Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Najua unapenda sana Kushughulika na kuhakikisha kuwa Jambo fulani linatendeka na linaenda unavyotaka Wewe ila kuna maeneo mengine unatakiwa upime au ujipime Kwanza hasa ukizingatia Usalama wako na jinsi Jamii Kubwa ya Watu hasa ' Maadui ' zako ulionao hapa Mkoani Dar es Salaam.

Binafsi nilishangaa sana ile Jana tena ukiwa barabarani na kuna Watu wengi wa kila aina ' ukijiachia ' kwa kutoka katika Gari yako na Kujumuika nao huku ukizunguka huku na kule pasipo na hata Wewe kuwa na jicho la pili kwa ' Usalama ' wako.

Najua unalindwa tena pengine kuliko hata wanavyolindwa ' VIP's ' wengine nchini ila binafsi nadhani kwa hali iliyopo na hasa ' Chuki ' za Watu dhidi yako ( nikimaanisha Maadui ) zako uliowatengeneza hukupashwa ' Kujiachia ' vile kwani lolote lingeweza kutokea Kwako na pengine leo tungekuwa na habari nyingine mbaya.

Mpaka sasa nawaza RC Makonda unajiamini vipi hadi unapenda ' Kujichanganya ' na Watu tena wale ' Changanyikeni Clan ' ambamo ndani yao humo kuna ambao wanakupenda na wasiokupenda pengine kama nia mbaya ingekuwepo dhidi yako jana basi ingekuwa rahisi Kwao ' Kutekeleza ' jambo lao.

Ushauri wangu Kwako Siku zingine kabla ya kwenda mahala hebu jaribu kupima ' Upepo ' Kwanza na ' Kutafakari ' kwa marefu na mapana hasa hasa ukizingatia suala zima la ' Usalama ' wako. Ila ningekuwa ni Mimi GENTAMYCINE jana ile nipo nawe kama sehemu ya ' Ulinzi ' wako kamwe nisingekuruhusu uwe unatokatoka vile katika Gari yako na kuja ' Kujichanganya ' na Watu ambao Kwanza huwajui vyema, akili zao wengine wanazijua wenyewe na wenye kuwa tayari pia kufanya lolote na kuja ' Kujutia ' baadae huku pengine Wewe ukiwa ' Mwaisela ' au ' ICU ' au umeshaungana na ' Mtani ' wangu katika ' Identity ' mpya ya Marehemu fulani.

Acha kujiamini sana na kuwa makini tafadhali. Yangu ni haya tu kwa leo na ukiona nakuambia hivi jua nakupenda na nakutakia maisha marefu na mema pia. Bado wale ' Maadui ' zako hawajalala usingizi na pia huwezi jua sasa wanajipangaje dhidi yako hivyo nawe pia yakupasha muda mwingi kuwa makini na ' Kujilinda ' huku pia ukipunguza sana kupenda ' Kuonekana ' mbele mbele. Kwani ile jana ambapo nawe ulikuwa ' Msafarani ' ungekuwa tu unatoa ' Maelekezo ' wa Watendaji wako hasa wa Kiusalama / Kiitifaki waliokuwepo pale au uliokuwa nao wasingefanya kile ulichokuwa unataka Kifanyike?

Yafanyie Kazi haya maelezo yangu ila ukiona hayakufai basi niachie tu mwenyewe.

Nawasilisha.
Analindwa na hirizi
 
Habari za kazi.

Pole na majukumu mazito ya mkoa wetu wa Dar es salaam, wote tunaona ni kwa namna gani unapambana na kujituma kwa dhati kuijenga Dar es salaam mpya.

Mheshimiwa Paul Makonda kwa muda sasa sisi kama wahitimu wa vyuo vikuu tuishio katika mkoa wako ambao hatujafanikiwa kupata ajira serekalini au kwenye sekta binafsi , tumekumbwa na changamoto kubwa nyingine ambayo ni umiliki wa ardhi .

Ni wazi kuwa kwa kipato tunachokipata kwa sasa hatuna uwezo wa kununua kipande cha ardhi kwa Pesa taslimu kwa mfano mil 5, 7 , 10, 15 n.k.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ni rai yetu sisi wahitimu wa vyuo vikuu kama wananchi katika mkoa wako utuandalie utaratibu wa kupata ardhi na tulipe kwa installment .

Upo uwezo wa kujipatia kipande cha ardhi kama utatuwezesha kulipa kwa installment, mheshimiwa tunafahamu fika unatujali sana wananchi wa mkoa wako, sisi wahitimu wa vyuo vikuu tunalitambua hilo.

Nafahamu fika wapo watakao dai kwanini tusiombe ajira kwanza, Mheshimiwa mkuu wa mkoa sisi wahitimu tunafahamu fika kuwa serekali inatutambua na itatukumbuka.

Wako katika ujenzi wa Taiifa

Frank Shedrack
Ilala-Dsm
0686 042 769
 
Huna lolote wewe ni mnafiki tu ! Mbona kuna kampuni nyingi hapo Dar zinapima viwanja na kuruhusu malipo kwa installment.

Mara mhitimu wa "vyuo vikuu", Mara huna ajira! Wewe ni ki.laza tu unapima upepo baada ya kuona Mkuu wa Mkoa Makonda anakurupukia petty issues kama hizo!

Ngoja kwanza Makonda amalizie kusajili ndoa Dar na zijadiliwe kwenye Mkutana wa SADC unaondelea " kwenye Mkoa wake" ndipo aje kuwashughulikia wahitimu wa vyuo vikuu msio na ajira mpate viwanja vya kulipia kwa installment!
 
Pole sana kuwa muhitimu wa chuo hakukufanyi uwe ombaomba. Leo hii RC aanze kushughulikia upate kiwanja? Mwisho utaomba matofari, cement na mengine mengi. Amka nenda kijijini katafute fulsa kijana.
 
Nasema hakuna, ni sawa na mama kwa mwanaye, hawezi kuyafuta mema ya mzazi wake, wala chochote juu yake.*
*Kitendo cha kumlea tangu akiwa tumboni, kumnyonyesha na kumfundisha lugha miaka miwili, akakua na kuufahamu Ulimwengu hakiwezi kufananishwa na chochote duniani.
Hata kama mama huyo atampiga na kumtusi vipi mwanaye lakini bado kosa lake haliwezi kufuta wema aliomfanyia.*

*Hivyo hivyo kwa Paul Makonda* ambaye leo hii ni Mkuu wa Mkoa, huyu amepigana vita kubwa kubwa zilizowashinda wengi, vita za Makonda ni sawa kama zile za Goliathi aliyetajwa katika Biblia, Masalakulangwa na Jing'weng'we waliotajwa katika simulizi za kale.
Makonda naye amesambaratisha makundi mbalimbali likiwemo maarufu kama kundi la Mafia la wauza madawa ya kulevya yalioangamiza vijana wa kitanzania na wengine kufungwa jela huko nje ya nchi, mfano nchini China, zaidi ya vijana takribani 200 walishitakiwa na wengine wamefungwa jela, nchini Brazil vijana wasiopungua 200 walishitakiwa na wengine wamefungwa jela, Afrika Kusini vijana wasiopungua 200 walishitakiwa kwa makosa ya biashara haramu na wengine wamefungwa jela, achilia mbali nchi nyingine na waliongamia na kushitakiwa hapa hapa nchini kwa sababu ya biashara hii haramu.

Jana, vyombo vya habari vimeripoti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesaidia watoto 60, wanaotoka familia masikini ktk Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Mkurugenzi mwendeshaji katika kitengo cha Moyo Profesa Mohamed Janabi amesema mapaka sasa watoto 30 kati ya 60 wamefanyiwa upasuaji ndani ya miezi mitatu na kadiri siku zinavyokwenda imeripotiwa kwamba, hadi sasa kuna zaidi ya watoto 500 wenye tatizo la moyo lakini wazazi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Pamoja na ripoti hiyo ya taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete imemshukuru Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuwajali watoto hao ambao anawalipia kila awamu watoto kumi 10.

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ameishukuru taasisi hiyo ya Moyo ya Jakaya Kikwete na vile vile ameishukuru Wizara ya Afya chini ya Waziri Mhe. Ummy Mwalimu kupitia Serikali chini ya Uongozi wa Rais Dk. Magufuli kwa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya matibabu kama hayo na kuongeza kuwa, anamshukuru Balozi wa Jumuiya wa Falme za Kiarabu kwa kumuunga mkono na kwa kuleta Madaktari Bingwa kutoka nje ya Nchi ili kuja kufanya upasuaji wa watoto hao wanaotoka familia duni za kimasikani.
Sambamba na hilo, Mkuu wa Mkoa Ndg. Paul Makonda amesema kwamba, mwezi wa 11 hadi wa 12 mwaka huu utakuwa mwezi wa kushukuru wananchi wa Dar es Salaam kwa namna wanavyotoa ushirikiano mbalimbali kwa serikali katika mkoa. Lengo kuu la tukio hilo ni kufanikisha upatikanaji wa fedha bilioni moja itakayokusanywa kutoka taasisi za kibenki, makampuni na wadau mbalimbali ili fedha hizo zikagharimie matibabu ya watoto hao.
Lakini pia, ameongeza kuwa, anatamani sana kuona watoto hao wanafurahi pamoja na jamii katika siku kuu mbalimbali zinazowakutanisha watu na kufurahi.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari, Makonda alikusia juu ya maswali mbalimbali yanayoulizwa na baadhi ya watu wanaohoji ni wapi Mkuu Makonda anapata fedha za kugharamia matibabu ya watoto na misaada mbalimbali anayoitoa kwa wahitaji/watu masikini?
*RC. Makonda amesema ya kwamba, "Nchi hii ni tajiri na watu wa nchi hii ni matajiri, wanachohitaji ni mtu mwaminifu, mwadilifu anayeomba fedha kwa matumizi sahihi."*

*Sasa nauliza, Mungu awape nini watanzania ikiwa vijana kama huyu Makonda wanafanya mambo makubwa ya kitume katika taifa hili?*
*Kuna kosa gani laweza kufuta wema anaoufanya Paul Makonda kwa watanzania?*
*Mimi nafikiri kama kuna jambo la kufanya ni watanzania kumuombea Makonda ktk njia zake na kumuomba pia Rais wa nchi Dk. John Magufuli ampe kiti/dhamanaa kubwa zaidi ya hapo alipo huyu "Paul Makonda" ili apate nguvu ya kuhudumia taifa zima akiwa kiongozi wa kitaifa. Hii ni kwa sababu, anayoyafanya Makonda si ya Mkuu wa Mkoa, kimkoa pekee, bali ni zaidi ya Mkoa.*

*Tumepata Rais mzuri, na tunapata vijana wazuri sana katika taifa letu, ni muhimu sana kuwashikilia kwa mikono miwili maana bahati haiji mara mbili mbili.*
 
Kuna watu ni maarufu kwa kupinga kila kitu ...!! yaani 'pinga pinga' wana mahusiano na mtaa wa ufipa pale k'ndoni ngoja wakuibukie.
 
Kwavitu vya msingi anavyofanya kusaidia jamii basi anastahili pongezi he is smart in that
 
Kuna watu ni maarufu kwa kupinga kila kitu ...!! yaani 'pinga pinga' wana mahusiano na mtaa wa ufipa pale k'ndoni ngoja wakuibukie.

Hata wauza unga waliwasaidia sana ndugu zao, na walitoa ajira kwa watu kutokana na uwekezaji wao. Mtu mwenye roho mbaya anayo tu hata akilazimisha kujisafisha haiondoi ukweli kuwa ni mtekeleza maovu.
 
Yote anayafanya kwa njaa zake, amekiri hivyo..

Nafasi kubwa huwezi kumpa Mtu mwenye njaa, ataisaliti Serikali.

Shetani pia ana mazuri yake ila atabaki kuwa shetani tu.
 
Bashite ni mnyang'anyi wa fedha kwa matajiri kwa kisingizio cha kuyoa misaada kwa watoto wenye matatizo.
 
Back
Top Bottom