Gwajima
JF-Expert Member
- Sep 6, 2018
- 253
- 406
Nawasalimu wana Jf, nawapa hongera kwa kutekeleza majukumu yenu na kufuatilia jukwaa hili pendwa hapa nchini, leo nina maoni yangu ambayo nadhani yanaweza kuwa na msaada mkubwa sana.
Sanaa ya Tanzania inalegalega kutokana na kukosa watu wenye uwezo mzuri. Siku za usoni watu wengi wamekuwa wakiwalaumu wasanii wa maigizo wa Tanzania almaarufu kama Bongo Movie kwa kukosa ubunifu katika kazi zao za sanaa jambo linalopelekea sanaa hiyo kudharauliwa na watu wengi. Tatizo ninaloliona mimi ni moja tu, wengi wanaoigiza ni watu wanaolazimisha fani yaani wamevamia fani kwa tamaa ya feha za haraka haraka.
Nasema wana tamaa kwakuwa wakikosa fedha basi utaona wanageukia muziki mara wanaweka picha chafu mtandaoni ilimradi tu wapate umaarufu na fedha za haraka haraka. Nataka niwaambie wasanii kwamba kipaji ni kipaji tuu na mwenye kipaji hatumii nguvu kufanikiwa katika jambo analolifanya.
Kwa maoni yangu, Bongo Movie inakosa watu wenye vipaji kama Mh. Paul Makonda ambaye anaweza kubadilika badilika na kucheza scene tofauti tofauti tena kwa ufanisi wa hali ya juu, Mf: Anaweza kuwa mkali, anaweza kulia ghafla tena akaonekana analia, anaweza kucheka, anaweza kuwa mtu wa watu nk. Kwa maoni yangu Mr Makonda ni aina ya wahusika wanaohitajika sana kuokoa sanaa ya Bongo Movie.
Tunahitaji sanaa yetu isonge mbele, nivema tuwatie moyo wale tunaodhani wanaweza kushiriki ktk kukuza sanaa yetu, naamini Mh Makonda ukiingia huko na kutoa Movie itauza Dunia nzima, hata mimi nitainunua, pia utapelekea taifa kupata fedha nyingi kupitia kodi.
Tafadhali, fikiria jambo hili.