Ushauri: Naomba nielezwe uhalisia wa ubora katika mabati ya gauge 28 na 30

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Heshima Mbele wadau,

Ningependa kupata real experience kwa wale ambao wamewahi kuezeka kwa mabati ya geji 30 tofauti ya ya geji 28.

Mimi nipo Dodoma, kuna kajumba kangu kamefikia hatua ya kuezeka. Mfukoni sipo vizuri sasa najiuliza niendelee na uamuzi wa kununua haya mabati ya geji 30 au mnasemaje wadau.

Ningependa kupata ushauri kwa wale waliowahi kupata experience halisia waweze kunisaidia kabla ya kufanya maamuzi haya ya kununua geji 30.

Natanguliza shukrani.
 
Kama nyumba yako inahitaji bati 80 basi nakushauri ununue nusu nusu kwa maana geji 30 nnunua bati na geji 28 nunua bati 40. Kitu kikubwa hapa utakuwa umepata faida mara mbili za geji zote.
 
Heshima Mbele wadau,
Ningependa kupata real experience kwa wale ambao wamewahi kuezeka kwa mabati ya geji 30 tofauti ya ya geji 28. Mimi nipo Dodoma, kuna kajumba kangu kamefikia hatua ya kuezeka. Mfukoni sipo vizuri sasa najiuliza niendelee na uamuzi wa kununua haya mabati ya geji 30 au mnasemaje wadau. Ningependa kupata ushauri kwa wale waliowahi kupata experience halisia waweze kunisaidia kabla ya kufanya maamuzi haya ya kununua geji 30. Natanguliza shukrani.
Kwema mkuu?
Gage 28 ni kubwa na nzito kuliko Gage 30, Gage 30 ni nyepesi na hua haishauriwi sana maeneo yenye upepo maana ni mepesi,
Ila kama unaona hali ya fedha si nzuri basi nunua hizo G30, angalia tuu usije nunua G32
 
haha poa mkuu nashukuru kwa ushauri, kwema kabisa
 
Kama nyumba yako inahitaji bati 80 basi nakushauri ununue nusu nusu kwa maana geji 30 nnunua bati na geji 28 nunua bati 40. Kitu kikubwa hapa utakuwa umepata faida mara mbili za geji zote.

Thanks for your comment mkuu
 
mkuu kama upo vizuri kipesa, nunua G28 maana ni ngumu na nzito pia utakuwa umechukua maamuzi ya kudumu na uhakika# hapo mpaka wajukuu kama sio vitukuu wataikuta. Japo hata G30 unaweza kutumia lakini kuna muda zitaomba kubadilishwa miaka ijayo kabla vitukuu na vining'ina hawajairithi.
N.b
Epuka G32 hizi maalumu kwa uzio wa ujenzi kama sheli au majengo makubwa na miundo mbinu mingine maana ni nyepesi sana pia haidumu kivile.
Nawatakieni mchana mwema wananzengo wote.
 
Ahsante sana mkuu kwa ushauri murua
 
Back
Top Bottom