huwa mbali na partner wake (hii imemtokea katika kila mahusiano aliyowahi kuwa nayo)

Anasema baadhi ya mahusiano yake huvunjika kutokana na yeye kuwa mbali na mwenza wake kwa mda mrefu.

Anapokuwa kwenye mahusiano anakuwa mwaminifu sana lakini ikitokea akazidiwa na kuamua kuanzisha mahusiano mapya tu, safari hutokea ghafla na yeye hujikuta analazimika kusafiri.

Sasa anachohitaji ni kujua sababu ni nini?

N.B hajawahi kumuumiza yeyote kimapenzi.
 
Aache mawazo potofu..mbona hilo ni jambo la kawaida apo hajapata mtu sahihi.subra yavuta kheri.
 
Sababu anaokutana nao wote hawapendi mahusiano ya mbali mbali

Sasa cha kufanya hapo em mtumie picha zangu na mi nitumie zake
Tujaribu kufanya ile kitu ya kuitwa loveconnect

Mimi hata akisafiri akakaa miaka nane bado atanikuta namsubiri
 
Kuna uwezekano katika mawasiliano na wenzi wake, hasa anapokuwa mbali nao, akawa hawaamini au anawashuku, mwisho anaamua kukata uhusiano. Tatizo ni kutojiamini.
 
Kuamini mahusiano ya mbali ni kujichimbia kaburr mwenyewe
 
Mahusiano ya mbali yanahitaji uaminifu na uvumilivu mkubwa.

Nimeshashuhudia madereva wa safari za mbali wakiwa na mwanamke kila kituo,yaan wengine wanafamilia hata tatu mikoa tofauti na kila mwanamke anajua huyo ni mumewe halali(japo hawajafunga ndoa)

Hawa makonda wa mabasi ya masafa marefu aisee hawaaminiki(wanatongoza ovyo)
 
Kama anaona hilo ndo tatizo aoe mapema mama wa nyumbani, ikitokea safari inayomtaka akae mda mrefu huko basi amchukue na mkewe. Kuna familia zinazoishi hivi.
 
Sababu anaokutana nao wote hawapendi mahusiano ya mbali mbali

Sasa cha kufanya hapo em mtumie picha zangu na mi nitumie zake
Tujaribu kufanya ile kitu ya kuitwa loveconnect

Mimi hata akisafiri akakaa miaka nane bado atanikuta namsubiri
Sijui nije Pm ....
 
Hahahaha nipe picha zako nimtumie
 
Huyu atakuwa dereva wa masafa ya nje ya nchi hapo avute jiko la moja kwa moja badala ya kutegemea mahusiano ya kuvunjika kila siku maana akioa ataweza kumwita mke wake wakae karibu maana mke atakuwa huru kuambatana nae
 
Mahusiano ya mbali yanahitaji uaminifu na uvumilivu mkubwa.

Nimeshashuhudia madereva wa safari za mbali wakiwa na mwanamke kila kituo,yaan wengine wanafamilia hata tatu mikoa tofauti na kila mwanamke anajua huyo ni mumewe halali(japo hawajafunga ndoa)

Hawa makonda wa mabasi ya masafa marefu aisee hawaaminiki(wanatongoza ovyo)

Asifiae mvuaa
 
Back
Top Bottom